Maandamanao ya wanafunzi wa elimu ya tarehe 15/08/2014- Nchi nzima

Maandamanao ya wanafunzi wa elimu ya tarehe 15/08/2014- Nchi nzima

Joined
Jan 29, 2014
Posts
35
Reaction score
37
Ikiwa ni wiki ya nane tangu mafunzo kwa vitendo(fieldwork) kuanza wanafunzi wa Elimu ya juu hawajapata fedha zao za kujikimu,hivo SIKU YA IJUMAA,TAREHE 15/08/2014 yatafanyika maandamano ya Amani Nchi Nzima kushinikiza kulipwa fedha hizi.

Maandamano ya Dar es Salaam yataelekea Ofisi ya Waziri Mkuu Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania (Mtoto wa mkulima,Mizengo pinda),Maandamano ya Mikoani yataelekea Ofisi za Wakuu wa Mikoa.Wito kwa wanafunzi wote wa Elimu ya juu,wadau wa Elimu,wanaharakati wa haki za Binadamu na Watanzania wa kawaida kuunga mkono maandamano haya


Wanafunzi vyuo vikuu kumvaa Pinda kesho

Alhamisi, August 14 2014
UMOJA wa Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu (TAHLISO) umetangaza kufanya maandamano ya amani kesho hadi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuishinikiza Serikali kulipa fedha zao kwa ajili ya Mafunzo kwa Vitendo.
Wanafunzi hao wametangaza uamuzi huo ikiwa ni wiki ya nane sasa tangu walipotakiwa kuripoti katika maeneo ya mafunzo ya vitendo, lakini kutokana na kukosa fedha wameshindwa kufanya hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Rais wa TAHLISO, Musa Mdede, alisema awali waliipa siku saba Serikali ili iwe imewalipa fedha wanafunzi lakini hadi sasa ni wiki ya nane hakuna fedha zilizopelekwa vyuoni.

Alisema mafunzo kwa vitendo ni muhimu kwani hiyo ni sehemu ya masomo yao na ikiwa hilo halitafanyika basi ni lazima mwanafunzi atarudia mwaka kutokana na kukosekana kwa alama ambazo lazima ziwepo ili kukamilisha masomo yake.

"Tumefuatilia sana hadi sasa, lakini hakuna kitu chochote kilichofanyika wanafunzi kutoka vyuo saba havijapewa fedha hizo, kitu ambacho kinaweza kufanya wanafunzi wengi kurudia mwaka," alisema na kuongeza;

"Baada ya kufuatilia kwa muda mrefu na kutoa siku saba ili Serikali ilipe fedha hizo ambazo ni sh. bilioni 1 hakuna kilichofanyika."

Mdede alisema kutokana na hali hiyo wanafunzi kwa sasa wameanza kuwa na wasiwasi kama watapewa fedha zao za kujikimu za mwezi Oktoba.

Alibainisha kuwa vyuo ambavyo hadi sasa havijapata fedha hizo ni Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM),Theophilo Kisanji cha jijini Mbeya,Chuo cha Mt. Augustino cha Mwanza,Tumaini Makumira cha Arusha,Chuo cha Mt. Augustine Tawi la Tabora,Chuo cha Kumbukumbu ya Stephano cha mkoani Kilimanjaro,Chuo cha Jordan cha mkoani Morogoro na Chuo cha Bugando cha mkoani Mwanza.

Akizungumzia hali hiyo, Waziri wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Waziri Juma, alisema wamefuatilia kwa kipindi kirefu lakini uongozi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HEALSB) ulisema hauna fedha.

"Tulikwenda Bodi ya Mikopo kupeleka kilio chetu na bahati nzuri tulikutana na Mkurugenzi wa Bodi hiyo na tulimwambia suala hilo, lakini alisema kama yeye angekuwa na fedha basi angewapa... lakini hakuna fedha; na Hazina haijapeleka fedha kwenye Bodi; hivyo fanyeni mnachoweza kufanya," alisema akimnukuu Mkurugenzi wa HESLB.


CHANZO:
Majira
 

Attachments

  • 1407986653000.jpg
    1407986653000.jpg
    78.7 KB · Views: 803
Vitisho tu...kila siku mnatishia kugoma hatuoni mkifanya hvyo,kizazi cha watoto wa chuo leo sikielewi,wote wamekuwa waseminari.How do you survive and torelate 8weeks bila kupewa chenu?I remember those years baana,hizo ofisi zao zisingekalika..... the then COET
 
Mie nimezisubiri hela hizo nimechoka nina harakati za kurudi nyumbani...hapo zimechelewa za field sasa tusubiri za kujikimu chuoni. Vyuo vikifunguliwa lazima tuone moto
 
Vipaza sauti ni bora kuliko nyie someni harama za nyakati,nimesikia gazeti la majira kwamba wanafunzi kumvaa pinda kesho.
 
Maandamano yalikuwa enzi hizo sasa hivi vijana wetu hamna umoja kabisa. Maisha yakiendelea hivi nchi imekosa wa kuiongoza. Mkipewa kanga, t-shirt na kofia mna lala usingizi kabisa.
 
Unganisheni mambo mengi kama ufisadi, ajira, ugumu wa maisha, mfumuko wa bei nk hapo tutakuwa pamoja na nyie. Msisahau kufunga matawi ya CCM vyuoni
 
Vitisho tu...kila siku mnatishia kugoma hatuoni mkifanya hvyo,kizazi cha watoto wa chuo leo sikielewi,wote wamekuwa waseminari.How do you survive and torelate 8weeks bila kupewa chenu?

So, unawataka wawe na akili kama za UKAWA? Ninyi mliozaliwa nje ya ndoa mna matatizo kila kitu kugoma, kulalamika na ubishi wa kishetani tu. Kuweni kama CCM
 
Kama wapo field, wataandamana kutokea wapi? Na nani mratibu wa hayo maandamano?
 
Ukisikia maandamano tu basi ujue CHADEMA ipo ndani
 
Unganisheni mambo mengi kama ufisadi, ajira, ugumu wa maisha, mfumuko wa bei nk hapo tutakuwa pamoja na nyie. Msisahau kufunga matawi ya ccm vyuoni
Kwa kawaida maandamano yanakuwa na dhima moja tu
 
Na je vipi kuhusu kibali kutoka jeshi la polisi?
 
Ila mkumbuke kuwa IGP wa sasa si shemeji yenu SAID MWEMA. Huyu ni Ernest Mangu.
 
Na wanaharakati tena? Nilitaka niwaunge mkono, sasa nimeghahiri. Haya maandamano ya kisiasa
 
Ila mkumbuke kuwa IGP wa sasa si shemeji yenu SAID MWEMA. Huyu ni Ernest Mangu.
Hawa wanafunzi wameanza kutumiwa vibaya na wanasiasa, usije ukashangaa mabango yameandikwa katiba mpya
 
Vitisho tu...kila siku mnatishia kugoma hatuoni mkifanya hvyo,kizazi cha watoto wa chuo leo sikielewi,wote wamekuwa waseminari.How do you survive and torelate 8weeks bila kupewa chenu?I remember those years baana,hizo ofisi zao zisingekalika..... the then COET
They know, they have been used by politicians
 
Back
Top Bottom