onjwayo
JF-Expert Member
- Apr 8, 2020
- 1,356
- 1,309
Kwa wiki ya pili Sasa Jamhuri ya Kenya na nchi jirani yetu wamekuwa kwenye mvutano kati ya serikali na wananchi. Nasema ni wananchi vs the government kwa sababu tumeshuhudia polisi dhidi ya raia wakikimbizana barabarani.
Kwanza kwa vipindi vyote 2, Jumatatu iliyopita na ya Jana trh 27/3/2023 naweza nikasema kuwa wananchi wamefaulu kwa hatua kubwa. Mosi ni azma Yao ya kuandamana imetimia na pili nguvu Yao imeonekana kubwa kudhibiti nguvu ya polisi na tatu ushujaa wao kutokujali nguvu kubwa ya polisi kutumia MABOMU ya kutoa MACHOZI na maji ya washawasha.
Ujumbe nilioubeba hapa ni kufanya masihara na kutokujishusha kunaweza kuleta maafa.
Serikali lazima ikae chini na viongozi wa waandamanaji na kuongea. Kutumia jeshi na makundi ya waalifu kwenda kuiba na kuvunja Mali za vinara wa waandaji maandamano kunazidi kuuchochea moto ulianza kuwaka kwa kuukoleza kwa petroli. Rais Ruto anaweza kuutuliza kwa sababu ni yeye ndiye amiri jeshi mkuu.
Majeshi haya yanayopambana na raia yeye ndiye wa mwisho kuzikomandi na Hawa raia yeye pia ndiye rais wao. Kwahiyo kukaa kimya bila kukemea ni sawa na baba mwenye mji anayewaacha watoto wapigane na mama Yao na asiwaamue lakini pindi watakapoumizana ndipo atachukua hatua.
Narudia kusema masihara kwenye jambo hili lisiruhusiwe.....Ruto aketi na Raila waongee japo tension ni kubwa ila Bora nusu Shari kuliko Shari kamili