Zanzibar 2020 Maalim Seif Sharif Hamad unataka kutugawa Watanzania kwa faida ya nani?

.......Lakini zaidi ya nusu ya Wazanzibari wanaishi bara na wanavitega uchumi bara,na hilo linaweza kuwa kikwazo cha kuvunja Muungano,labda utabuniwa ushirikiano wa kindugu bila nchi hizo mbili kuingilia mambo ya nchi nyingine.
Hilo wala siyo shida.. mbona wahindi Wana vitega uchumi vingi Tanzania, na hakuna muungano kati ya Tz na India?
 
Hilo wala siyo shida.. mbona wahindi Wana vitega uchumi vingi Tanzania, na hakuna muungano kati ya Tz na India?
Mimi staki kumungunya maneno,tukivunja muungano kwa jazba,usishangae wakaja watu na visasi kuwa wazenj wote rudi kwenu.
Mimi nimeona General Idd Amin alivyowafukuza zaidi ya 70,000 wahindi Uganda.

Pia nimeona Kenya mara kunapokuwepo msuguano wa kisiasa kati ya Tanzania na Kenya,mara nyingi watanzania waliopo Kenya watakamatwa ,kupigwa na kuharibiwa mali zao.

Hii ni tabia yetu.
 
Muungano haujawahi kuenziwa kama unavyotaka tuamini. Ni wa kulazimishana tokea mapinduzi yake, kuna ushahidi wa kutosha wa Nyerere kuleta majeshi kupindua serekali ya Zanzibar na baadae kumtishia Karume lazima akubali muungano.

Haujawahi kuenziwa muungano huu, si na wazee wala sie vijana. Na sababu ya msingi ya sisi wazanzibari kuukataa sio ubaguzi, ni sababu ya kiuchumi. Umedhoofisha kila sekta ya uchumi wa visiwa vya Zanzibar na kuwatia watu ufukara.
 
Hitaji la siku nyingi la Wazanzibari waliokuwa wengi ni kulivua na hatimaye kuondokana na koti la muungano. Huu ndio ukweli wenyewe, ni sisi Watanganyika ndio ambao hasa tunauhitaji kwa udi na uvumba.
Jamani Matajiri wa pemba na wengine wa ZNZ watawekeza kwenye soko gani , na hizi nyumba zao zilizoko huku bara itakuwaje??
 
Umeandika upuuzi, yule anayesema hapa sitaleta maji mkichagua tofauti na chama changu huyo ndiyo anahubiri umoja na kusema watatumia dola kubaki madarakani ndiyo umoja? shame on you
Ungemuongeza na lingine hawa hawana aibu kbs. Hakuna kauli mbaya kama ya ubaguzi eti sileti maji au sileti umeme. Hizi siasa za ajabu sana.
 
Bara ubaguzi nje nje!
Ukichagua upinzani no maendeleo.
Maalim kamatia hapo hapo.
Usikubali Ukhanithi.
 
Kama muungano ulikuwa wa hiari, kwa nini uwashikie watu bunduki kulazimisha waendelee na ambacho hawakitaki tena?
 
Kwa faida ya Wazanzibari. Wazanzibari hawautaki Muungano na kama mnabisha, jaribuni kura ya maoni muone matokeo yake. Hata Watanganyika walio wengi hawautaki Muungano, maana hawaoni faida yake kwa mwananchi.

Anaeutakia mema Muungano hawezi kuzuia miradi ya Zanzibar. JMT imekataa kujenga Bandari Zanzibar, yule Mkuu wa mkoa wa Zanzibar zoba nae hana la kusema, Mafuta na Gesi mnataka kuyachukua wakati madini yenu hamtaki tugawane, Mkuu wa mkoa wa Zanzibar na Juj wa Majuj (Balozi Seif Sura Mbaya Ally Iddi) wake wameufyata, mpaka leo hamna kinachoendelea!

Muungano hautakiwi na Wazanzibari! Kila mmoja achukue mbao zake tu na kama mbuzi tu ale kutokana na urefu wa kamba yake. CCM imebaki kununualia watu mafuta na kugawa flana waende mikutanoni 😀
 
Anayetugawa ni yule anayesema usinichagulie huyu maana mtajuta sitowaletea maji!
 
Kwa namna ipi?
Nchi ndogo yenye mafuta na gesi asilia,utalii,bahari kwa uvuvi ,uchukuzi na kilimo cha mwani,kilimo cha mazao ya karafuu nk.Ni rahisi kujiongoza na kupiga hatua haraka zaidi kuliko kwenye muungano.
Wakiweza kuboresha sekta ya utalii kutoka watalii laki sita kwa mwaka kwa sasa hadi milioni 2 tu,ukiongezea na uchimbaji wa mafuta na gesi ni wazi nchi hii ndogo yenye watu million 2 itakuwa nchi tajiri kuliko nchi yoyote katika Afrika Mashariki.
 
Kwasasa ni nani anawazuia kufanya hicho unachosema?, Kuna yeyeote mwenye maamuzi juu ya hayo asiye mzanzibar?
 
Maalim Seif ndio alivyo. Ni mchochezi na mnafiki tangu enzi zake CCM.
Bila huu muungano angeweza kuzunguka bara kwa uhuru hadi watoto wake wakasoma huku?
 
Watanganyika ni WAKOLONI WEUSI hamna chochote machogo
 
Kila mwaka mnaleta majeshi yenu mnabaka na kuuwa Kisha mnatuita sisi ndugu zenu
 
Kwasasa ni nani anawazuia kufanya hicho unachosema?, Kuna yeyeote mwenye maamuzi juu ya hayo asiye mzanzibar?
Katika Muungano kuna mipaka yake.Kwamfano majeshi ni sharti la Muungano, majeshi yana gharama kubwa.Zanzibar akiwa nje ya Muungano anaweza kupata ulinzi kutoka baadhi ya mataifa makubwa bila yeye kugharimia kitu,labda taifa kubwa wao kugharimia ustawishaji wa Zanzibar.
 
Maalim Seif ndio alivyo. Ni mchochezi na mnafiki tangu enzi zake CCM.
Bila huu muungano angeweza kuzunguka bara kwa uhuru hadi watoto wake wakasoma huku?
Wakenya wangapi wanazunguka huko jee mumeungana nao nyinyi ni WAKOLONI WEUSI hamna lolote mumezoea kunywa damu za wazanzibar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…