Maandamano kupinga mauaji na watu wasiyojulikana yanatakiwa kuwa ya wananchi wote bila kujali dini wala chama cha siasa

Maandamano kupinga mauaji na watu wasiyojulikana yanatakiwa kuwa ya wananchi wote bila kujali dini wala chama cha siasa

Gabeji

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2024
Posts
1,530
Reaction score
1,903
Ndugu watanzania, inchi yetu inapitia kipindi kigumu sana hasa juu la swala la mauwaji hayakubaliki kabisa iwe kwa sbb yoyote ile, mfalme yoyote yule hana mamlaka ya kukatisha uhai wa mtu yoyote yule.

Rai yangu watanzania swala la kudai haki kwa njia ya amani ni la kikatiba, mandamano yanatakiwa yawe ya wananchi wote bila kujali itikadi, dini, rangi, elimu, kabila, ukanda nk, hivyo elimu ya kujitambua ni Muhimu sana, elimu ya kuondoa ubinafsi, uchawa, unafiki, uchama, udini, ukanda inatakiwa itolewe kabisa kwa watanzania wote kuanzia ngazi ya familia.

Pia soma: Kuelekea 2025 - Yaliyojiri kwenye Maandamano ya CHADEMA 23/9/2024

Badala yake itolewe elimu ya uzalendo na upendo juu ya taifa letu la Tanzania. Mchawi mkubwa wa taifa letu hili sio CCM, sio, katiba, sio dini la katoriki, sio wazee waliopo ndani ya CCM, bali ni utamaduni wetu mbovu wa kuwa na" unafiki" kuto sema kweli, wapo wana CCM wengi hawakubaliani kabisa na mauwaji lakini hamna hata mmoja alie kemea.

Kuna gap kubwa sana la kiuchumi Kati ya viongozi wetu na wananchi idara zote, iwe siasa, dini, nk. unafiki unazaa ubinafsi na ubinafsi unazaa umasikini.

Mungu bariki Tanzania yetu.

Samahani sio mwandishi mzuri.
 
downloadfile.png
 
Back
Top Bottom