Maana halisi ya neno " zanzibar kumezwa"

tpmazembe

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Posts
2,469
Reaction score
586
Kila yajapo mawazo ya Muungano wa serikali moja neno hilo huibuka kama kwamba ndio jibu sahihi na pekee linalozuia muungano wa serikali moja.

Najiuliza huko kumezwa kutakuwaje? Kwani kama ni sehemu inaitwa zanzibar si itaendelea kuitwa hivyo hivyo zanzibar na majengo yake na watu wake kuwa pale pale. ni nini hasa maana ya neno hili?

Zanzibar ina historia yake ni kweli lakini ziko sehemu nyingi zenye historia maalum ndani ya Tanzania na zimeendelea kubaki hivyo hivyo . sasa huku kumezwa maana yake nini? ukienda ujiji kigoma hata kesho utaona tu asili yake,ukienda tanga utaona asili yake ,ukienda maeneo ya tabora utaona.huku kumezwa mbona hakujaonekana labda kumezwa ni nini?mbona mbuga zote hazijapotea watu wa maeneo hayo ni wale wale.

Hili neno kumezwa maana yake ni nini?
 
  • Thanks
Reactions: SMU
hata mimi neno hilo linanitatiza sana. Mbona marekani ni muungano wa states nyingi lakini kwao hakuna kumezwa? mbona alaska iliojiunga na marekani dunia haikuogopa kuwa alaska na historia yake itamezwa. kwani haya mataifa yamegawanywa kimiaka na Mungu? si hao hao wazungu.

Trust me hata kwenye kero za muungano kuna msukumo wa wazungu .
 
kumezwa kwa mtizamo wa kutokuwa na mamlaka take ya kujiongoza. huwezi linganisha znz na tabora ambayo haijawah kuwa nchi. kwa mfano mdogo sana ni sawa na mwanamume afunge ndoa halafu asiwe na usemi ktk nyumba yake. madaraka yote amiliki mama wakati wote wawili wananafasi sawa ktka ndoa. watoto (tabora) hawawezi kupigania nafasi yao ktk ndoa ya baba na mama yao.
 
sikuwa na maanisha zanzibar ni sawa na tabora,bali nilikuwa namaanisha uhalisia wake na utamaduni wa mahali fulani unaendelea kubaki hivyo hivyo.

Ndani ya serikali moja sina maana kuwa katiba itasema rais na viongozi wa umma wawe wanakuwa watanganyika hapana. katiba inatoa haki kwa raia wote wa nchi hyo moja. yeyote pale ataruhusiwa kuwa kiongozi wa taifa hilo bila kujali atokapo bali uwezo wake. maana yake tunakuwa na serikali moja na kusahau utanganyika na uzanzibar ambayo ni majina asisiwa na wakoloni.

embu nielezee vizuri huko kumezwa.
 
..Hili neno kumezwa maana yake ni nini?
Kwa kuwa Zanzibar ni ndogo (idadi ya watu na hata kijiografia), ukiichanganya na Tanganyika hupati "Tanzania", utaendelea kubakia na "Tanganyika" tu (watu hawata feel kuwa ni nchi mpya imeundwa na nchi mbili).
 
Mkuu Bobwe2, nasisi tunasema Tanganyika kwanza! Vyetu vyenu, vyenu...vyenu!
 
Kwa kuwa Zanzibar ni ndogo (idadi ya watu na hata kijiografia), ukiichanganya na Tanganyika hupati "Tanzania", utaendelea kubakia na "Tanganyika" tu (watu hawata feel kuwa ni nchi mpya imeundwa na nchi mbili).

Hiyo sababu mbona haina faida yeyote ,kiuchumi wala kijamii.mbona kenya na Tanzania ziko eac na rwanda na burundi? kikubwa sio watu kufeel bali maendeleo ya nchi wahusika.kila mmoja kuwa huru kufaidia popote ndani ya muungano huo.

nini hasa maana ya neno kumezwa kwa zanzibar?
 
  • Thanks
Reactions: SMU
mleta mada sidhani kama kuna jibu maana hata neno kumezwa ni neno la kisiasa lenye maana hawataki kuvunja serikali yao.
 
hata wanaotumia neno hilo nadhani hawaliju maana yake
 
kukaa kimya ucdhani ndio ushindi wa hoja yako, bali watu hasa sie Wazanzibar hatutaki kupumbazwa na mtu mjinga kama wewe, miaka yote hiyo neno kumezwa huilijui maana yake...? hata mtoto wa chekechea haulizi upuuzi huo, lakini kama sie hatujui maana ya kumezwa, hebu muulize Warioba huewenda akalijua maana yeye ndio kutwa hulitumia neno hilo..
 
mimi sijaona huko kumezwa kunakosemwa maana hakuna mpare ataacha kulimba tangawizi kuja unguja au pemba bila sababu. labda apelekwe kama mpishi au mfuta meza kwenye hizo hotel za kitalii basi ambayo bado ni kazi ya kitumwa. kama ni kuja huko hivi hivi kujazana hata sasa anaweza kuja maana hajazuiwa. sasa huko kumezwa kuko wapi
 
Kila yajapo mawazo ya Muungano wa serikali moja neno hilo huibuka kama kwamba ndio jibu sahihi na pekee linalozuia muungano wa serikali moja.

Najiuliza huko kumezwa kutakuwaje? Kwani kama ni sehemu inaitwa zanzibar si itaendelea kuitwa hivyo hivyo zanzibar na majengo yake na watu wake kuwa pale pale. ni nini hasa maana ya neno hili?

Zanzibar ina historia yake ni kweli lakini ziko sehemu nyingi zenye historia maalum ndani ya Tanzania na zimeendelea kubaki hivyo hivyo . sasa huku kumezwa maana yake nini? ukienda ujiji kigoma hata kesho utaona tu asili yake,ukienda tanga utaona asili yake ,ukienda maeneo ya tabora utaona.huku kumezwa mbona hakujaonekana labda kumezwa ni nini?mbona mbuga zote hazijapotea watu wa maeneo hayo ni wale wale.

Hili neno kumezwa maana yake ni nini?

"angalia clip hii waweza kupata mwanga .... KAMATI YA MARIDHIANO SIX:WARIOBA AWASILISHA RASIMU 18 MARCH 2014 PART 3/5 - YouTube "
 
Back
Top Bottom