Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
Kwa umri wangu huu babu yenu nimeshaona maandamano mengi ya kupinga, ya kudai na yakuunga mkono jambo Fulani lakini sijawahi kusikia maandamano ya kudai pombe
ILA ninachoweza kusema ni kuwa umuhimu wa kitu anaujua mtumiaji na hali hiyo ilipelekewa watumiaji wa pombe nchini Marekani kuaandaa maandamano ya kudai pombe
"TUNATAKA POMBEEE"
TUNATAKA TULEWEEEE
TUNATAKA BIAAAA"
Huenda hizo ndio zilikuwa sauti zao walizozitoa kipindi cha maandamano hayo
Kutokana na kukithiri Kwa maovu katika jamii ya wamarekani, baadhi ya viongozi wa dini na umoja wa kina mama walio kwenye harakati waliishauri serikali iliyopo madarakani wafungie pombe (PROHIBITION)
Wao waliamini ulevi umechangia kwa kiasi kikubwa sana kuongeza Rushwa katika jamii, kuongeza uhalifu, wanaume kutelekeza familia zao, na watu kutoheshimu sheria
Mawazo hayo yaliingia moja kwa moja kwenye kichwa cha aliyekuwa Rais wa Marekani kwa wakati huo (1920) Bwana Woodrow Wilson na kusaini muswada wa kuzuia utumiaji wa pombe, usafirishaji wa pombe na uzalishaji WA pombe kuanzia mwaka 1920 na sheria hiyo ilidumu kwa zaidi ya miaka 10...japo sio pombe zote zilifungiwa kuna baadhi ya wine hazikufungiwa kwa sabab ya shughul za kidini na pombe kwa ajil ya tiba
Malengo ya kufungia pombe yalikuwa mazuri lakin kwa bahati mbaya njia walizotumia zilikuwa mbaya zaidi kwa sababu hawakupata kile walichotarajia. Yaani baada ya kufungia walitarajia rushwa ipungue, uhalifu upungue, watu wajielekeze kwenye kufanya mambo ya msingi zaidi
lakini hali haikuwa hivyo mambo yakawa mabaya zaidi uhalifu ukaongezeka, watu wakatafute vilevi vyengine kama cocaine, opium na bangi na watu wakakosa ajira kutokana na viwanda kufungwa, rushwa ikaongezeka maradufu, biashara ya pombe za kienyeji ikashamiri zaidi, maelfu ya watu kufariki, makundi ya kihalifu yakaongezeka zaid kwa sabab wao ndio wakawa wameishikilia biashara hiyo ya pombe na baya Zaidi maandamano ya watu kudai pombe yakazuka
Kupiga tu marufuku ya pombe kulisababishia serikal ipoteze zaidi ya dola za kimarekani bilion 11 huku wakitumia zaid ya dola za kimarekan million 300 kwa ajili ya kuitekeleza sheria hiyo
Tar 5/12/1933 Raisi wa Marekan Bwana Franklin D. Roosevelt aliruhusu pombe
Je, kwa mfano pombe ingezuiliwa hapa Tanzania, ni rafiki yako yupi usingemkosa kwenye maandamano ya kudai pombe?