Maana ya Mistari ya mikono ya kushoto na kulia, picha na decoding

Maana ya Mistari ya mikono ya kushoto na kulia, picha na decoding

  • Life line: huu mstari unasimamia afya na uhai. ( Rangi ya Kijani)
  • Heart line: huu mstari unasimamia mapenzi(upendo) na hisia (Rangi ya Pinki)
  • Money line: huu mstari unasimamia kazi na bahati. (rangi ya Zambarau)
  • Head line: huu mstari unasimamia akili. (rangi ya Bluu)
  • Marriage line: maisha ya ndoa na mahusianio. (Rangi ya Nyekundu)[emoji176][emoji818]
 
Hakuna nilichoelewa
* Life line: huu mstari unasimamia afya na uhai. ( Rangi ya Kijani)
  • Heart line: huu mstari unasimamia mapenzi(upendo) na hisia (Rangi ya Pinki)
  • Money line: huu mstari unasimamia kazi na bahati. (rangi ya Zambarau)
  • Head line: huu mstari unasimamia akili. (rangi ya Bluu)
  • Marriage line: maisha ya ndoa na mahusianio. (Rangi ya Nyekundu)
 
Nimeangalia picha zote nankufananisha na kiganja changu ila kuna hata moja iliyokaribia kufanana na kiganja changu so huu uzi ni utopolo tu.
 
Inakuwaje pale mtu hana kazi ya kueleweka,maisha yake analima mbogamboga na Moneyline ndio umejaa kisawasawa,maisha magumu balaa...
 
Sasa mimi mbona sina iyo line ya mapenzi na kweli bado nipo single
 
View attachment 2331092
Usomaji wa alama za viganjani ulianzi nchini India na sasa ni maarufu sana duniani kote kama njia ya mtu kujua hatima ya mtu hapa ulimwenguni. Usomaji hufanyika kwa kuangalia mistari, umbo la kiganja na rangi pia.

Mistari hiyo kama inavyoonekana kwenye picha hapo mwanzo inawakilisha vitu vifuatavyo:
  • Life line: huu mstari unasimamia afya na uhai. ( Rangi ya Kijani)
  • Heart line: huu mstari unasimamia mapenzi(upendo) na hisia (Rangi ya Pinki)
  • Money line: huu mstari unasimamia kazi na bahati. (rangi ya Zambarau)
  • Head line: huu mstari unasimamia akili. (rangi ya Bluu)
  • Marriage line: maisha ya ndoa na mahusianio. (Rangi ya Nyekundu)
Kuna msemo usemao kwamba mkono wa kulia ni wa kike na wa kushoto ni wa wanaume katika usomaji wa viganja. Hii ni kwa sababu upande wa mkono wa kushoto unahusishwa na wanaume na upande wa kulia na wanawake katika mila za Kichina.

Katika usomaji wa kawaida wa mistari hiyo, jinsia hupuuzwa. Inaaminika kuwa mkono wa kulia ndio mkono mkuu kwa watu wengi na unawakilisha wakati wa sasa na siku zijazo, wakati mkono wa kushoto unawakilisha siku za nyuma na sifa ambazo mtu alizaliwa nazo.


Ni muhimu zaidi kusoma mkono wa kulia, isipokuwa kama unatumia mkono wa kushoto, ingawa mikono ya watu wengi ni linganifu (yenye tofauti ndogo ndogo).

Muuonekano wa kwanza ya mistari ya viganja ni Rangi. Rangi ya mistari ikiwa angavu na yenye kuonekana vizuri inaashiria bahati nzuri.
Sasa nyosha kiganja na tusome mistari mitano mikuu mmoja baada ya mwingine.

1. Life line: Afya na Uhai. (Mchoroni ni Rangi ya Kijani)

Mstari wa maisha ni mstari unaoenea karibu na kidole gumba. Kawaida unafanana na theluthi moja ya duara zima (arc). Urefu wa mstari wa maisha hauna uhusiano na muda gani mtu anaishi. Inaonyesha afya ya mtu na uchangamfu wa kimwili.
1a.
View attachment 2331162
Tukianzia kushoto mwa mchoro; Ikiwa mstari wa maisha una arc kubwa na inaonekana wazi, inamaanisha mtu huyo ni mwenye nguvu. Kadiri mstari wa maisha unavyozidi mrefu ndo vile sifa hii huzidi kuwa bora. Watu walio na mstari wa maisha mrefu kawaida huwa wazuri katika michezo.

Kulia mwa mchoro; Ikiwa mstari wa maisha ni mfupi na uko karibu na kidole gumba, ni ishara kwamba yeye huchoka na kuchoka kirahisi.

1b.
View attachment 2331176

Mchoro Kushoto; Ikiwa kuna zaidi ya mstari mmoja wa maisha, hii pia inaonyesha kwamba mtu huyo amejaliwa/atajaliwa maisha marefu.
Mchoro Kulia; Ikiwa mwanzo wa mstari wa maisha (karibu na kidole gumba) umevunjika, basi yeye alikuwa mgonjwa wakati wa utoto.

1c.
View attachment 2331179
Tukianzia Kushoto; Ikiwa mwisho wa mstari wa maisha (karibu na kifundo cha mkono) unaonekana kuwa umechambuka au dhaifu, anapaswa kuzingatia sana shida za kiafya anapozeeka. Kuna uwezekano wa kupata matatizo ya kiafya hasa uzeeni.
Mchoro Kati; Ikiwa kuna mduara (kama kisiwa) kwenye mstari au mstari umekatwa mahali fulani, anaweza kuumia kimwili/kupata ajali au kuwa kulazwa hospitalini kutogana na magonjwa. Ukubwa wa duara huonyesha uzito wa ugonjwa/jeraha.
Mchoro Kulia Pichani; Ikiwa mstari wa maisha ni mnyoofu na upo sambambana na mstari wa kichwa, yeye ni jasiri na kwa kawaida ana hulka ya urafiki na utu.

2. Heart line: mapenzi(upendo) na hisia (Rangi ya Pinki)
Mstari wa moyo, wakati mwingine huitwa mstari wa upendo, ni mstari unaojichora kwenye mkono moja kwa moja chini ya vidole. Mstari wa moyo huakisi mambo yanayohusiana na moyo, kama vile hisia, miitikio, udhibiti wa kihisia, n.k.
Kadiri inavyozidi kuwa ndefu na kunyooka ndivyo inavyokuwa bora zaidi.

Ikiwa mstari wa moyo ni mfupi na umenyooka, mtu huyu ana nia ndogo katika kuonyesha upendo au mahaba.

Ikiwa mstari wa moyo ni mrefu, atakuwa mapenzi mazuri/ya dhati, na mwenye ufahamu wa kina wa mapenzi.
2a.
View attachment 2331213
2a.i Ikiwa mstari wa moyo huanza kutoka kwa kidole cha shahada/nne, mtu huyu anatabiriwa mapenzi/mahusiano yenye furaha.
2a.ii Ikiwa inaanza kutoka kwa kidole cha kati, inamaanisha mtu huyo kwa kawaida anajifikiria zaidi kuliko mpendwa/wapenda wake (yani ni mbinafsi).
2a.iii Ikiwa mstari wa moyo huanza kati ya kidole cha kati na kidole cha pete, atapenda kwa urahisi.

2b.
View attachment 2331226
2b.i Ikiwa mstari wa moyo una kupanda na kushuka kama wimbi kwa kiasi kikubwa, huenda mtu huyo ataanguka kwenye mahusiano na watu kadhaa. Mahusiaono yake hudumu kwa muda mfupi.
2b. ii Ikiwa kuna duara moja au zaidi kwenye mstari wa moyo au umegawanywa katika sehemu kadhaa, au kuna baadhi ya mistari miembamba miembamba inayovuka mstari wa moyo, kwa kawaida inamaanisha kuwa hafurahii sana maisha yake ya sasa ya mahausiano/upendo.


3. Money line: kazi na bahati. (rangi ya Zambarau)
Mstari wa pesa, unaoitwa pia mstari wa hatima, ni mstari unaoenea kutoka kwenye kofi hadi kidole cha kati. Huu Unaonyesha bahati na kazi ya mtu.
3a.
View attachment 2331248
3a.i Ikiwa mstari wa pesa na wa maisha huanzia kwenye sehemu moja , mtu huyo kwa kawaida ana tamaa ya kufanikisha jambo na anajiamini sana.
3a.ii Ikiwa kuna mistari miwili ya pesa, anaweza kuwa na kazi mbili kwa pamoja au kazi na biashara pembeni.

3b.
View attachment 2331251
3b.i Ikiwa mstari wa pesa unaonekana ang'avu na mnyoofu, kwa kawaida ina maana ya maisha mazuri yanakuja na ya bahati nzuri. Kwa kawaida hahitaji kufanya mambo mengi kubadilisha maisha yake na maisha yanakuwa shwari.
3b.ii Mstari wa pesa wa watu wengine umegawanyika katika sehemu mbili au zaidi. Ina maana pengine atabadilisha kazi mara kwa mara au maisha/kazi yake itakuwa na mabadiliko makubwa.
Ikiwa mstari wa pesa ni mfupi, inamaanisha anaweza kuacha kufanya kazi kabla ya kustaafu.

4. Head line: huu mstari unasimamia akili.(rangi ya Bluu)
Mstari wa kichwa, huonyesha akili na mawazo ya mtu. Kwa kawaida huanza kati ya kidole cha shahada na kidole gumba (chini ya mstari wa mapenzi) na kisha kunyoosha hadi upande mwingine wa kiganja, ikionekana kana kwamba inagawanya kiganja kwa nusu.
View attachment 2331260
4a.i Ung'avu, wembamba, na urefu wa mstari wa kichwa huonyesha umakini wa kiakili na werevu.

4a.ii Arc kubwa ya mstari wa kichwa inatuambia kwamba yeye ni tajiri katika ubunifu.

4a.iii Mstari mfupi wa kichwa kwa kawaida unamaanisha kuwa mtu ana nafasi zaidi ya mafanikio ya kimwili kuliko yale ya kiakili.

4b
View attachment 2331263
4b.i Ikiwa kuna mduara kwenye mstari wa kichwa, au mstari wa kichwa hukatwa vipande viwili (au zaidi), au mstari wa kichwa una mawimbi, mtu huyu ana kumbukumbu mbaya ya kulinganisha mambo, pia atasumbuliwa kwa urahisi na watu wengine, na kwa kawaida hawezi zingatia/kufanya kitu chochote kwa muda mrefu.

5. Marriage line: maisha ya ndoa na mahusianio. (Rangi ya Nyekundu)
Mstari wa ndoa ni mstari mfupi unaochomoza mara moja chini ya kidole kidogo. Inaakisi mahusiano ya kimapenzi na ndoa ya mtu.

Watu wengine wana mstari mmoja tu wakati wengine wana mistari kadhaa. Idadi ya mistari haimaanishi chochote. Zingatia tu mstari unaoonekana vizuri zaidi.
5a.
View attachment 2331274
5a.i Ikiwa kuna mistari miwili ya ndoa iliyo wazi/ang'avu kwa usawa wa urefu, mtu huyuanahitaji kuwa mwangalifu na pembetatu ya upendo. Pembe tatu hii ipo kiganjani, na ina tafsiri yake. Nitaiielezea huko mbeleni.

Ikiwa kuna mistari kadhaa ya ndoa bila kuwa na msatri mkuu (hapa inakua mistari mingi yenye kufanana), maisha yake ya ndoa yanaweza yasiwe ya kufurahisha.

5b.
View attachment 2331278
Ikiwa mstari umejikunja kuelekea juu au ni mfupi na umefifia, kwa kawaida mtu huyu hataoa au kuolewa mapema.

5c.
View attachment 2331280

5c.i Ikiwa mstari wa ndoa umeenea hadi kati ya kidole kidogo na kidole cha pete, mtu huyu ana vigezo vya juu wakati wa kuchagua mwenzi. Wanachagua chagua sana tabia, muonekano na hali za wapenzi.

5c.ii Ikiwa mstari wa ndoa umeenea kwenye kidole cha pete, inatabiri kwamba familia ya mwenzi wake ni tajiri na rafiki kwake.

5c.iii Ikiwa mstari umenyooka na umepitiliza mpaka kwenye kidole cha kati, hii sio sifa nzuri. Huenda tabia na bahati nzuri vinaweza kuathiriwa na ndoa.

5d.
View attachment 2331288
5d.i Ikiwa kuna kisiwa (kama mduara) kwenye mstari wa ndoa, wanandoa wanaweza kuishi mbali kwa sababu fulani kwa muda.

5d.ii Ikiwa mstari wa ndoa umegawanyika katika sehemu mbili chini ya kidole kidogo, anapaswa kuzingatia usimamizi wa upendo, kwani wanandoa wanaweza kuachana.

Mistari Adimu: Kiganja cha Kukata
View attachment 2331293

Kiganja cha kukata (nusu-kiganja): Jambo hili hutokea wakati mstari wa kichwa na mstari wa upendo unapokuwa karibu sana kana kwamba inaonekana kama mstari mmoja tu mnene unaokata kwenye kiganja.
Kuna msemo mmoja nchini China usemao: “Mtu aliye na mstari huu atakuwa na kazi nzuri; kama ni mwanamke mwenye kiganja hiki kwa kawaida huwa huru kiakili.”

Masomo ya Wakaldayo wa Babylonian ya Nabuchadnedza. Elimu hii walifunzwa na Wanefili (fallen angels).

Wakaldayo wale pia walikuwa na masomo ya kufundisha kuongea na wafu, kusoma na kutambua nyota (of course ndio waanzilishi wa hii zodiac system tunayoijua Leo). Mambo ya Kupiga Ramli n.k.

Elimu hizi na zinazofanana nazo zilishamiri mno wakati wa Nabuchadnedza maana yeye aliasisi taasisi na vyuo maalum kuendeleza hizi Shughuli.

Swali ni je, elimu hii inatija?


Jibu ni Hapana maana Wafalme waliokuwa wakitumia elimu hizi walifika mahali wakakwama hasa walipopata maono ya kiroho kuhusu tawala zao. Pharao alipopata ndoto kuhusu ng'ombe 7 walionawili na ng'ombe saba wenye njaa aliwaita waganga wake wenye hizi elimu, lakini hawakuweza kumfungulia ndoto yake Ile. Ndoto yake ilijibiwa na mtumwa Joseph mwana wa Jakob aliyesema uwezo wa kutambua mambo ya kiroho upo kwa Mungu pekee.

Nabuchadnedza pia alijipata na maono ya kiroho, akaita waganga wabobezi na maprofesa wa elimu ya Kikaldayo lakini hawakuweza kumfaa. Ilibidi aletwe mkimbizi Daniel ili kutafsiri ndoto husika. Daniel alimwaambia Nabuchadnedza kuwa mwenye kujua maono ya rohoni ni Mungu tu.


Tufanyeje sasa?
Hizi elimu na masomo ya Wakaldayo ni mambo yanatuchelesha kufikia full potential zetu. Tumtafute Mungu, muumba wa mbingu na dunia na vitu vyote vilivyomo. Yeye anajua wapi aliweka nguzo za kuisimamisha dunia kwenye mhimili wake. Yeye anajua atatufungulia vipi mengi yajayo tusiyoyajua.

Mungu na atujalie word of knowledge.
Mungu na atujalie word of wisdom.

If we do this, we will do well!
 
Back
Top Bottom