Serikali imetangaza kwamba kuanzia sasa watoto wa shule wasiingie kwenye vijiwe vya kuonyeshea TV.Naipongeza serikali kwa kuelewa kwamba vijiwe hivyo vinachangia katika uharibifu wa maadili, lakini mbona kwa kuchelewa sana?Hata hivyo hatua hiyo ni ndogo sana.Ninaloshauri mimi ni kwamba serikali iende mbali zaidi.Ihakikishe kwamba vituo vya Television na Radio havitoi matangazo yeyote yanayopotosha maadili,na pia makampuni ya biashara nayo hayasambazi matangazo yanayochangia katika uhamasishaji wa ngono na upotoshaji wa maadili.Tukumbuke kwamba upotoshaji huo hautokei kwenye vijiwe vya kuonyeshea kanda za video na matangazo ya television tu, bali unatokea hata majumbani.