Maamuzi ya CHADEMA yanasubiri 'VAR'. Tumtazame Mbowe akisoma

Maamuzi ya CHADEMA yanasubiri 'VAR'. Tumtazame Mbowe akisoma

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
339
Reaction score
678
Jana Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA na Mbunge wa zamani wa Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro alisoma maadhimio ya kikao cha Kamati Kuu kilichoketi jana asubuhi hadi Usiku.

Kikao hicho kwa mjibu wa Mbowe kilikuwa na ajenda moja tu ya kuwajadili Wanachama wa BAWACHA ambao walienda kula kiapo cha kuwa Wabunge wa Viti Maalumu mbele ya Spika Jobu Yustin Ndugai.

Mapema wiki hii baada ya kiapo alijitokeza Katibu Mkuu wa CHADEMA kuwa wale ni Wabunge batili kwa kuwa hawajapitishwa na vikao halali vya chama. Baada ya kauli hiyo NDUGAI alijibu na baadae tume ya uchaguzi. Lakini leo staki kuzungumzia haya, ila ninataka kuzungumzia uzito wa kikao na saikolojia ya msomaji wa azimio.

Kwanza tukiri kuwa kikao kilikuwa kizito na inaonyesha wazi kulikuwa na minyukano mikali mle ndani ya kuto kukubaliana, hii inadhihirishwa na muda ambao kikao kilitumia kumaliza ajenda moja ambapo kilitumia zaidi ya saa 15( kumi na tano). Hii ni wazi wapo wanaoafikiana na kiapo hicho na wapo wanaokataa ili kuonyesha umma kuwa wao chama kwanza na si cheo.

Lakini wakati hayo yakizungumzwa, basi anza kumtazama Mbowe muda wote akiwa anasoma tamko. Mbowe ukimtazama kwa umakini ambapo alikuwa akibadilika badilika lakini sura yake usoni haifanani na kile ambacho kinatoka moyoni. Kuna ukinzano kati ya sura na imani ambayo inatafsiriwa na body language. MBOWE kila alipotaja jina la Mdee na Matiko ilikuwa inaonyesha wazi kuwa hakubaliani na makubaliano ya CC, lakini kwa kuwa ameambiwa asome kwa niaba basi hana budi.

Hii inaonyesha kuwa wapo walioshiriki mchakato huu wa Wabunge hawa kula kiapo akiwepo Mwamba Freeman Aikael MBOWE, lakini baada ya reaction kutoka nje ndipo wakajifanya mchezo huo hawajashiriki.

Kinachosubiriwa sasa baada ya Bunge, Tume na CHADEMA kusema basi ni VAR ya kuthibitisha kuwa hawa wataendelea kuwa wabunge au laa? VAR ndiyo itakayotuonyesha kama sheria zilifuatwa hasa baada ya kuona replay.

Baada ya food for thought kila mtu anayo fursa ya kuipitia upya video ya Mwenyekiti ili kuthibitisha haya. Mimi siungani na waliosema alikunywa, ila ninasema ile ni sura ya kuto kukubaliana.
 
Naunga mkono hoja, inavyoonekana hii ni kauli ya kuwatuliza wanazi wa chama hapa jukwaani na kwengineko ila ukweli ni kuwa walibariki Waheshimiwa wabunge wakale kiapo.

Acheni propaganda Chademaaa.
 
Siku hizi mmeamua muanze na namba za simu mwanzoni mwa bandiko badala ya mwishoni!Sijui mmegundua huwa hawasomi mpaka mwisho?Na bado,shwain kabisa!Uteuzi mtausikia kwenye bomba!
Hongereni Chadema kwa kuwaruhusu wakina Mama kwenda kuapa kwa Hakika mlifanya uamuzi wa Busara.

Jana mliitisha mkutano ili kuwazuga mashabiki maandazi kama hawa ambao wanajaa kwenye mikutano halafu hawapigi kura.
 
Mbowe Mbowe Mbowe nimekuita mara tatu.

Mungu azidi kukuweka Baba wanaokudis najua wanakukubali kila siku, kila dakika na kika sekunde
 
Back
Top Bottom