Kila yajapo mawazo ya Muungano wa serikali moja neno hilo huibuka kama kwamba ndio jibu sahihi na pekee linalozuia muungano wa serikali moja.
Najiuliza huko kumezwa kutakuwaje? Kwani kama ni sehemu inaitwa zanzibar si itaendelea kuitwa hivyo hivyo zanzibar na majengo yake na watu wake kuwa pale pale. ni nini hasa maana ya neno hili?
Zanzibar ina historia yake ni kweli lakini ziko sehemu nyingi zenye historia maalum ndani ya Tanzania na zimeendelea kubaki hivyo hivyo . sasa huku kumezwa maana yake nini? ukienda ujiji kigoma hata kesho utaona tu asili yake,ukienda tanga utaona asili yake ,ukienda maeneo ya tabora utaona.huku kumezwa mbona hakujaonekana labda kumezwa ni nini?mbona mbuga zote hazijapotea watu wa maeneo hayo ni wale wale.
Hili neno kumezwa maana yake ni nini?