Maana ya ujasiriamali

Maana ya ujasiriamali

blinky255

Member
Joined
Oct 2, 2015
Posts
28
Reaction score
7
Karibuni wadau.
Mjasiriamali ni nani?
Mjasiriamali ni mtu mbunifu, ambaye ununifu wake anaunadi na kutumia ili apate faida.
Mjasiriamali ni kitendo cha kuchukua hatua na kuanzisha kitu kipya au kufanya jambo ambalo linafanywa na wengine lakini katika njia ya tofauti.

Ikumbukwe kuwa: Kila mjasiriamali ni mfanyabiashara lakini Si kila Mfanyabishara ni mjasiriamali.
Sifa as Mjasiriamali.
•ni mtu ambaye yupo tayari kuthubutu.
•ni mtu mvumilivu.
•ni mtu jasiri asieogopa kufeli au kushindwa
•ni mtu ambaye kila siku anatafuta njia mpya as kuzalisha na kuleta maendeleo.
•ni mtu anaetumia changamoto kama fursa
•ni kiongozi
•ni mshindani asiyekata tamaa.
Sio lazima uwe na sifa zote zilizo orodheshwa hapo juu, hata sifa chache zinakufanya uwe mjasiriamali. Kitu cha kuzingatia ni kwamba baadhi ya sifa mtu huzaliwa nazo na zingine mtu hujifunza tu. Hivyo nawe unaweza jifunza ukawa mjasiriamali mkubwa na mwenyewe mafanikio.
 
Back
Top Bottom