Asante dear, maana nilifikiria hivyo pia. Tena basi kinachonifurahisha ni kuwa baada ya kumjibu yangu (kuwa asiwe na wasiwasi msg nimeiona na waeendelee tuu na mambo yao mimi sina noma yoyote...) acha mwan´dada anikurupukie na maneno, ooh, msg ilikuwa inaenda kwengine sio kwa mme wangu, mara sijui mme wangu sio type yake, yeye ni mtu high class, nikitaka kumjua vizuri niulize watu, mara angelikuwa anamtaka nisingekuwa nimekanyaga ulaya...too much rubbish. Nilichomwambia ni Thanks for the information tuu. Nikweli mme wangu anajigonga sana kwa huyu mama (maana ni mzee kweli tumepishana kama 15 years) ili nimuone mkali, siunaelewa tena. Anyway thanks for the advice.