Maalim Seif na mimi

Maalim Seif na mimi

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
MAALIM SEIF NA MIMI

Nakumbuka kama jana vile siku niliyokutana na Maalim Seif kwa mara ya kwanza uso kwa uso Starlight Hotel mwaka wa 1992 na aliyenijulisha kwake alikuwa Sheikh Khalifa Hamisi.

Siku zile Sheikh Khalifa alikuwa anaendesha gazeti la Mizani na mimi nikiwa mmoja wa waandishi wake.

Urafiki wetu ulianzia hapa na siku hii.

Maalim kipindi hiki alikuwa anaanza shughuli ya kuijenga CUF Tanzania Bara na haya ndiyo yakawa mazungumzo yetu.

Nilimuahidi Maalim kuwa kesho In Shaa Allah nitakuja na wenzangu na wao ni wakubwa kwa madaraka kunipita mimi kwa mbali sana ili tuwe na kikao kingine.

Yalipita mengi baina ya siku hii hadi kufikia uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka wa 1995.

Mimi ndiye nilimjulisha Prof. Ibrahim Lipumba kwenye mkutano mkuu wa CUF ndani ya Ukumbi wa Starlight Hotel kama mgombea Urais Tanzania Bara katika Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa vyama vingi 1995.

Hapa nataka nitie neno kidogo.

Hii ''mimi mimi'' naogopa msomaji asijenge picha kuwa nilikuwa kiongozi wa harakati hizi kwa hiyo mtu muhimu sana.

La hasha hii kumjulisha Prof. Lipumba kwa Kamati Kuu ya CUF ilikuwa ifanywe na mtu mwingine lakini ikatokea kuwa alipatwa na kifua na sauti ikamkaua ndipo aliponiomba mimi nifanye kazi hiyo.

Kuanzia hapa pia siku ile hadi kufika mkutano wa kufunga kampeni Kibanda Maiti, Zanzibar yapo mengi In Shaa Allah ipo siku wanahistoria watakuja kuyaandika.

Katika shajara yangu kuna mikutano miwili kwangu ilitia fora na ilinipa picha ya hali ya baadae ya CUF Tanzania.

Mkutano wa kwanza ni ule wa Tangamano Tanga Prof. Lipumba alipowakumbusha watu wa Tanga siku zao za nema na kuwaomba waitizame hali yao ilipofikia.

Wenyeji walitueleza kuwa haijapata kutokea mkutano uliojaza watu kama ule hata wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Mkutano wa pili ndiyo huu wa Kibanda Maiti Maalim Seif na Lipumba walipounguruma na kuwapa Wazanzibari matumaini mapya.

Nilikuwapo na kalamu yangu na camera yangu.

Ofisi yetu chini ya mti Malindi nje ya mkahawa maarufu ''The Passing Show.''

Hapo ndipo tulipokutana na wenzetu kutoka Zanzibar tukipeana taarifa.

Asubuhi siku ya uchaguzi ilinyesha mvua kubwa sana.

Nikawa najiambia kuwa huenda hii mvua ni ishara ya kheri kwetu.

Taarifa ya asubuhi ile ilitufurahisha sote.

Wataalamu wa mambo ya uchaguzi wamewaeleza CCM kuwa hawawezi kushinda uchaguzi huu.

Sisi kutoka Tanganyika tulifurahishwa zaidi na taatifa hii kwa sababu moja kubwa kuwa Maalim akishika serikali Zanzibar ikatulia hawa ndugu zetu watapata muda wa kutusaidia na sisi.

Sisi tulijua fika kuwa tuna kazi kubwa sana ya kupambana na CCM Bara na tukijua kuwa Prof. Lipumba hawezi kumwangusha Benjamin Mkapa lakini tulikuwa tunaweka msingi wa ushindi huko mbele tunapokwenda.

Hapa nataka niseme kitu sijapatapo kukisema.

Iko siku nilialikwa chakula nyumbani kwa Abbas Sykes na niliowakuta pale alikuwapo Hamza Aziz, Iddi Simba na Ahmed Rashad Ali.

Huu ndiyo ulikuwa wakati wa kampeni za uchaguzi.

Wazee wangu hawa waliniuliza maswali mengi sana.

Mimi nikiwaamini watu hawa ingawa nikijua walikuwa CCM.

Lakini kutokana na mazungumzo yetu huko nyuma walikuwa na kinyongo na chama chao jinsi kilivyogeuzwa na kuwa kinyume na matarajio yao.

Kuanzia siku hii hadi mwisho wa kampeni za uchaguzi ule wa 1995 nikaanza kupokea msaada kutoka kwa Abbas Sykes.

Nilijua bila ya Bwana Abbas kuniambia wapi msaada ule unakotoka.

Abbas Sykes wakati wao yeye ndiye akitumwa na TANU kupeleka fedha kwa Karume na ASP leo bila ya kutumwa anatoa msaada kwetu.

Yaliyotokea Zanzibar katika uchaguzi ule wa mwaka wa 1995 hakuna asiyejua.

Maalim kama ilivyotegemewa alishinda uchaguzi ule kwa kumbwaga chini Komando Salimini Amour.

Ali Ameir akaandika barua Tume ya Uchaguzi Zanzibar kukataa matokeo.

Inataka kitabu kizima kumueleza Maalim.

Nimehudhuria Kongamano la Maalim Seif Foundation.

Si kama mimi sikuwa najua kuwa Maalim Seif alikuwa mtu mkubwa sana lakini yale niliyosikia kutoka kwenye kinywa cha Rais Amani Karume yalizidisha yakini yangu.

(Nimepata kuandika makala, ''Maalim Seif The Greatest.'').

Lakini pia si hayo tu bali nimetambua uzito aliojitwisha Rais Amani Karume katika kufungua mlango mpya wa mustakbali wa kuitafutia Zanzibar amani ya kweli na ya kudumu.

Ingawa amani ya Zanzibar ni neema kwa watu wake lakini kwa wengine ni dhahma kubwa.

Kwao ni dhahma kwa kuwa wanajua hawatoweza kamwe kuirejesha Zanzibar nyuma na Wazanzibari watasonga mbele bila wao kupitia sanduku la kura.

Katika Kongamano hili kila aliyesimama kuzungumza alimsifia Maalim kwa kuinusuru Zanzibar na machafuko na kuipa amani.

Sikupata kuwa mbali na Maalim na uhusiano wetu huu ukajatiwa nguvu zaidi na mke wangu Bi. Riziki Shahari alipochukua nafasi ya uongozi katika CUF kufikia kuwa mbunge wa kuchaguliwa.

Nina mengi sana ya Maalim na nimekuwa nikiimpiga picha kila mara kwa takriban miaka 30 kwa ajili ya maktaba yangu na ilikuwa azma yangu nikae kitako na yeye tuandike kitabu cha chaguzi sita alizoshiriki na kushinda zote.

Nimeweka picha ya kwanza niliyopiga nimesimama mbele ya picha yeke kubwa iliyokuwako katika ukumbi wa mkutano wa Golden Tulip palipofanyika Kongamano la Maalim Seif Foundation.

Picha ya tatu siku Maalim alipopandisha bendera ya CUF Wazalendo kwenye ofisi ya mpya kwa ajili ya Wabunge wa CUF Mh. Riziki Shahari Kiongozi wa Wabunge wa CUF akiwa pembeni yake.

Picha ya pili ni mimi na Maalim.

Screenshot_20211108-140108_Facebook.jpg
 
Mkuu nakushukuru kwa kuyaeleza haya hadharani ili watu waijue historia ya nchi hii ktk Demokrasia. Kwa mfano mimi sikuwa najua kuwa Maalimu Seif alishinda ktk chaguzi zote sita za urais Zanzibar alizoshiriki.

Ombi langu kwako ni kuyaandika mambo haya yote kwa urefu na mapana yake ili kizazi cha sasa na kijacho viyatambue na hivyo kujua Taifa lilipitia njia ipi ktk kujenga Demokrasia yake.Ahsante.
 
Waislamu wana mchango mkubwa sana kwenye ujenzi wa Taifa letu, ila akiingia rais Mwislamu mambo huaharibika sana.

KIPINDI CHA MKWERE NCHI ILIKUWA SHAMBA LA BIBI. LEO TENA BIASHARA YA VUMBI IMEANZA KUSHAMIRI
 
Daaaa hii nzuri Mzee wangu Asante Kwa kushare historia hii adhimu tunajivunia uwepo wako hapa jukwaani!
🙏🙏🙏
 
Kuna kitabu Cha maisha ya Maalim au upo mpango wa kukiandika?
Je,ulisikia chochote kuhusu kitabu hicho kwenye uzinduzi wa Maalim Seif foundation?
 
..ccm wanamsifia maalim kwasababu amekufa.

..wakati yuko hai walikuwa wakimtukana matusi mabaya kwelikweli.
Sanaa...Musiba aliwahi kuandika ZITTO KABWE NA MAALIM SEIF WAGOMBANIA SHOGA!! Na walikuwa wanachekelea tu
 
Mohamed Said,

..nilitamani mngemuenzi Maalim wakati bado yu hai.

..walau mngemfanyia birthday mkacheka, mkamtania, na kumtuza / kumtunza.

..Nashauri watu wenu wazito msisubiri watangulie mbele za haki ndipo muutambue mchango wao.

..Najua hili ni jambo geni kidogo na halijazoeleka, lakini nadhani ni vizuri mkalijaribu.

..What you did is good, but I think it could have been better.
 
Waislamu wana mchango mkubwa sana kwenye ujenzi wa Taifa letu, ila akiingia rais Mwislamu mambo huaharibika sana.

KIPINDI CHA MKWERE NCHI ILIKUWA SHAMBA LA BIBI. LEO TENA BIASHARA YA VUMBI IMEANZA KUSHAMIRI
Yule mfu aliwalisha ugali na makalamata na ilibaki robo tu akaombe ugali wa yanga kwa Xi Jingpin.......
 
Waislamu wana mchango mkubwa sana kwenye ujenzi wa Taifa letu, ila akiingia rais Mwislamu mambo huaharibika sana.

KIPINDI CHA MKWERE NCHI ILIKUWA SHAMBA LA BIBI. LEO TENA BIASHARA YA VUMBI IMEANZA KUSHAMIRI
Yule mfu aliwalisha ugali na makalamata na ilibaki robo tu akaombe ugali wa yanga kwa Xi Jingpin.......
 
Back
Top Bottom