Maamuzi, kupata, kukosa

Maamuzi, kupata, kukosa

LOVINTAH GYM

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2015
Posts
459
Reaction score
653
Kwenye maisha huwezi kupata kila kitu unachokihitaji hii ndio tunaita Scarcity of resources kwenye uchumi.

Kwenye mchoro imewakilishwa na point F. Inamaana hiki ni kile kitu ambacho unakitamani sana ukipate lakin hauna uwezo wa kukipata kutokana na uchache wa mali zako, elimu yako nk



Kwasababu huwezi kupata kila kitu inabidi uchague kitu kimoja wapo ambacho ni bora zaidi kwako, hiki kitendo kinaitwa Choice making.

Imewakilishwa na point A,B,C na D



Ukichagua jambo moja inamaana kuna mambo ambayo utayakosa hiki utakachokikosa ndio tunakiita opportunity cost.

Mfano:

Ukichagua A lazima utakosa B,C, na D



Unattainable point inawakilisha vile vitu ambavyo unavihitaji kwenye maisha ila hauwezi kuvipata kutokana na uhaba wa resources.

Hii ni point F



Inefficiency ni point E, inamaana ungeweza kufanya vizuri zaidi lakini umeamua ku produce chini wakat unauwezo wa kupata zaidi kutokana na resources ulizo nacho.



Na huu mchoro wote unaitwa PRODUCTION POSSIBILITY FRONTIER .



Sasa kwenye maisha huu mchoro unatumika sana,

Mfano:

Mwanafunzi akiamua kuolewa na kuacha masomo inamaana choice aliyo make ni kuolewa na opportunity cost anayoipata ni kuacha shule.



Ukiamua kuwekeza pesa kwenye fixed account badala ya kwenda vacation. Inamaana choice ni kutunza pesa fixed account ambayo utanufaika kupata faida , na opportunity cost ni umekosa kusafiri na kula bata.



Point ya muhimu ni kwamba hizi decision tunazozifanya ndio zinakuja kuamua maisha yetu yatakavyokuwa. Unaweza hisi maamuzi uliyoyofanya leo ni madogo sana ila kwa miaka 5 mbele yatakuja kuku affect either positively au negatively. So think careful before making any decision.

Tumia Pro and Cons strategy kabla ya kufanya maamuzi.



Shuleni , mwalimu anaweza akamchapa sana mtu aliepata 70 kuliko aliyepata 50, hii ni kwasababu anajua huyu aliyepata 70 huenda uwezo wake ni mkubwa zaidi .

aliyepata 70 ndio yupo kwenye point E kwenye mchoro wetu, kuwa anaweza akafikia point B au C akiongeza juhudi.



Karibu kutoa mifano hai ya choice na opportunity cost,efficiency, inefficiency, unattainable point unazopitia katika maisha yako.



#economics #PPF #choice #decisionmaking #oppotunitycost #efficiency #inefficiency

ppf.png
 
Back
Top Bottom