Maalim Seif Shariff Hamad Aitikisa SMZ


Hizo mahakama zimeshapigwa kikumbo zamani na CUF au huna habari ?
Utakwendaje mahakamani wakati unaemshitaki ni msudani Jaji ni msudani wakili ni msudani ?

Amka wacha kutetea ujinga na kujiona unazungumza la maana kumbe ni limbukeni tu ,yaani unafurahisha watu wengi kwa kumuudhi mtu mmoja.Pole sana kama ungekuwa mwanangu ningekubadilisha na mkate tu.
 
WaTanganyika msiwe na haraka na kuiponda CUF au kumponda Maalim Seif Sharif Hamadi SImba wa Nyika ambae sio anaitikisa SMZ peke yake ,anaitikisa hata Serikali ya Muungano tena amefika mbali sana natumai hotuba yeke aliyoitoa baada ya Raisi Kikwete kutembelea Pemba na kufungua bomba la upepo mliisikia vizuri sana.
Aliitikisa vipi Serikali ya Muungano? Huyu bwana kwani sera gani ni za Chama chake zaidi ya kuota kuingila Ikulu?

CUF kama Chama kikuu cha Upinzani Tanzania basi itegemewe kuwa kufanikiwa kwake ni kufanikiwa kwa vyama vyote vya upinzani ,vita inayopigana CUF sio vita ya mchezo ni vita kuu kabisa katika siasa za Tanzania.
Kwani CUF wako vitani? Au ndio hayo mabomu yaliyoteguliwa?
CUF haina wafuasi wengi kama walioko Bara (Tanganyika),kama mnavyopima idadi ya wananchi wa Zanzibar kwa kulinganisha na jimbo au mtaa wa bara basi inatakiwa muelewe kuwa kwa upande wa wafuasi CUF inao wafuasi wengi zaidi huku Tanganyika.
Unajichanganya-haina wafuasi wengi vs inao wafuasi wengi, tushike lipi? Toa basi na takwimu za hao wafuasi unaowaita.

Kama vitendo vilivyotokea Pemba vimefanywa na wazalendo wenye kuchoka na utawala wa CCM nitakuwa mwenye kufarijika sana na kuona kuwa sasa tunaingia katika hatua nyingine ya kuzipinga tawala za kidhalimu ,hatua ambazo wananchi wa Nchi nyengine wamezifikia na kuwasaidia katika kuziondoa tawala zao za kidhalimu.
Kumbe na wewe gaidi? Unafarijika kutaka kubomolewa kwa madaraja?

Haya ni mambo yaliyopangwa na hao mapolisi waliokwenda kwa makundi huko na sasa inaonekana namna wanavyotekeleza yale waliyoyaandaa au waliyopangiwa kuyafanya ila kasoro inayojitokeza ni kuwa wanatekeleza kiwoga woga hawatekelezi vile inavyotakiwa ,matokeo yawepo mazuri kuwa masheha wakumbwe na vifo ,waandikishaji walipukiwe na mabomu.
Toa ushahidi!

Pemba Nchi ambayo imetawaliwa na kiza..........
Uhuru wenu mmeupata lini?
 

Shame on you!!
 
Hujaelewa, ni chama cha Kigaidi!

umeshawahi kuona mikutano ya aliyekuwa kiongozi kipenzi wa kijerumani na nchi nyingi za ulaya ?Mr Aldof Hitler alivyokuwa anaendesha propaganda zake zidi ya watu ambao hakuwapenda wa ISRAIL?hali kama hiyo ndio inayoendeshwa hivi sasa hapa Zanzibar. mimi kama muslim namini kauli ya Mmungu alipotwambia (Haliwi isipokuwa lile analolitaka yeye liwe) pia nakumbuka maneno ya Ali sultan katika uzinduzi wake wa kitabu aliposema :alihukumiwa kifo lakini walio muhukumu kifo wao ndio walio kufa na yeye bado yuhai na akazidi nakusema kuwa huo ndio uwezo wa Muumba.
 
Kibunango, mwenzako nilikuwa huko huko(najuta sana) tena nilikuwa si mbali na jikoni kunakopikwa hizo mbinu chafu, nakuapia kuwa, CCM haikuwahi kushinda uchaguzi wa urais Zanzibar bila ya hizo mbinu chafu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…