Maana halisi ya Rastafari


Yeah_alikuwa mwanautambuzi makini sana mkuu...r.i.p Munga Tehnan
 


Mkuu NattyDread! Kwa hivyo hizo makala zake zilipingana au zilisisitiza umuhimu kuwa na imani ili pawepo na hofu ili tujisahihishe au niaje hasa? fafanua kidogo au ikiwezekana tupia japo makala hizo tupate elimu japo kidogo.
 

Kuna machapisho ya Moabi ukiyasoma hautaogopa kifo hata chembe,
 

Unaijua lakini vizuri historia ya Nimrod, haswa imani yake?
 
Mkuu NattyDread! Kwa hivyo hizo makala zake zilipingana au zilisisitiza umuhimu kuwa na imani ili pawepo na hofu ili tujisahihishe au niaje hasa? fafanua kidogo au ikiwezekana tupia japo makala hizo tupate elimu japo kidogo.
Katika makala za Munga ilikuwa kuelimisha watu kujitambua,uwezo ambao binadamu anao katika maisha yake bila kujua,katika makala hizi alionyesha binadamu ni kiumbe pekee mwenye akili na utashi lakini ni kiumbe pekee anaeishi katika viwango vya chini vya utambuzi,binadam ni zaidi ya mwili na katika hili anauwezo wa kutaka vitu/kitu ambacho mwili hauwezi kukitenda,hapa unapata tofauti kati ya mwili na roho,udhaifu unaopatikana katika mwili ndio unaotengeneza IMANI.Nimejaribu kutafuta makala zake nyingi zipo katika vitabu vyake ila nimepata moja embu jaribu kuipitia katika utulivu na upana wa fikra......
HAPA UNAWEZA PATA KIDOGO KUHUSU IMANI

[h=3]SAYANSI YAKIRI BINADAMU HAFI, HUBADILIKA.[/h]
Kwa zaidi ya miongo miwili sasa, wanasayansi wamekuwa wakijitahidi kutafuta jibu la swali la, je binadamu anaendelea kuishi baada ya kupoteza mwili wake? Kuna wanaoonesha kwamba wanakubaliana na hilo na kuna wale ambao wanasema huenda hakuna kitu kama hicho.
Kwa mfano kuna wale wanasayansi ambao wanakiri kwamba, watoto wanaofahamika kwa jina la Indigo, ni watoto ambao wana akili kubwa kuliko zile za binadamu wa kawaida. Tafiti zinaonesha kwamba, watoto hawa walianza kuzaliwa hapa duniani kuanzia mwaka 1975. Ni watoto ambao uwezo wao katika kuelewa mambo ni mkubwa kuliko tulivyozoea kuona.

Baadhi ya watoto hawa, kutokana na uwezo mkubwa, wamekuwa wakikumbuka maisha yao ya nyuma, kabla hawajafa. Watoto hao wamekuwa wakisema waliishi zamani sana na kufa au kupoteza miili yao na kuja tena kuzaliwa mahali pengine.

Hakuna idadi maalum ya watoto hawa hapa duniani, lakini inadaiwa kwamba, wako wengi kiasi cha kufikia elfu kadhaa. Wanatofautiana pia kiuelewa, wengine wakiwa na kumbukumbu kali na uwezo mkubwa sana kiakili, kuliko wengine, ingawa wote wana ufahamu wa kiajabu.
Kwa nini wameanza kuzaliwa miaka ya 1975? Kuna nadharia nyingi zenye kujibu swali hilo. Moja kubwa ni ile inayohusisha ukuaji wa dunia na ulimwengu kwa ujumla. Kwamba itafika mahali, maarifa mengi yaliyojificha yataibuliwa. Kizazi cha watoto hawa kinadaiwa kwamba, kimekuja kumwonesha binadamu kwamba, amekuwa akiuchukulia ulimwengu na maisha, ndivyo sivyo.

Hivi karibuni mwanasayansi mmoja nchini India, amekiri kwamba binadamu anapokufa, huja kuzaliwa tena na kupewa mwili mwingine . Hii ina maana kwamba, sisi pia tumeshawahi kuishi huko nyuma kabla hatujafa na kurejea tena tukiwa na miili mipya, tuliyo nayo hivi sasa.
Mwanasayansi huyu Vikram Raj Singh Chauhan, amesema ana uhakika ataweza kuthibitisha hilo baada ya kukutana na mtoto wa umri wa miaka sita ambaye anakumbuka maisha yake ya nyuma kwa kiwango kikubwa sana. Mtoto huyo wa kiume, Taranjijt Singh anasema aliwahi kuishi miaka michache nyuma, ambapo alifariki kwa ajali ya pikipiki akiwa bado mdogo.

Mtoto huyo akiwa na umri wa miaka miwili alianza kusema kuhusu maisha yake ya nyuma na alikuwa akitoroka sana nyumbani . Alikuwa akiwaambia wazazi wake kwamba anakumbuka kijiji alichokuwa akiishi na hata jina la shule aliyokuwa akisoma.

Alikumbuka pia jina la baba yake wa zamani {kabla hajafa}. Awali ilionekana kama aina fulani ya kisirani cha mtoto, lakini ilibidi wazazi wake waanze kuwa na wasiwasi kwa kadiri alivyokuwa akiongezeka kiumri.

Mtoto huyo alikumbuka pia siku aliyokufa . Aliwaambia wazazi wake kwamba, alikufa September 10,1992. Alikufa baada ya kugongwa na pikipiki wakati akiwa kwenye baiskeli akiwa anakwenda shuleni asubuhi. Baada ya ajali hiyo alipata majeraha kichwani na alifariki siku ya pili baada ya ajali.

Baba yake wa sasa hivi, Ranjit Singh, anasema, mtoto wake alipozidi kusisitiza kuhusu maisha yake ya zamani, waliamua na mkewe kumpeleka huko kijijini anakodai kwamba, ndiko alikoishi kabla hajafa. Awali hawakuweza kumpata mtu ambaye alikuwa anafanana na maelezo ya mtoto huyu. Mkazi mmoja wa kijiji hicho aliwaomba waende kijiji cha jirani kinachofuata.

Kwenye kijiji hicho walikwenda kwenye shule ya kijiji ambapo mwalimu mkuu wa shule hiyo alithibitisha kamba, September 10, 1992 alikufa mwanafunzi wa shule hiyo kwa ajali ya pikipiki. Kupitia shuleni hapo, walibaini mahali wazazi wa mtoto yule aliyekufa kwa ajali ya pikipiki, walipokuwa wakiishi.

Ni kweli waliwakuta wazazi ambao walithibitisha kufiwa na mtoto katika tarehe na njia iliyoelezwa. Baba wa sasa wa mtoto huyu, Tanjit Singh alieleza kwamba, mtoto wao aliwaambia kwamba madaftari aliyokuwa nayo wakati wa ajali yalilowa damu baada ya ajali ile na alitaja kiwango cha fedha ambazo zilikuwa kwenye mkoba wake wa shule.

Mama wa zamani wa mtoto huyu ambaye kwa maana hiyo ni mama wa mtoto aliyefariki mwaka 1992 aliposikia hivyo aliangua kilio kikubwa , kwani maelezo hayo yalikuwa sahihi bila doa la kosa. Alisema vitabu na fedha hizo bado vipo, kwani aliviweka kwa kumbukumbu ya kifo cha mwanaye .

Baadae mtoto huyu alirudi na wazazi wake wa sasa nyumbani kukiwa na maswali yasiyo na majibu. Wazazi wake wa zamani pamoja na ndugu zake, walikwenda kumtembelea kwao baadae. Mtoto huyu aliibaini picha ya siku ya ndoa ya wazazi wake, ambayo walikuja nayo wakati walipokwenda kumtembelea kwa wazazi wake wapya.

Awali mwanasayansi, Vikram Chauhan, alikataa kukubaliana na maelezo kuhusu mtoto huyu , lakini baadae alijipa moyo wa kuanza uchunguzi. Alitembelea vijiji vyote viwili , cha zamani alikozaliwa na kufa na hiki cha sasa alipozaliwa.

Alizungumza na wazazi wote na kupata maelezo ambayo yalimfanya kuona kuna jambo la maana kuhusiana na kifo na ‘kufufuka' kwa mtoto huyu. Kwenye kijiji alichozaliwa na kufa mtoto huyu, muuza duka mmoja alikiri kwamba ni kweli , mtoto kama huyo alikuwepo na yeye alimkopesha madaftari jana yake na alipogongwa alikuwa akielekea dukani kwake kumlipa madaftari hayo.

Chauhan alichukua sampuli ya mwandiko wa mtoto huyu na ule wa kwenye madaftari ya marehemu. Ilipokwenda kupimwa na wataalamu wa mwandiko, ilibainika kwamba, ilikuwa ni ya mtu mmoja.
Kumbuka kwamba mwandiko wangu hauwezi kuwa sawa na wa mtu yeyote, kama ilivyo alama za vidole. Kila mwandiko una sifa zake maalum ambazo haziwezi kupatikana kwenye mwandiko wa mtu mwingine.

Wataalamu wana uwezo wa kubaini mwandiko wa kughushi hata kama umefanywa na mtaalamu wa kiasi gani wa kughushi miandiko.
Kubwa zaidi ni kwamba mtoto huyu ambaye alishaanza kusoma kwenye maisha yake ya kabla ya kifo, hivi sasa hajapelekwa shule, kwa sababu familia yake ya sasa ni maskini. Hata hivyo katika jambo la kushangaza zaidi alipotakiwa kuandika alifabeti za kiingereza na ki-punjabi aliweza kufanya hivyo bila tatizo. Kama hajasoma ingewezekana vipi kufanya hivyo? Anatumia akili ya zamani ya kabla hajafa.

Familia yake ya zamani imeomba kukabidhiwa mtoto wao, lakini familia yake ya sasa imesema hapana, huyo ni mtoto wao. Kisheria, bila shaka, familia yake ya sasa ambayo ni maskini sana, wakati ile ya zamani ilikuwa na uwezo, ndiyo yenye uhalali wa kuishi na mtoto huyu.
Huenda baada ya sayansi kuthibitisha kwamba watu hufa na baadae kurudi wakiwa wanamiliki miilia tofauti, familia kama hii ya zamani ya mtoto huyu, ndipo itakapoweza kupata haki.

Hata hivyo, bila shaka kila familia kati ya hizo mbili, itakayoishi naye, itakuwa na mashaka ya aina fulani.

Mwanasayansi kama Chauhan na wengine wanaamni kwamba, kama roho ikihama kutoka mwili mmoja na kwenda mwili mwingine, huenda huko na akili au mawazo na hisia pia. Kinachoachwa ni mwili unaoonekana, lakini hiyo miili mingine huwa pamoja. Hii ina maana kwamba, hata mwandiko utabaki kuwa uleule kama ilivyokuwa.
Chauhan anasema, hivi sasa anao ushahidi wa kisayansi kuthibitisha kwamba, binadamu anapokufa, huja kuzaliwa tena, lakini hutumia mwili mwingine. Hata hivyo anasema anahitaji muda zaidi kuthibitisha jambo hili.

Bila shaka, ushahidi wa wazi kabisa kuhusu watoto hawa wa indigo, unaweza kutuonesha kwamba, tunapokufa, maana yake tumepoteza mwili , lakini bado hisia, akili, na roho ambavyo huja kuingia kwenye mwili mwingine ambao utatengenezwa na wazazi wengine wawili au wale wale, vinakuwepo.

Ni vigumu kupingana na maelezo ya mtoto huyu, ambaye tangu akiwa na umri wa miaka miwili, alikuwa akizungumzia kuhusu kumbukumbu alizonazo juu ya maisha yake ya nyuma. Ugumu wa kupinga unatokana na ukweli kwamba, hatimaye maelezo yake yalithibitika.
Kama ingekuwa Chauhan sio mwanasayansi, tungeweza kusema, suala hili bado, halijatazamwa kisayansi na hivyo, haliwezi kuelezewa kama jambo halisi.

Kwa mwanasayansi kuvutiwa na jambo hili na kuanza kulifanyia utafiti huku akikiri kwamba, kuna mambo yenye kutanza, ni hatua kubwa katika binadamu kuingia mahali ambapo atabaini ukweli wa kuwepo maisha baada ya kifo.

Lakini sio maisha baada ya kifo peke yake bali pia kukubali kwamba huenda binadamu ataendelea kuwepo, kwa sababu uwepo {being} haujapotea na hauwezi kupotea. Mwili wako utaharibika, lakini uwepo wa binadamu hauwezi kupotea.
 
Unaijua lakini vizuri historia ya Nimrod, haswa imani yake?

Hope unaipata japo kidogo_hebu imwage hapa kwa faida ya wanajamvi mkuu.

Maake huyu jamaa i.e Nimrod_hawa wajenzi huru nao wanamhusisha na imani yao mara huku kwa marasta tena naona wanamconnect nako.
 
Hebu tuwekeeni hapa japo kidogo kwa faida ya wanajukwaa mkkuu

Kwanza ili tumfahamu vema Nimrodi nivema tukaanza kurejea nyuma kwanza kuyajua haya,

Wazungu 90% ni Majini:


Kwakutumia historia ya binadamu kibiblia, ukichambua kila uzao na sambuli zake unaweza kubainisha wazi hilo nilisemalo, japo laweza kuwa zito kwa wengine.


Kwa wale muaminio biblia mnaweza kukubaliana na mimi kuwa sababu kuu ya Mungu kuiangamiza dunia enzi za Nuhu, ni kutokana na wanadamu kumuasi mungu, maasi yalikuwa yakufuru hasa yakihusisha mwingiliano wa majini na binadamu, wanyama na binadamu nk na baada ya angamizo hilo, manusura walikuwa ni Nuhu, wanawe, mke wake, na kila kiume kibaya na chema aliviokoa mke na mme. Mwanzo 7:1-11


Hapa tunaona kuwa na majini yaliokolewa na Nuhu, Sasa tukirejea katika masimulizi yetu tunaona sasa baada ya Nuhu kuokolewa na safina, wanae watatu wakiume ambao tayari walikuwa wameoa (enzi za gharika) mmoja wao Yafethi alikuwa kaoa jini, wakati wawili Shemu na Hamu wao biblia inasema walioa mahali ambapo si chukizo mbele za Mungu. Mwanzo 10:1-7


Uzao wa wana wa Nuhu ndio unatupatia ukweli wa nikisemacho, kwanza tunaona kuwa wana wa Yafethi alieoa jini ni, Gomeri (Ujerumani), Magogu (Cambridge UK ), Madai (Hispania), Yavana (Italia), Tubali au Yunani (Ugiriki), Mesheki (Lebano) na Tirasi (Ufaransa), Mpaka hapotumeona uzao wenye ushirika na majini wa Yafethi

Sasa tuangalie uzao Hamu unaotajwa kuwa Mungu aliupenda na kuupa baraka tele, uzao huo ni Kushi (Ethiopia), Misri (Misri), Kanaani (Israel) na Putu (Libya)

Mwanzo 10:21-23
Tunasoma yakuwa wana wa Shemu ambe ni sehemu ya kipenzi cha Mungu, ni Elamu (Saudi Arabia), Ashuru (Syria), Arfaksadi (Kuweit), Ludi (Jordan), na Aramu (Qatar)

Mpaka hapo tumepata mwangaza kuwa uzao wa Yafethi wenye tokezo la majini/uovu ndio uzao wa mataifa karibu yote ya Ulaya. nauzao wa Hamu na Shamu ndio uzao uliopewa neema na muumba hii ni kwamujibu wa maandiko ya kiroho.

Kwamaandiko hayo tunaamini kabisa kuwa Mashariki ya kati, na Afrika ndio maeneo muhimu ambayo mungu aliwabarikia watu wake.


Hata ukitumia Kuruani takatifu hayo yote yanabainisha wazi kabisa.

Kwamsaada zaidi rejea Mwanzo 4:16-24, Ufunuo 16:13-15, Ufunuo 20:7-8, Ezekieli 27:12-14, Ezekiel 38:1-9


Kwakupanua wigo wa mjadala nje ya biblia hasa wale wenzangu waaminio Freemasonry ijapokuwa watetezi wake hupinga kuwa si ushetani/ujini, watambue kuwa uzao wa asili wa freemasonry ni Magogu (Cambridge UK) japo katika historia inasema ni Scotland UK

Haya ndugu zangu nawakaribisha katika tafakuri njema
 
Rastafarian asili yake ni Tafari-Ras!

kulikoni kuupotosha ukweli au kupost usilolijua ni bora kukaa kimya!

Naaam mkuu wangu,

Punguza jazba kisha tulia kwa nera ya juu!

Unaonekana unayo mengi mazuri yakuwasomesha marastafari,

Hebu tumwagie hapa mkuu, huo ndio msingi wakujibu maandiko na sio mkato!
 

ahahahahahahhaaaaaaaaaaaa_nakumbuka thread yako moja ilibeba ujumbe huu wa majini kuwa wazungu,...with thanks mkuu
 
Hehee ndio tunaamini kupitia maandiko hayohayo

Yeah_maandiko hayo hayo waliyotuletea wenyewe na kutukaririsha with porojo nyingi_ambayo wametuachia sisi na wao kuendelea na dini mpya in the name DEMOKRASIA....sisi huku tukiuana bila kujua chochote mkuu.
 
Yeah_maandiko hayo hayo waliyotuletea wenyewe na kutukaririsha with porojo nyingi_ambayo wametuachia sisi na wao kuendelea na dini mpya in the name DEMOKRASIA....sisi huku tukiuana bila kujua chochote mkuu.

Machafuko ya kiimani yamebaki kuwa sehemu kuu ya janga la mataifa ya dunia ya tatu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…