JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Vyombo vya habari huru humaanisha kuwa hakuna mtu anayepaswa kudhibiti na kushawishi utangazaji wake wa habari.
Hakuna mtu anayepaswa kuviambia vyombo vya habari ni nini kinachoweza kuingizwa na nini hakipaswi kuingizwa katika habari wanazozitoa. Inamaanisha kuwa vyombo vya habari havifai kuwa chini ya shinikizo la mtu yeyote.
Iwapo vyombo vya habari vitakuwa huru vitaweza kufanya majukumu yake ipasavyo kama kuhamasisha uwazi na uwajibikaji kwa viongozi na kuleta maendeleo.
Na iwapo vyombo vya habari havitakuwa huru, vitakuwa vikisema sauti moja na hii na sauti ya wale wanaoviongoza na kuvidhibiti na kupelekea sauti za watu wa chini kutosikika na kusababisha uvunjifu wa demokrasia.
Upvote
0