Maandamano Kenya: Tutegemee masihara kuleta maafa

Maandamano Kenya: Tutegemee masihara kuleta maafa

onjwayo

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2020
Posts
1,356
Reaction score
1,309
Kwa wiki ya pili Sasa Jamhuri ya Kenya na nchi jirani yetu wamekuwa kwenye mvutano kati ya serikali na wananchi. Nasema ni wananchi vs the government kwa sababu tumeshuhudia polisi dhidi ya raia wakikimbizana barabarani.

Kwanza kwa vipindi vyote 2, Jumatatu iliyopita na ya Jana trh 27/3/2023 naweza nikasema kuwa wananchi wamefaulu kwa hatua kubwa. Mosi ni azma Yao ya kuandamana imetimia na pili nguvu Yao imeonekana kubwa kudhibiti nguvu ya polisi na tatu ushujaa wao kutokujali nguvu kubwa ya polisi kutumia MABOMU ya kutoa MACHOZI na maji ya washawasha.

Ujumbe nilioubeba hapa ni kufanya masihara na kutokujishusha kunaweza kuleta maafa.

Serikali lazima ikae chini na viongozi wa waandamanaji na kuongea. Kutumia jeshi na makundi ya waalifu kwenda kuiba na kuvunja Mali za vinara wa waandaji maandamano kunazidi kuuchochea moto ulianza kuwaka kwa kuukoleza kwa petroli. Rais Ruto anaweza kuutuliza kwa sababu ni yeye ndiye amiri jeshi mkuu.

Majeshi haya yanayopambana na raia yeye ndiye wa mwisho kuzikomandi na Hawa raia yeye pia ndiye rais wao. Kwahiyo kukaa kimya bila kukemea ni sawa na baba mwenye mji anayewaacha watoto wapigane na mama Yao na asiwaamue lakini pindi watakapoumizana ndipo atachukua hatua.

Narudia kusema masihara kwenye jambo hili lisiruhusiwe.....Ruto aketi na Raila waongee japo tension ni kubwa ila Bora nusu Shari kuliko Shari kamili
 
Ruto aketi na Raila waongee japo tension ni kubwa ila Bora nusu Shari kuliko Shari kamili
Ruto piga hao wanaona nchi ni mali ya kabila lao usilegeze, mwaga moto watakuelewa, weka ulokole pembeni kidooogo. Waoneshe kuwa wewe.....ler
 
Ni kweli kabisaa.

Waswahili wanamsemo;
"Mchelea mwana hulia mwenyewe"

Anacho endelea kukifanya Raila na kundi lake kitaitumbukiza Kenya kwenye machafuko.

Tumeshuhudia kwenye maandamano ya jana wandamanaji wakivamia shamba la Rais mstaafu Uhuru Kenyatta na kuiba mifugo na kuharibu miti kwa kukata na kuchoma.
 
Rigathi Gachetha, Makamu wa Rais wa Kenya, bila kumfunga speed governor, namuona anaiangusha serikali ya Ruto.

Ni kama mtu anayewashwa na pilipili au anatembelewa na siafu.

Raila anakuwa na nguvu sana pale unapomuwekea vikwazo, taking into account ushindi wao ni tofauti ya kura laki mbili, nusu ya nchi anayo Raila, nusu anayo Ruto, Ruto ameanza mapema mivutano, kwanza alitakiwa awe na uungwaji mkono mkubwa kabla ya kuanza fitna za kisiasa.
 
Rigathi Gachetha, Makamu wa Rais wa Kenya, bila kumfunga speed governor, namuona anaiangusha serikali ya Ruto.

Ni kama mtu anayewashwa na pilipili au anatembelewa na siafu.

Raila anakuwa na nguvu sana pale unapomuwekea vikwazo, taking into account ushindi wao ni tofauti ya kura laki mbili, nusu ya nchi anayo Raila, nusu anayo Ruto, Ruto ameanza mapema mivutano, kwanza alitakiwa awe na uungwaji mkono mkubwa kabla ya kuanza fitna za kisiasa.
Anacho kifanya Raila ni uchokozi kwa Serikali ya Ruto, ila Rais na Makamu wameonyesha busara kubwa sana tatizo lipo kwa Babu hataki kukubali kama alishindwa uchaguzi, qlienda mahakamani napo akabagwa bado hakubali.

Babu ni mtata sana, lakini safari hii chini ya Rais Ruto na Makamu wake asitegemee hand shake Wala nusu mkate, asubiri uchaguzi Mkuu 2027 panapo uhai.

Huwezi kuiondoa Serikali iliyo chaguliwa kidemokrasia madarakani Hadi uchaguzi Mkuu. Maandamano yanayo fanywa na Raila na kundi lake kuishiniliza Serikali iondoke ni uhaini nadhani wanamvumilia tu lakini ni vyema akae kimya.
 
Babu ni mtata sana, lakini safari hii chini ya Rais Ruto na Makamu wake asitegemee hand shake Wala nusu mkate, asubiri uchaguzi Mkuu 2027 panapo uhai.
Raila mbinafsi sana. Hakuna uchaguzi alioshindwa ambao haujafuatiwa na vurugu anazoanzisha.

Bahati mbaya sana analo kundi kubwa la wafuasi, wengi wakiwa wa kabila lake, ambao ni watiifu bila kuhoji kwa lolote atakalowaelekeza kufanya.

2027 kwake ni mbali sana. Asipodhibitiwa ataliangamiza taifa.
 
Na huku Je?



Hii France Ina Waafrika wengi ndio maana Huwa haiishi maandamano ya kipumbavu ya mara Kwa mara tena yenye ghasia.

Watu Weusi hawanaga ustaarabu bila chuma Huwa hawaelewi
 
Huyo Raila amolo odinga ndie anatakiwa kushughurikiwa,huyo mzee alishazoea vya mkato,na hata mda huu anatafuta aingizwe serikalini kwa mlango ws nyuma,
 
Back
Top Bottom