Maana ya Pete ya Mvuvi "Fisherman's Ring" ya Papa Leo 14 Aliyopokea Aliposimikwa Rasmi leo

Maana ya Pete ya Mvuvi "Fisherman's Ring" ya Papa Leo 14 Aliyopokea Aliposimikwa Rasmi leo

Kindred Spirit

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2023
Posts
457
Reaction score
666
Tunaposema Kanisa Katoliki ( hapa nitaita tu kwa ujumla kanisa) lina utaratibu wake haimaanishi ni taratibu zilioibuka tu. Wengi ambao siyo Wakatoliki au hata Wakatoliki "lukewarm" wanaweza kuyumbishwa na madai kwamba kanisa linafanya mambo nje ya Biblia, wakati si kweli hata kidogo.

Kusema ukweli, kila ambacho kinafanywa na kanisa kinatokana na Biblia yenyewe. Kila kitu ukifutilia kina msingi wake kwenye Biblia na hasa katika Injili ya Yesu Kristo mwenyewe, lakini pia Matendo ya Mitume na kwingineko. Kama vile kuhusu Pete ya Mvuvi maarufu kama Fisherman's Ring ambapo Papa mpya hupewa anaposimikwa.

Tumeshuhudia leo Papa Leo XIV akiwa very emotional wakati anapokea pete hii akiiangalia mara kadhaa na visibly akionekana kufight machozi.

Inatokana na maana yenyewe inayotoka kwenye Injili mfano Luka 5 (na vitabu vingine vya Injili). Hapa ni wakati Yesu ndo kwanza anaianza kazi yake na anakusanya wanafunzi wake wale thenashara.

Hapa Petro tunaona anavyokabidhiwa jukumu na Yesu alipowakuta wanavua samaki. Hapa hata hawajaanza kufanya kazi pamoja. Petro anahangaika zake tu kutafuta maisha na kazi yake ya uvuvi.

Ilianza hivi: Yesu aliomba boti ili aweze kuongea vizuri na makutano, akapewa boti ya Simoni Petro. Alipomaliza kufundisha mkutano wake akamshauri Petro arushe tena nyavu zake, wakati huo jamaa alishafunga kazi siku hiyo na alishasafisha nyavu zake tayari kujiondokea, yumkini walikuwa wanasubiri tu Yesu amalize kuongea wasepe zao.

Kwa maneno yake Petro alimjibu Yesu akisema "Bwana mkubwa, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha, lakini kwa neno lako, nitashusha nyavu" (Luka 5:5)

Petro alipofanya hivyo na wavuvi wenzake, hawakuweza tena kuvuta zile nyavu, maana walikuwa wamekamata samaki wengi sana, na hadi nyavu zikaanza kuchanika, hali iliyowalazimu kuomba msaada kwa wavuvi wengine waliokuwa karibu.

Wakajaza boti mbili nazo hata zikataka kuzama kwa uwingi wa samaki.
Hali hii ilimshangaza sana Petro na wenzake hadi kupata hofu.

Lakini Yesu akamwambia specifically Petro. ...." Usiogope, tangu sasa utakuwa mvuvi wa watu" (Luka 5:10)

Ikaishiaje: Biblia inasema Simoni Petro, Yakobo na Yohane wana wa Zebedayo waliacha kila kitu wakamfuata yesu, yaani walitelekeza boti na samaki na kila kitu baada tu ya kuzivusha nchi kavu palepale wakawa moja ya wanafunzi wale 12. Huenda wale wavuvi wengine waliachwa wahangaike na wale samaki.

Mwishoni nako mwa utume wa Kristo kabla hajauliwa anarudia tena kwa Petro na kumkabidhi funguo za mamlaka na kuwatunza kondoo wake. Yesu alikuwa very specific kuhusu Petro tangu mwanzo hadi mwisho.

So hapa kanisa linaendeleza kile ambacho Yesu mwenyewe alikianzisha. Hapa Papa anakabidhiwa jukumu kubwa la kuwa "mvuvi wa watu".

Ni lazima kanisa libaki na Petro muda wote. Ni lazima kuwa na mvuvi mmoja wa watu, ni lazima kuwa na mtu mwenye "funguo za mamlaka", ni lazima kuwa na "mchungaji wa kondoo wa Bwana". Kwa kufanya hivyo kanisa nimebaki imara tangu enzi za akina Petro na wenzake.

Tumeshuhudia "makanisa" mengine yaliyojimega kutoka Kanisa Katoliki yakivunjika vipande tena na tena na tena kwa kukosa mwongozo huu. Leo hii tunazungumzia maelfu ya denominations za Kikristo. Sivyo Yesu alivyotaka. Yeye alifanya kazi kama timu na wanafunzi wake, hawakugawanyika kila mtu akaanzishe kundi lake, alipowatuma walienda kwa mamlaka yake. Walipobaki wenyewe walikuwa pamoja pia hata kama walitawanyika maeneo mbalimbali. Kristo akiwa juu then Petro then hierarchy inashuka hivyo kama ilivyokuwa wakati wa Kristo, kanisa moja takatifu la Mitume!

Ni ngumu kubaki stable pale kila mtu anapoclaim mamlaka, ngumu sana maana mnakuwa na kelele nyingi za wachungaji huyu anasema kondoo waende huku na huyu huku na huyu huku na matokeo yake ni kondoo kupoteza mwelekeo.

Mfano leo tunashuhudia kiongozi mmoja anakemea serikali na mwingine anaibuka kutetea hayohayo ambayo mwingine amekemea, tunaumiza, kugawanya na kuwachanganya waumini.

Au kwa lile tukio la padre kupigwa, kanisa lilitoa waraka mmoja kwa majimbo nchi nzima na maamuzi yalikuwa wazi tunasubiri uchunguzi. Unaona tukio kama hilo lifanyiwa maamuzi kuanzia juu kabisa, siyo kila parokia au jimbo litajiibukia na maelezo yake, ndo maana unaona kumetulia tuli nchi nzima licha ya ukweli kuwa lilikuwa tukio baya sana. Katika umoja hata migogoro inapojitokeza ni rahisi kupatiwa ufumbuzi sahihi, lengo ni kuchunga kondoo wa Bwana wasitawanyike.

Katika kanisa, masomo ya kila siku yanasomwa dunia nzima, kila Mkatoliki anapata kujifunza kwa lugha yake, same message. Hili siyo jambo dogo, unaona kabisa Roho Mtakatifu amehusika kufikia level hii, maana kiubinadamu siyo rahisi. Maan waliojaribu nje ya hapa wameishia kuwa vipande vyenye maelfu ya makanisa kila mmoja akidai yuko sahihi na kuwakosoa wengine. But RC imebaki kama ilivyokuwa mwanzo.

Au namna kanisa lilivyobaki stable karne baada ya karne licha ya allegations za kila namna zinazosemwa, kubezwa na kuhubiriwa kila siku dunia nzima. Yaani upigwe mawe kiasi hiki na bado umesimama imara, not easy!

Basi tukiwa tunasherehekea kumpata mrithi wa Mvuvi wa Watu duniani kote, tunamshukuru Mungu sana kwa namna Roho Mtakatifu anaendelea kutenda kazi yake ndani ya kanisa ambalo limechagua kufuata nyayo za Yesu Kristo mwenyewe!
 

Attachments

  • Screenshot_20250518-170606_Google.jpg
    Screenshot_20250518-170606_Google.jpg
    192.2 KB · Views: 38
Usitudanganye. Co kweli kwamba kila kinachofanywa na kanisa katoliki kimeelekezwa kwny biblia,
Tuanze na hili, utaratibu wa kumpata papa umeelekezwaje kwny biblia? Kile tunachokishuhudia (uchaguzi) ndicho kilichoelekezwa kunako biblia?

Halaf nakuuliza ww, bila shaka (umeoa au kuolewa)? Hilo fundisho la ww kuoa au kuolewa, limefundishwa wapi kwny biblia? Sifa za mtu kuoa au kuolewa, zimeelekezwaje kwny biblia?

Namna ya kuzika, biblia inatuelekezaje juu namna gani ktk kuzika? Msingi wa swali langu unaanzia hapa, yesu alizikwa na sanda. Je, leo hii kanisa katoliki linawazika watu wake ktk sanda?

Leo hii kanisa katoliki halimziki mtu asiyeenda kanisani au kwny jumuia? Hili limekaaje? Biblia inatufundisha nini juu ya hili?
ZINGATIO: MASWALI YANGU YOTE YAMEJIKITA KATIKA MAELEKEZO YA BIBLIA
 
Back
Top Bottom