Fernando Wolle
JF-Expert Member
- Aug 19, 2022
- 387
- 770
Kwanza tukubaliane kwamba ili Tanzania isonge mbele na iweze kujitegemea inamuhitaji kila Mtanzania kuwajibika kwenye nafasi aliyopo huku serikali ikiwa ndio injini inayoaminika kusukuma sehemu zote kwa uaminifu kabisa na ufanisi mkubwa.
NDIO! Tanzania inaweza kuwa kinara wa maendeleo Afrika na kufikia hatua ya kujitegemea yenyewe. Haya yote yanawezekana ndani ya miaka 20 kwa kujifunga mkanda kama nchi na kwa wananchi wote huku serikali ikiwa inawajibika kwa 100%.
Kwanini inawezekana tukajitegemea ndani ya miaka 20? Ikumbukwe kwamba Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye fursa na rasilimali nyingi sana zinazojitosheleza, na kwa karne ya sasa hatutahitaji kuumiza vichwa kufanya uvumbuzi wa miaka na miaka kupata teknolojia ya kuzichakata na kuzitumia rasilimali tulizonazo bali ni suala la kuiga tu teknolojia iliyopo na kuitumia.
Tanzania ina idadi ya watu takribani milioni 55 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 ingawa kwa sensa ya mwaka huu 2022 naamini idadi itakuwa imeongezeka mara dufu, hivyo nchi yetu ina nguvu kazi ya kutosha na ina soko la ndani la kutosha. Vilevile Tanzania ina ardhi kubwa yenye rutuba sana, ina mito, maziwa, bahari na madini ya aina nyingi sana.
Sasa, hatua ya kwanza kabisa serikali iweke sera ya elimu ya mafunzo ya ufundi kuwa ni lazima na ni bure kwa kila mtanzania kama ilivyo kwa wanafunzi wanaomaliza kidato cha sita Kwenda jeshi la kujenga Taifa. Halikadhalika kwenye elimu ya mafunzo ya ufundi stadi. Hapa tutakuwa na uwezo wa kupata wataalam wa chini kwaajili ya kuendesha shughuli zozote watakazopangiwa baada ya kumaliza. Kwa ufupi Serikali ni lazima iwashughulishe watanzania kwa manufaa sawia yaani anayefanyishwa kazi aone anafaidika na wakati huohuo serikali nayo inafaidika. Hapa elimu ya ufundi stadi ijumuishe mambo yote ya msingi na sio lazima mtu asome kiundani sana bali elimu itakayomwezesha kupata A, B na C za shughuli atakazofanya ni kama Sayansikimu ijumuishe ufundi, masuala ya kilimo na ufugaji na elimu ya biashara ya ujasiriamali kwa ujumla.
Sasa tuone namna tunavyoweza kufanya;
Kwa uhalisia huu hakuna kukwama! Sasa ili tusonge mbele ni lazima tuhakikishe tunauza zaidi nje kuliko kununua nje kwa maana ya kwamba tukiuza nje tutakuwa na uwezo mkubwa wa kupata fedha za kigeni na hii inawezekana pale tutakapofanya kazi za uzalishaji sisi wenyewe.
Tujenge viwanda vya kutosha, hili suala la viwanda limezoeleka kutamkwa lakini kutekelezaji wake huonekana kuwa na ugumu kutokana na serikali kuwaachia watu binafsi kwa kutoa wepesi Fulani wa kuanzisha.
Nataka kusema nini kuhusu viwanda? Kama nilivyosema awali, Tanzania tuna kila kitu na kuhusu teknolojia wala sio ya kuumiza kichwa ni suala la kuiga tu teknolojia. Serikali kupitia wizara ya Viwanda na biashara ina uwezo wa kuanzisha viwanda kila mkoa vyenye mtaji wa Shilingi Bilioni 500 ndani ya miaka 2 na kila mwaka kuendelea na ujenzi wa viwanda vingine. Ndio inawezekana! Nimefuatilia pale kiwanda cha nguo kilichopo Mabibo External jijini Dar es Salaam (EPZ), kilianzishwa kwa mtaji wa bilioni 500 na kina wafanyakazi Zaidi ya mia nne. Kiwanda hiki hakipumziki na kinatoa nguo za daraja la kwanza na husafirishwa Kwenda nje huku malighafi zinazotumika ni za hapahapa nchini. Kiwanda kimetengeneza ajira Zaidi y amia nne, fikiria serikali ikishirikiana na wananchi ikajenga viwanda vya aina hii kila mkoa na ikaingia kwenye wilaya ni ajira ngapi za moja kwa moja zitatengenezwa?
Kupitia viwanda hivi, kutakuwa na wafanyabiashara wa ndani na wanaosafirisha Kwenda nje kwa kushirikiana na serikali na sio lazima viwe viwanda vya nguo tu, bali ni aina zote za viwanda vya usindikaji na utengenezaji wa bidhaa au viwanda vya malighafi zinazoongezewa thamani.
Suala la ufugaji na kilimo, hapa serikali badala ya kugawa pesa Kwenda kwenye halmashauri ili kuwakopesha vijana ambazo kwa asilimia kubwa fedha hizi huwa haziwafikii walengwa, sasa ianze kuandaa vikundi vya vijana kuanzia wanaohitimu elimu ya vyuo vya ufundi kwakuwa elimu hii ya ufundi stadi wanakuwa tayari wanayo. Hivyo serikali inatenga maeneo kwaajili ya utekelezaji tu. Wataalamu wabobezi wapo, ambao watawaongoza hawa vijana wanaotoka kwenye mafunzo hayo.
Tusiwaachie wageni wafanye hizi kazi mfano wachina au wazungu kana kwamba wana mapenzi mema sana na nchi yetu, hawa wamekuja kuchuma tu na kuondoka. Hivyo jukumu hili la kufanya nchi yetu ijitegemee ni letu sote, Mtanzania yeyote hawezi kukwepa kwenye hili.
Makundi haya ya vijana kwnywe Nyanja za kilimo na ufugaji yatatafutiwa soko ambalo litakuwa ni viwanda vilivyopo nchini na pengine baadhi ya mazao yatasafirishwa nje huku tahimini ya uongezaji wa thamnai na bei ikitazamwa na taasisi husika. Wakati huohuo magereza yote nchini lazima yafanye kitu hichohicho cha uzalishaji wa malighafi na kuviuzia viwanda ambavyo vitakuwa vimeanzishwa. Hapa tutaweza kuuza bidhaa nyingi na mazao ya kilimo na ufugaji nje ya nchi kuliko kuingiza ndani. Tukiwa na pesa nyingi tutatununua teknolojia yoyote ile.
Kama ilivyokuwa kwa Tanzania miaka ya 1980 Malaysia, Singapore, India, China na Korea ya Kusini, zilikuwa ni nchi maskini za ulimwengu wa 3 lakini nchi za wenzetu zilipata mabadiliko makubwa miaka 20 baadae na kutuacha sisi tukiogelea kwenye dimbwi la umaskini.
Sasa kama wenzetu waliweza kusogea mbele ni kwanini Tanzania ishindwe? Nguvu kazi tunayo, Fursa zipo nyingi, kila kitu tunacho suala ni moja tu kuthubutu! Na kama nchi yetu tulisema ni ya kijamaa basi serikali ni lazima ikubali kutia mkono wake na kufanya maamuzi magumu kuisaidia nchi kujitegemea ndani ya miaka 20.

Bofya ‘Like’ na toa maoni yako nipo kwaajili ya majadiliano. Asante.
Upvote
1