SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Kuna mengi nimekuwa naelezea humu ndani kwa muda mrefu ila nadhani nilikuwa sieleweki ila nadhani sasa mtanielewa. Yanga haiwezi kumfunga Simba goli 5 katika mazingira yoyote ya kawaida na pamoja na mafanikio yoote ya Yanga, moja ya kitu ambacho walikuwa wanatamani kukifanikisha ili kweli wadhihirishe ubora wao kwa Simba ni kuitandika goli za kutosha. Hili jambo lilihitaji mkakati wa kutosha.
Maandalizi yaliyokuwa yanafanyika yalijumuisha kukidhoofisha kikosi cha Simba kwa kufanya usajili mbovu kwa misimu miwili. Usiniambie yule aliyewasajili mbilikimo zaidi ya 3 kwa mkupuo ndani ya dirisha moja la usajili alikuwa na nia njema na Simba. Halafu wakaletwa kina Sawadogo. Huku ndani ya kikosi una yule mchezaji ambaye aliletwa kwa mkakati maalumu, kila akigusa mpira 90% anaupoteza au anaanguka ila namba hakosi na kutolewa hatolewi, anachekacheka tu uwanjani. Halafu ikaja kumpiga pini Phiri baada ya majeraha ili timu ipate changamoto kupata ushindi lakini zaidi wachezaji wengine wacheze kwa tahadhari wakijua wakiumia tu, hawapati namba tena na hiyo ikashusha kabisa morali ya timu. Pia wakahakikisha wanaocheza kila siku ni wachezaji wale wale 13, mwanzo kisingizio kilikuwa walioko benchi hawana uwezo. Ukafanyika usajili mpya wachezaji zaidi ya 10, wakajazwa mawinga huku mahitaji ya ulinzi na kiungo hayakuzingatiwa, usajili wa kipa wote tuliona ulivyofanyika na katika wote waliosajiliwa wanaopewa nafasi kucheza ni 2 tu. Usiniambie aliyesimamia zoezi hili la usajili alikuwa na nia njema na Simba.
Kuhakikisha wachezaji wanapoteza kabisa fitness na utimamu wa kimwili, wakahakikisha kuna benchi dhaifu la kiufundi hasa kocha wa fitness ili siku ya kipigo wote tuseme kweli wachezaji hawana utimamu. Wachezaji hawafanyi mazoezi ya kueleweka, wanakimbia kimbia tu kama wanafunzi wa shule ya msingi na mizaha mingi mazoezini. Hii baada ya muda matokeo yake ndiyo haya tunayoyaona sasa.
Nilipokuwa nasema nakaa pembeni kwenye mambo ya mpira kulinda hisia zangu nilikuwa nayaona maandalizi haya yanakaribia kuzaa matunda. Kipigo cha goli 5 wala hakijanishtua wala kunishangaza.
Matatizo ya SImba hayataisha kirahisi kama mnavyodhani maana waliyoyaleta walidhamiria.