Maamuzi niliyoyafanya juu ya mke wangu..

hapo kwenye saba sielewi ,wewe umesema umeamua aache kazi aamie ughaibuni ...huo mshahara wa kutumia atautoa wapi akiacha kazi?

Pia 6 anatuambia hela ya matumizi awasiliane na wazazi hapo umetuchanya tuweke sawa
 
1.Mke wangu bado atabaki kuwa mke wangu katika hari yoyote ya maisha hiwe ya shida au tabu..nakumbuka nimetoka naye katika hari ya chini sana bado tukiwa wachumba.hivyo pesa isiwe kigezo cha kututenganisha leo zipo kesho hazipo.zaidi nikiona ametoka nje ya ndoa hapo maamuzi yatakuwa mengine.



Mkuu nadhani msingi wa mada yako ulikuwa hapo juu kwenye red..lakini nashangaa umeanza na hii kauli az if kwamba sisi ndio tumekwambia kwamba mkeo 'anafuja pesa' wakati wewe ndio umetuambia..any way..
Baki to ze topiki naomba tu unifafanulie:
-kwa nini mtoto hutaki aje huko ulipo?..
-kitendo cha kufanya marekebisho katika upokeaji/utumaji wa pesa kupitia wazazi endapo mkeo atashindwa kuja huko nadhani ungekifikiria zaidi..idea nzuri ingekuwa kumpunguzia amount na yeye kukupa mchanganuo..BTW ngoja tuone hii plan A kama itawork..ikishindwa njoo tena jamvini for plan B..
 
Uko sawa!huo ndio uanaume!Umefanya maamuzi magumu kwa mustakabali mwema.
 
Think twice before u decide coz a little mistake can lead misunderstanding btn u & wife so fikiria mara mbilimbili kabla ya kuchukuwa hatua
 
Ndio maana mimi huwa in rela life situation sithubutu kumshauri mtu mambo ya ndoa; jamaa anataka kutuuzia kesi kiaina; kumbe na wewe umeliona hilo. Lol.

 
Ndio maana mimi huwa in rela life situation sithubutu kumshauri mtu mambo ya ndoa; jamaa anataka kutuuzia kesi kiaina; kumbe na wewe umeliona hilo. Lol.

Mambo ya ndoa ukijifanya mjuaji ukashauri watu kuachana, wakati wakikutana wawili huko wanayaongea vizuriiiiii ulieshauri kuachana unabaki kuaibika. Yani jamaa hapo skype mke alipolia wamebembelezana weee, bi dada hajui hata kama huku JF alishajadiliwa.... haya bana ..ila nimejuuuuuuta kushauri ishu za ndoa
 
well ,mm napinga suala la hela kupewa wazazi ni dharau kwa mkeo
pili uamuzi wa mtoto akae wapi si wako peke yako ni wa wazazi wote hili
akilipeleka ustawi wa jamii na mahakamani atakushinda
huna haki kumchukua mtoto alelewe na wazazi wako wkt mkeo ana
kazi na anauwezo wa kumlea kwa hilo nakupinga mzee kumbuka yeye
ndio ana uchungu na mtoto kuliko hata ww kambeba miezi 9 thats not fair hii ndio tunaipigia kelele kila siku
tatu suala la kuacha kazi wkt hata viza hujapata sio hoja yenye mshiko afanye kazi hadi upate viza ndio amue kuacha kazi ama la.
la mwisho mkuu iweje utake kumchukua tu mke umwache mtoto kwa wazazi nyie mkaishi nje mama hatakuw ana amani na pia hamumtendei mtoto haki
napenda kukuasa tu kuwa ww binafsi huna mamlaka ya mwisho ya mtoto atunzwe wapi ni suala la nyie wawili kuamua.naona bado una maamuzi ya kizamani kuwa mwanaume ndio last say ukasahu kuna sheria zinawalinda mama na mtoto unless kama huyo mtoto sio wa huyo mama
 
Kwa nini usimchukue pia na mtoto muishi nae huko ughaibuni? Kwa nini huwa tukifanya maamuzi kwenye ndoa interests za watoto hazitiliwi maanani? Wakati mnafanya hayo maamuzi mlimpa mtoto nae fursa ya kufanya maamuzi anataka kuishi na nani na wapi? Or you just took him/her for granted?
 
kuna ututa mahali flani kwenye maamuzi haya.....ngoja nije
 
Mmmmmmmmmmh, May God be with you on your decisions.
 

naunga mkono haya mawili!

Chief hata iweje kama kipato chake insignificant kiasi gani.....usimwachishe mkeo kazi; ni hatari kuliko unavyoweza fikiri.isitoshe hata huko ulipo ikiwa lengo ankuja kukaa tu.............mimi siafiki kabisa kwa sababu nayo ni hatari nyingine.........unaua uwezo wake wa kufanya kazi ilhali huyu ni partner wako katika familia na sio mali yako! yanaweza kutokea mabaya kuliko unavyoweza kufikiri;

Nikushauri uungane na suala la kuamua kupunguza pesa unayoituma kwa kuanzia na huku ukifuatilia peasa uliyotuma mwanzo imefanya nini.
 
Umeamua vyema kama mume ila maamuzi yako kwa upande mwingine kama walivyosema hapo juu wengine hauko sahihi. Umesema mkeo ni mkeo na ataendelea kuwa mkeo sasa kumwambia awe anachukua pesa kwa wazazi huoni umemshusha hadhi kuwa mke? Na suala la mdada kuacha kazi ungesubiri upate kwanza hiyo visa halafu ndio umuite mkeo huko, na si visa tu uhakikishe akifika huko atapata na kakibarua na si kukaa tu nyumbani.

Halafu suala la mtoto kuchukuliwa na wazazi halijakaa vyema wakati mama yake yupo na sijaona hata sehemu moja ukisema mama ameshindwa kulea mtoto wake so akikugomea kwamba hampeleki popote ujue kwamba mtoto hatoenda kokote sheria pia itamlinda mama na mtoto.

Hebu jaribu kuzungumza nae ajaribu kupunguza matumizi yake ya kila siku na kwamba hizo pesa unazomtumia ahakikishe zinatosha, na usijaribu kupunguza kile kiasi ulikua unamtumia mwanzo ila mwambie ahakikishe ile hela inatosha. Kama ikishindikana ndio labda umwambie hizo habari za yeye kuacha kazi na kukufuata wewe huko ughaibuni kwani atakua ameshindwa masharti mwenyewe. Na kwa sababu umesema alilia na machozi inawezekana akajirekebisha.

Kila la kheri
 
Hayo maamuzi bwana mengine sio mimi naona asiache kwanza kazi afanye kazi ila aendelee kukaa kwa wazazi pia mtumie tu hela kidogo mkuu hata dola 100 au mia 2 bwana
 
Duh! kwa hayo yooote uliyoyaandika, sidhani kama huyo mke unamuhitaji bado, labda kama ni bado under age, La! ana akili zake timamu kuna hatari utampoteza mazimaaaa. Anyways goodluck, but Never underestimate her, kwani huwezi jua naye akuwazia nini
 
Kwetu ni matusi ; kuoa halafu ukarudisha mke ake na wazazi wako; labda kuwatembelea na siku kaa!
 
Hongera kwa maamuzi, napingana na wewe hapo kwenye namba 6, mkeo kuchukua hela kwa wazazi wako? Mi naona haijakaa vizuri mkuu!
 
uamuzi mzuri kumchukua mkeo kuishi nae ughaibuni, ila...

kwanza, hakikisha amepata visa kwanza kabla hajaacha kazi.
Pili, mtoto ndiyo security yako bana, iweje leo hii uamue mtoto akakae kwa wazazi wako mkeo umuache mkiwa?...aisee maamuzi mengine unatafuta lawama sasa...
tatu, unamnyang'anya mke nyumba akakae kwenu/au kwao halafu nyumba unawapa shemeji zako, aisee?!

...ujue akikosa atajiskia unyonge sana kupoteza mume, mtoto, kazi, nyumba, na hata fedha ulizokuwa unamtumia...
anyway, nawatakia kila la kheri kwenye ndoa yenu.
 
Maisha ni mitihani - na kwa bidii mmefaulu mmoja mkubwa na kwa umoja na mapenzi mtafaulu ijayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…