JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Hisa zikishatolewa na makampuni ya umma haziwezi kurudishwa mpaka kampuni itakapofilisika. Lakini hisa zinaweza kuhamishwa kutoka mmiliki mmoja kwenda kwa mmiliki mwingine.
Hivyo kama mtu anayemiliki hisa atahitaji kubadilisha hisa zake kuwa pesa hatoiomba kampuni kumfanyia hivyo bali atatafuta mtu anayehitaji kununua hisa kisha mtu huyo atampatia yeye pesa na kampuni itabadilisha jina la mmiliki wa hisa.
Ongezeko la wanaohitaji kuuza na kununua hisa likapelekea kuanzishwa kwa soko la hisa ambalo ni mahususi kwa kuuza na kununua hisa ambazo zilikwisha tolewa.
Sababu za kushuka na kupanda kwa bei ya hisa ni kama zifuatazo:-
Kutegemea zaidi utendaji wa kampuni. Kama kampuni inaingiza faida kubwa bei ya hisa itapanda kwakua watu wengi watahitaji kununua.
Kuungana kwa makampuni kunaweza kupelekea kubadilika kwa bei ya hisa.
Maendeleo ya bidhaa mpya katika kampuni hupelekea bei ya hisa kupanda. Wakati huo huo maendeleo ya bidhaa mpya za kampuni iliyo kwenye ushindani na kampuni hiyo inaweza kupelekea kushuka kwa bei ya hisa.
Sera ya Serikali juu ya tasnia fulani inaweza kuathiri bei ya hisa kwenye makampuni yaliyo katika tasnia hiyo. Mfano kutaka bei za magari kushuka hupelekea kushuka kwa bei za hisa kwenye makampuni yanayotengeneza magari.
Hali ya uchumi kwa ujumla huathiri bei ya hisa.
Uhitaji wa faida kubwa kwa wauzaji wa hisa.
Upvote
0