Kwa uzoefu wangu Watanzania hatukawii kusahau na kuchukulia jambo kuwa NI KAZI YA MUNGU. baada wa SUMATRA kupandisha nauli najua keshokutwa sisi tunaotumia usafiri wa daladala wengi wetu hiyo siku ya kwanza na yapili huenda na ya tatu , tutajifanya kususia usafiri huo na kuunga mkono azimio la Arusha tukijifanya kuonyesha hasira juu ya jambo hilo. lakini baada ya siku nne hivi KIMYAAAAAAA NA WOTE TUNAGOMBANIA USAFIRI TENA PENGINE KUPITIA DIRISHANI.
Bila shaka utakuwa unamaani "yako wapi maisha bora kwa kila mtz? "kwa ufupi tz ni sawa na watu waliyomo ndani ya ukumbi wa disco, kila unapopigwa muziki mkali na DJ ,wachezaji husahau na kufuta wimbo wa zamani.mean's mpaka disco linaisha wachezaji huwa wapo hoi na faida ya kuwa hoi haipo!!