ndolelejiUduhe
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,837
- 3,027
Selfishness ndio Jinamizi letu Waafrika kila mtu mahali pake na kwa nafasi yake anafikiria zaidi kujinufaisha yeye na jamaa zake tu !Trump sio kioo cha kufuta ufukara wa Africa, bali ni jinamizi ambalo hujui kesho ataamka je,unpredictable scumbag.
Ethiopia ilijenga bwawa kubwa ili kutatua matatizo makubwa ya kufua umeme,na kukuza kilimo hasa cha umwagiliaji bila kuhadhiri upatikanaji wa maji ya mto Nile kwa Nchi ya Misri.
Kama kawaida Misri anaejiona kama ndio tu mwenye madaraka ya kutumia maji ya mto Nile akaendekeza uongo wakati Trump akiwa Raisi,akatishia Ethiopia kuwa atalibomoa bwawa hilo kwa makombora.
Trump mfanyabishara aliyefilizika zaidi ya mara sita sio kioo cha jamii kwa ustawishaji wa uchumi kwa Africa.
Afrika ina watu wenye akili mara billioni kuliko kifaduro Trump.Ni kuogeza juhudi na kutumia akili zetu ili kutatua mambo yetu.
Naamini ni wachache kama wapo wanaozifikiria zaidi Nchi zao na watu wao katika kupata maendeleo !
Sisi Asili zetu ni za kupenda kuwatambia wenzetu kuanzia vijijini mpaka mijini !
That means kila mtu akishapata yeye anaona ameshamaliza kazi wengine potelea mbali watajijua wenyewe !
Hapo wenye kuwepo kwenye position nzuri inakuwa ni mwendo wa kupiga pesa na kula Bata kwa sana !