Maandalizi ya refinery ya mafuta yaanza Chongoleani, Tanga

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2012
Posts
23,234
Reaction score
28,473
TANGA , Kamati ya Pamoja ya Ufundi kati ya Tanzania na Uganda (Joint Technical Committee) imekabidhi eneo la Chongoleani, Tanga, kwa Mshauri Mwelekezi kutoka Worley Consulting Group Limited kwa ajili ya kuanza maandalizi ya ujenzi wa miundombinu ya kupokea, kuhifadhi na kusafirisha mafuta yaliyosafishwa.

Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano kati ya Tanzania na Uganda katika miradi ya kimkakati ya nishati.

Worley Consulting Group Limited inatarajiwa kuanza kazi za awali za upembuzi yakinifu, ikiwemo upimaji wa udongo, tathmini ya mazingira na usanifu wa awali wa miundombinu hiyo.

Mradi huo unatarajiwa kuongeza thamani katika mnyororo wa mafuta ghafi yatakayopita kupitia Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), huku ukichangia usalama wa upatikanaji wa bidhaa za petroli na kuongeza fursa za biashara katika Afrika Mashariki.

Kamishna Msaidizi wa Mkondo wa Kati na Chini wa Petroli kutoka Wizara ya Nishati, Grace Mwakasege, alisema mradi huo ni wa kimkakati na unatarajiwa kuifanya Tanga kuwa kitovu cha shughuli za mafuta na gesi katika ukanda huo.

Kamishna Msaidizi kutoka Wizara ya Nishati na Madini ya Uganda, Mhandisi Geofrey Ogwang, alisema ushirikiano huo utasaidia kuongeza ajira, uhamishaji wa teknolojia na shughuli za kiuchumi kwa wananchi wa Chongoleani na Tanga.
1000017342.jpg
 
TANGA , Kamati ya Pamoja ya Ufundi kati ya Tanzania na Uganda (Joint Technical Committee) imekabidhi eneo la Chongoleani, Tanga, kwa Mshauri Mwelekezi kutoka Worley Consulting Group Limited kwa ajili ya kuanza maandalizi ya ujenzi wa miundombinu ya kupokea, kuhifadhi na kusafirisha mafuta yaliyosafishwa.

Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano kati ya Tanzania na Uganda katika miradi ya kimkakati ya nishati.

Worley Consulting Group Limited inatarajiwa kuanza kazi za awali za upembuzi yakinifu, ikiwemo upimaji wa udongo, tathmini ya mazingira na usanifu wa awali wa miundombinu hiyo.

Mradi huo unatarajiwa kuongeza thamani katika mnyororo wa mafuta ghafi yatakayopita kupitia Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), huku ukichangia usalama wa upatikanaji wa bidhaa za petroli na kuongeza fursa za biashara katika Afrika Mashariki.

Kamishna Msaidizi wa Mkondo wa Kati na Chini wa Petroli kutoka Wizara ya Nishati, Grace Mwakasege, alisema mradi huo ni wa kimkakati na unatarajiwa kuifanya Tanga kuwa kitovu cha shughuli za mafuta na gesi katika ukanda huo.

Kamishna Msaidizi kutoka Wizara ya Nishati na Madini ya Uganda, Mhandisi Geofrey Ogwang, alisema ushirikiano huo utasaidia kuongeza ajira, uhamishaji wa teknolojia na shughuli za kiuchumi kwa wananchi wa Chongoleani na Tanga. View attachment 3682027
Wakati mwingine ni bora tukawa wakweli kwa nafsi zetu. Kibiashara hatuwezi kuwa na refinary kubwa mbili moja Lamu na Nyingine Tanga.

Tukubali kama nchi tulishindwa kuichangamkia fursa ya uwekezaji wa Dangote, mwisho akaenda Kenya.

Tusisahau Kenya ni ndugu zetu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hivyo ni vyema tukafikiria miradi gani mingine complimentary yakufanya badala ya kuanzisha ligi zisizo na mbele wala nyuma.

Kwa hapa tulipofika tunahitaji zaidi uangalifu na busara. Maamuzi ya hasira hayatatusaidia
 
Tusisahau Kenya ni ndugu zetu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hivyo ni vyema tukafikiria miradi gani mongine complimentary yakufanya badala ya kuanzisha ligi zisizo na mbele wala nyuma.

Chawa watakuja na matheories yao kubrag ukweli huu mchungu! Wanajua refinery ni km kiosk cha matunda!
 
there is a thin line bwetween “mradi wa mafuta” na “mradi wa kiwanda cha kusafishia mafuta (refinery)”

cc JamiiCheck
 
Sisi tunajua Worley ndio main contractor wa EACOP hizi za Samia na Mu7 ni za kwenu, mradi ni wa TOTAL Energies na serikali ya Uchina sisi ni wawezeshaji tu..
 
Wakati mwingine ni bora tukawa wakweli kwa nafsi zetu. Kibiashara hatuwezi kuwa na refinary kubwa mbili moja Lamu na Nyingine Tanga.

Tukubali kama nchi tulishindwa kuichangamkia fursa ya uwekezaji wa Dangote, mwisho akaenda Kenya.

Tusisahau Kenya ni ndugu zetu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hivyo ni vyema tukafikiria miradi gani mongine complimentary yakufanya badala ya kuanzisha ligi zisizo na mbele wala nyuma.

Kwa hapa tulipofika tunahitaji zaidi uangalifu na busara. Maamuzi ya hasira hayatatusaidia
Ivi Kenye Crude oil ataitoa uganda huko huko au inakuaje kama na sisi tukiwa na iyo refinery ya "mashemeji"
 
Wakati mwingine ni bora tukawa wakweli kwa nafsi zetu. Kibiashara hatuwezi kuwa na refinary kubwa mbili moja Lamu na Nyingine Tanga.

Tukubali kama nchi tulishindwa kuichangamkia fursa ya uwekezaji wa Dangote, mwisho akaenda Kenya.

Tusisahau Kenya ni ndugu zetu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hivyo ni vyema tukafikiria miradi gani mongine complimentary yakufanya badala ya kuanzisha ligi zisizo na mbele wala nyuma.

Kwa hapa tulipofika tunahitaji zaidi uangalifu na busara. Maamuzi ya hasira hayatatusaidia
Kuna shida gani zikiwepo 2
 
Wakati mwingine ni bora tukawa wakweli kwa nafsi zetu. Kibiashara hatuwezi kuwa na refinary kubwa mbili moja Lamu na Nyingine Tanga.

Tukubali kama nchi tulishindwa kuichangamkia fursa ya uwekezaji wa Dangote, mwisho akaenda Kenya.

Tusisahau Kenya ni ndugu zetu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hivyo ni vyema tukafikiria miradi gani mingine complimentary yakufanya badala ya kuanzisha ligi zisizo na mbele wala nyuma.

Kwa hapa tulipofika tunahitaji zaidi uangalifu na busara. Maamuzi ya hasira hayatatusaidia
Hii sio hoja, uhitaji wa mafuta bado ni mkubwa hata zingekuwa katika kila mkoa wenye bahari. Mfano uwepo wa bandari ya mombasa haufanyi bandari ya Dar isifanye biashara
 
Back
Top Bottom