Mbahili
JF-Expert Member
- Nov 28, 2016
- 281
- 525
Awali ya yote, napenda kutumia fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kunifikisha siku hii ya leo na pia sitakuwa mtenda haki bila kuwashukuru waanzilishi wa forum hii. Baada ya kusema hayo machache, ningependa kukushukuru na wewe unaetumia gharama zako kusoma uzi wangu, huenda kuna mabadiliko ninayoweza kukuletea katika fikra yako hasa nitakachojadili hapa hususan kisiasa.
Kwa kusema hayo ,napenda niende moja kwa moja kwenye mada yangu. Mada yangu nitatumia marejeo tofauti, hivyo msishangae pia. Ninaweza anza na mifano michache.
Mfano wa kwanza
Tulipokuwa wadogo na kwenda kwa wajomba zetu, namaanisha mboga saba, wanakula kwa wakati na chakula kweli kizuri, Tunakaa kwa takribani mwezi mzima. Tukirudi nyumbani ratiba inayojirudia ni ugali, maharage, chai bila vitafunwa na pasi ndeeefu( nahisi naeleweka). kuna muda kama mtoto unaweka pingamizi flani moyoni, na unamiss urudi kwa mjomba au siyo? kile kitendo cha kutoridhika na ratiba ya chakula nyumbani na ku pamiss kwa mjomba, basi huo huitwa upinzani.
Huenda sisi ni familia moja ila unagoma kula chakula hicho na kuhamasisha japo tule kama kwa mjomba.
Mfano wa pili
Katika maandiko matakatifu, tunaambiwa kilichotokea mbinguni kwa shetani kufikiri kutaka kurithi kiti cha Enzi cha Mungu, hapo tunaona Shetani na Mungu wakawa Maasimu wakubwa. Ila cha kushangaza zaidi tukisoma katika kitabu cha Ayubu tunaambiwa Shetani kakutana na Mungu na Mungu kumtambia mjakazi wake Ayubu. Haiwezekani kuwa ilikuwa mara ya kwanza kwa Mungu kukutana na Shetani, kwa sababu maongezi yao yalionekana kama huwa wanazungumza mengi sana. Tunaona kama Mungu na Shetani ni Maasimu, lakini huwa wana mazungumzo so inshort sio Maadui kama tunavyoaminishwa. Hapa Tumejifunza kumbe upinzani sio uadui?
SWALI LETU
JE, UPINZANI NI NINI?
Neno UPINZANI umetikana na kitenzi PINGA, kwa wale wenzetu wa |the school bus| wanaita be AGAINST. Upinzani ni hisia, upinzani si ugomvi, si uadui, si vita, si Usaliti. ila upinzani ni hisia. Kwa sasa tuna bunge la chama kimoja, wanazungumza lugh moja, wana mwenyekiti mmoja, wana kila kilichofanana sawa. Akina Lema, Zitto, Heche, Sugu hawapo bungeni tena. Je hili limeua chama pinzani au limewapa sifa? Tunaweza sema, Limewapa sifa, ukiwa mchunguzi wa mitandao watu hufuatilia Lema, Lissu, Mbowe waliwahi sema nini bungeni?
kwa sababu upinzani sio Chama bali upinzani ni hisia. Bungeni hawazungumzi Lugha moja kama mipango walivyoweka, wabunge wanatengeneza makundi mengine mingi ndani ya Bunge. Kuna watu wanaunda timu na sio kuwa ni wabaya, bali ndio hulka za binadamu. Huwezi mzuia mtu kuwa mpinzani sababu upinzani sio chama, sio dhambi, sio uadui. BALI UPINZANI NI HISIA.
Naomba kuwasilisha, unaweza nipata kwa njia ya email kama [hermanwilliam06@gmail.com]