Kuna mtaalam mmoja huko uingereza aliwahi kusema "Jambo jema likifika kwa wajinga, hugeuka dhahama"
Mfano wa Msemo huu tunaweza kuurejelea kwenye tamthilia ya "The god must be crazy" pale ambapo Chupa iliangushwa kutoka kwenye ndege na kuokotwa na 'Bush man'!
Kwa hali yao ya ujinga, ile chupa badala ya kuhifadhia dawa na maji yao, waliona inafaa kutumika kama nyundo! Waliponda vitu vyao kwa chupa, watoto wa bushman waliitumia chupa kupigiana vichwani!
Mjinga katika jambo jema mara nyingi huharibu maana!
Condom inayotakiwa kuvaliwa sehem za siri kwa mjinga yeye ataivaa kichwani lli masikio asisikie kelele!
MPANGO WA BIMA KWA WOTE ni jambo jema sana kwa wananchi lakini Wasimamizi wa kufanikisha zoezi hili watalifanya liwe kero!
IPO mipango inafanyika BIMA kwa Wote iwe ni LAZIMA!
Kwamba Mwananchi akienda kuomba maji lazima aambatanishe na kadi ya BIMA
Kwamba akitaka TIN namba lazima aambatanishe na kadi ya BIMA
Kwamba akitaka pembejeo wamuombe utambulisho wa BIMA
Kwamba akitaka hati ya kiwanja lazima aambatanishe na kadi ya BIMA
Sehemu pekee ambayo hawatahitaji BIMA ni siku ya kupiga kura ili warudi madarakani!
Hapo unaona wazi kwamba BIMA NI JAMBO JEMA! Lakini linapofika kwa Bushman wa uongozi analigeuza kero!
Kwa utaratibu huo hawaoni kwamba wataongeza rushwa maofisini
Kwa utaratibu huo hawaoni kwamba watawanyima haki za msingi wananchi
Kwa utaratibu huo hawaoni kabisa kwamba itakuwa ni adha kubwa sana kwa wengine!
Sababu kubwa ya kufanya hivyo ETI NI KUTAKA MAKUSANYO MENGI YA WANACHAMA WA BIMA ILI WAPATE KUWAHUDUMIA WACHACHE!
Hii hoja kwa mtu asiye waza sawasawa anaweza kudhani ina mashiko.
Kuna msemo unasema "Usiporidhika kwa kidogo hata ukipata kikubwa ni Yale Yale"
Kama ulikusanya michango kwa watu 10 ukashindwa kumhudumia vyema mtu 1, Je, Utawezaje kuwahudumia watu 10mil kutoka kwenye michango ya watu milion 100?
Jibu ni kwamba huwezi kwasababu hesabu huwa haidanganyi!
USHAURI WANGU
Kama serikali ina mpango wa kuanza kutekeleza bima kwa wote kwanini ISIANZE KUWAHUDUMIA VYEMA WENYE BIMA ili iwe kivutio cha Bima kwa wote?
Kwanini nchi yangu haipendi kutumia njia ya Huduma bora kama kivutio kwa wananchi?
Nashauri Bima kwa wote iwe huru mtu aweze kuingia na kutoka mwenyewe!
NASEMA HAYO KWASABABU
Inchi yetu haina historia ya kufanya vyema, hata ikianza jambo vizuri huwa halidumu!
Tuliona hayo kwenye NIDA, Tuliona hayo kwenye mradi wa mwendokasi, tuliona hayo kwenye Uviko 19, Tuliona hayo kwenye shule za kata, tuliona hayo kwenye miamala ya simu, tuliona hayo kwenye usimamizi Mali na fedha za umma! N.k
Mtakumbuka waziri mkuu alipokemea matumizi mabaya ya "Sheria ya posho makazini maalufu per DM
Ukiambiwa kiasi cha pesa za posho pa DM kwenye vikao vya kupitisha TOZO unaweza kuzimia!
Wanajadili UOZO wanalipana VINONO
Chonde chonde nashauri Bima kwa wote ISIWE LAZIMA KWA KUNYIMANA HUDUMA ZINGINE ZA KIJAMII
Lakini kwasababu watanzia waliowengi tunapenda kusubiri kulalamika, ngoja ipitishwe ndipo tuje kutoa maoni! Sahivi ni kama halituhusu!