Zanzibar 2020 Maalim Seif Sharif: Mwisho wa enzi, Pemba

Zanzibar 2020 Maalim Seif Sharif: Mwisho wa enzi, Pemba

Kwa data izo wapinzani warudi tu ulaya wakawaambie wale walio watuma kua mambo uku ni magumu Tanzanja haijaribiwi kizembe, maana siku zote mabeberu wanajivuniaga kututenganisha waafrika kupitia udini, ukabila, na ukanda, kwa Tanzania icho kiti hakipo yaani wazungu wanaumiza vichwa wafanye nini, ndipo wanaamua kutumia wanafiki kama tundu lissu, maalim na wenzie, hawatoweza kamwe ccm ni chama imara.
Quote ReplyReport Edit
 
Kwa umati huu naamini kabisa ndio Mwisho wake Maalim seifView attachment 1572153
Imebidi kwanza nicheke. Kwa mwenye ndugu Pemba ambaye ni mfanyakazi wa Serikali amuulize. Huo ni mjumuiko wa mkutano wa Wafanyakazi wa Serikali waliolazimishwa kwenda mkutanoni, wana CCM, wanafunzi, makada kutoka Unguja waliokuja na msafara wa mgombea, komba komba ya watu maeneo yote kwa magari ya bure, matumizi ya pesa nyingi na gharama kubwa.

Pemba tena. Hio analysis ya Mtoa Mada inaonesha haijui Zanzibar seuze Pemba.

Kura za CCM Pemba ratio yake ni hii 2015, 2010, na huko nyuma 5(Maalim Seif) : 0. 1( CCM)

Mwaka huu ni hivyo hivyo.

145,000 Kura 2020. 7: 0. 1.

Pemba kura hazibadiliki.

Fuatilia ujuzwe zaidi.
 
TAKWIMU HAZIDANGANYI

Kwa kawaida Kisiwa cha Pemba limekuwa chini ya himaya ya Maalim Seif kwa muda mrefu, mara zote kura za Pemba zimekuwa ni kura za uhakika kwa Maalim, kwa kifupi Pemba ilikuwa ni Ngome ya Maalim Seif, ukweli huu kwasasa umebadilika. Mapokezi ya Dkt Mwinyi jana yamekuja na taswira mpya ya Pemba.

Twende sawa kitakwimu,

Kura za CCM Pemba hazijawahi kuzidi 20,000 kati ya kura 125,000 zinazopigwa miaka ya 2010 na 2015. Mwaka huu wa 2020 wamejiandikisha wapigakura wapya 23,000 na kufanya idadi ya wapiga kura kufikia 148,000 kwa Pemba.

UMATI wa Wapemba uliojitokeza Gombani jana ni zaidi ya watu 60,000. Hawa ni mbali na wale waliojipanga mabarabarani wakimpokea Dkt Mwinyi akitoka Airport.

FACTS ON VOTER'S BEHAVIOR

1: Wapemba sio Wanafiki

Kwa waPemba tofauti za kiitikadi zinafanana kabisa na itikadi za kidini. Mtu akishajidhihirisha katika Dini yake anakuwa muumini kamili. Wapemba wamedhihirisha Imani yao kwa sasa.

2: Wapemba wanapiga kura
Wakati wote ambapo takwimu za wapiga kura zinapungua Tanzania Bara, Pemba hazijawahi kupungua, wakati wote over 95% ya waliojiandikisha hujitokeza kupiga kura. Mpemba aliyekuwepo Uingereza, Italy, Dubai, Oman, Qatar, Kamachumu, Liwale, Kakonko na hata Ukala, atajiandikisha na kuhakikisha anasafiri umbali wowote aliopo kwenda kupiga kura.

3: Wapemba wengi (wafuasi kindakindaki wa Seif ni Diaspora) Kwa maana hawaishi Pemba, ndio maana mipango ya ushindi ya ACT Wazalendo imeenda kupangwa Dubai. Kwa hali ya Dunia kwasasa ambapo kuna Corona na Lockdown katika nchi zenye wafuasi hao kama ilivyo Uingereza, Ulaya na Canada pamoja na nchi za kiarabu ni wazi watashindwa kushiriki kupiga kura mwaka huu.

4; Umri wa Wapigakura.
Ukweli ni kwamba Idadi ya Wapemba wahafidhina (wafuasi wa Seif) imeendelea kupungua kwenye daftari la wapigakura. Vijana wenye maono,elimu na matarajio mapya wamejiandikisha kwa wingi. Age Sex structure inaonyesha 40% ya wapiga kura wana umri chini ya miaka 35 na walio na umri wa chini ya miaka 50 (Umri wa Mgombea wa CCM Dkt Mwinyi) ni asilimia 87 ya wapigakura (Age mates)

Ikiwa Maalim Seif ana miaka takribani 80, umri huo (miaka 75 - 85) kwenye daftari la wapigakura ni pungufu ya asilimia 1. Hawa ndio waliokuwa pamoja na Maalim, kusoma pamoja na kuishi pamoja. Kwa ufupi watu ambao wanamjua na kumfahamu Maalim Seif kwa undani kabisa.

5; CCM imejipanga Pemba,
Ushuhuda wa Kazi ya Dkt Shein na mashineri ya CCM imejimarisha zaidi katika kipindi cha miaka 5 iliyopita. Ni kipindi hiki ndipo Ndugu Polepole alifanya ziara Pemba exclusively kwa zaidi ya siku 45, ziara ya Dkt Bashiru na Mikakati ya ushindi ya Chama hakika zimezaa matunda. Ni katika kipindi hiki Wabunge na Wawakilishi kutoka Pemba walijiuzulu na kujiunga na CCM.

6: Mpasuko wa CUF / ACT / ADC
Kwa miaka 5 iliyopita, migogoro mikubwa imeikumba Kambi ya Upinzani, CUF ikapasuka, Maalim akahamia ACT Wazalendo.Mpasuko huo umeacha athari kubwa Pemba, CUF bado haijakata roho, ADC imeendelea kujiimarisha na ACT imjipenya Pemba, lakini ukweli ni kuwa Chama hiko hakina mizizi wala nguvu,Nguvu iko kwa Maalim mwenyewe sio ACT, ACT haina nguvu wala mashineri ya Ushindi.

7: Sifa binafsi za Mgombea,
Waswahili walisema, Wema hauozi na chanda chema huvikwa Pete.Maisha ya Dkt Mwinyi tangu wakati wote wa Uongozi wake yamekuwa ni ya kujishusha. Tabia njema imekuwa ndio SIFA KUU inayomtambulisha. Hana kashfa wala makandokando. Anakubalika na Vijana na anapendwa na Wazee na Watu wazima. Mapokezi ya jana yameakisi taswira ya mapenzi ya watu kwa Mgombea, hakuna Mgombea wa CCM aliwahi kupata mapokezi hayo tangu kuanza kwa vyama vingi, HATA Dkt Shein ambae amezaliwa Pemba na kuwa na ndugu huko HAKUWAHI kupata mapokezi hayo.

NYOTA NJEMA HUONEKANA ASUBUHI NA TAKWIMU HAZIDANGANYI KUWA DKT MWINYI NI RAIS WA MIOYO YA WAZANZIBAR.

Ni wazi na ukweli usio na shaka yeyote kuwa kura za Dkt Mwinyi Pemba ni zaidi ya 90,000 Mwaka huu.

#YanayoNineemaTupu.
#Ushindiwamapema
#Mwinyi2020✅
View attachment 1572087
Kwakua lengo la seif sio jema basi hata akishindwa hatakubal na badala yake ataona kaonewa
 
Umeandika kinyume chake ila wajuzi tumekuelewa pemba sio hawamtaki Huseini ,Husein ni muislamu mwenzao hawawezi hata siku moja kumkataa ulilokuwa hulijui na umelisahaulisha kulieleza ni hivi CCM haitakiwi Pemba,imeshakataliwa tokea zamani na hata wanaozaliwa leo,wameshaichoka,haina tija zaidi ya dhiki na madhila.

Hivi hukuona mapokezi waliyopokelewa ACT wazalendo tokea airport mpaka uwanjani watu wamejipanga pande zote mbili za barabara nanda kagoogle RSTV au Kipepe TV huko kwa youtubers,ujionee maafa yanayoisubia CCM mwaka huu,wapemba wameshaicheza ngoma ya mwaka huu ,wansubiri kuihakikishia dunia mwaka huu upumbavu na wapumbavu hauna na hawana nafasi.

Msimamo wa Pemba makamanda wengi wa polisi wanaufahamu na wanawaelewa hivyo ni mambo madogo yanayorekebishika kiakili,
Hata mleta uzi yeye mwenyewe haitaki CCM maana imeleta ufukara wa kutosha
 
Kiumbe mwingine kutoka Lumumba asiyeijua Pemba, Wapemba wala siasa za Pemba!!

Pitia hii picha hapa chini:-
Pemba.png

Je, baada ya hilo "nyomi" Dr. Shein na CCM walipata nini Pemba?!!
 
Umeandika kinyume chake ila wajuzi tumekuelewa pemba sio hawamtaki Huseini ,Husein ni muislamu mwenzao hawawezi hata siku moja kumkataa ulilokuwa hulijui na umelisahaulisha kulieleza ni hivi CCM haitakiwi Pemba,imeshakataliwa tokea zamani na hata wanaozaliwa leo,wameshaichoka,haina tija zaidi ya dhiki na madhila.

Hivi hukuona mapokezi waliyopokelewa ACT wazalendo tokea airport mpaka uwanjani watu wamejipanga pande zote mbili za barabara nanda kagoogle RSTV au Kipepe TV huko kwa youtubers,ujionee maafa yanayoisubia CCM mwaka huu,wapemba wameshaicheza ngoma ya mwaka huu ,wansubiri kuihakikishia dunia mwaka huu upumbavu na wapumbavu hauna na hawana nafasi.

Msimamo wa Pemba makamanda wengi wa polisi wanaufahamu na wanawaelewa hivyo ni mambo madogo yanayorekebishika kiakili,
Kiukweli ndugu mawazo huwa hayapigwi rungu mawazo yanajibiwa na mawazo yaliyobora zaidi ,, ni vyema ndugu kama huna hoja ya kujibu andiko la tandaleone ni Bora unyamaze , taka yako wewe sio taka ni takataka , taka yetu sisi ndio taka na tunaisimamia ,,taka ya wananchi ni kuichagua CCM na watu wake wote kuanzia Raisi,Wabunge na Madiwani.
 
Yaani CCM Zanzibar wanapenda kujifariji sana.

Nani asiejua kuwa wanafunzi kuanzia Form 1 mapak 6 wameambiwa lazima waende mkutanoni? Tunajua kuwa wafanyakazi wote wa umma mmewalazimisha kwenda kwenye mkutano na wasipokwenda kibarua kitaota nyasi. Vipi kuhusu wana CCM mliowakomba Unguja na kuwapeleka Pemba kwa kutumia pantoni ya Sea Express 1? Masheha wakigawa shati na kofia usiku kwa kila mtu bila kujali chama gani 😀 😀 😀

CCM haijawahi kukubalika Pemba na wala haitokubalika. CCM wenyewe hawaipendi Pemba na wapemba wake. Walisema mpemba kuingia ikulu ni sawa na mbwa kuingia msikitini!
 
Hata kama haitashinda pemba, zanzibar siyo pemba peke yake, lakini pia ukae ukijua kwamba kura za pemba mwaka huu kwa ccm zitaongezeka hata kama hazitazidi za ACT,,

Huko kusema CCM inalazimisha watu.kuhudhuria mikutanoni ni propaganda tuu na hazina udhibitisho wowote.

Tusubir tuone tarehe ya uchaguzi ukweli utaonekana wazi
 
Yaani CCM Zanzibar wanapenda kujifariji sana.

Nani asiejua kuwa wanafunzi kuanzia Form 1 mapak 6 wameambiwa lazima waende mkutanoni? Tunajua kuwa wafanyakazi wote wa umma mmewalazimisha kwenda kwenye mkutano na wasipokwenda kibarua kitaota nyasi. Vipi kuhusu wana CCM mliowakomba Unguja na kuwapeleka Pemba kwa kutumia pantoni ya Sea Express 1? Masheha wakigawa shati na kofia usiku kwa kila mtu bila kujali chama gani 😀 😀 😀

CCM haijawahi kukubalika Pemba na wala haitokubalika. CCM wenyewe hawaipendi Pemba na wapemba wake. Walisema mpemba kuingia ikulu ni sawa na mbwa kuingia msikitini!
Chilubi ni bora uwe mtu ambaye unafikili sana na kuongea sana kuliko kufikiri kidogo na kuongea sana
 
Ccm wanaliwa pesa zO tu.
 
Chilubi ni bora uwe mtu ambaye unafikili sana na kuongea sana kuliko kufikiri kidogo na kuongea sana
Tunajua mbinu zenu za kuvusha watu kwa maji 😀 😀 😀 Bila shaka na wewe ni miongoni mlovushwa kuja kuongeza idadi!
 
Back
Top Bottom