Halisi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2007
- 2,802
- 614
Naweza kuwa bubu(kutochukua upande) katika maudhui ya maandamano, lakini jambo kubwa na la msingi, ni kwamba ghafla Watanzania tumesahau ya Mwembechai, Zanzibar na kadhalika, kwa kitendo cha polisi kuzuia watu wasiandamane. Hilo ni kosa kubwa sawa na lile la MP's wa CCM wakiongozwa na EL na chambo wao Mudhihir kumfungia Zitto. Polisi wangeruhusu lakini wakahakikisha ulinzi ni mkali. Wangeweza hata kuwazuia wasiende ubalozi wa Kenya na badala yake waishie Jangwani ama popote na wawakilishi wao wapeleke huo waraka kwa ubalozi wa Kenya, lakini kitendo cha kuzuia watu kufanya wanachoamini ni kukiuka HAKI ya Msingi ya KIKATIBA.
Lakini pia maandamano ni kupeleka salaam kwa Wakenya kwamba yanayowakuta tunayaona na ni fundisho kwetu.
Kuhusu kuwa na upande nadhani kwa wapinzani wana haki kabisa kuwa na upande. Kwa serikali si sahihi kuwa na upande kwa sasa japo inawezekana kwa siri wako na Kibaki ama mwenzake Raila (japo ni ndoto).
Suala la utata wa kura, Watanzania hatuwezi kukwepa jumuia ya kimataifa inayoona kuna tatizo na hata Watanzania ukiwamo ubalozi unafahamu hilo.