Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Wengi wanapenda kuitwa 'boss' makazini, bila kujua uzito wa hilo jina. Wengine wanalazimisha waitwe hivyo, na wengine inatokea tu wanaitwa hivyo kutokana na wanavyotatua kero za wafanyakazi wao hasa kimaslahi.
Wenye kulipenda hilo jina wengi wao wanafikiri kuitwa 'boss' ni kuwa na uwezo wa kuajiri na kufukuza tu; huu ni uelewa mbaya sana. Kuwa 'boss' maana yake una uwezo mkubwa wa kiakili wa kuweza kuiwezesha kampuni yako kujiendesha kifedha na kutatua changamoto zozote zinazoweza kujitokeza kwa wafanyakazi/watumishi wako, pamoja na taasisi au kampuni yako kwa ujumla, kujiendesha kwa faida.
Utajisikiaje pale wewe ni 'boss', mfanyakazi wako anakuletea changamoto zake zinazohitaji fedha, mfano; kuuguliwa na familia, nyumba kuungua, kukosa kodi ya pango, kuishiwa hela ya chakula n.k ,na ukashindwa au ukakosa uwezo wa kutatua kero zake. Je kwa mazingira hayo, wewe ni 'boss' au ni 'box'
Tujifunze kuwa na mahusiano mazuri na wafanyakazi/watumishi tunaowasimamia.