Maandamano makubwa ya kupinga ubaguzi wa rangi yametokea Belfast, Northern Ireland, UK

Maandamano makubwa ya kupinga ubaguzi wa rangi yametokea Belfast, Northern Ireland, UK

Traxtion

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2021
Posts
8,000
Reaction score
16,414
Picha nzima ya kinachoendelea kwa ufupi ni kwamba
Kuna raia kutoka Sudan alimjeruhi vibaya sana raia mmoja mzungu wa Belfast kwa kumchoma choma visu vya uso, na kuharibu jicho la kushoto la mzungu huyo, huku jicho la kulia bado zima lakini limejeruhiwa vibaya. Baada ya kumchoma visu mzungu huyu, akaanza kumchinja shingoni yani akate kichwa chake mazima, ndipo wasamaria wema wakaebda kumwokoa mtu huyo kabla hajakatwa kichwa
Video yenyewe hii hapa

.
Jambo hili liliwapa hasira kali wananchi wa Belfast kwa hiyo wakaandamana wakiwa wamevaa mask kama majambazi, kisha wakavamia makazi ya immigrants na kuanza kuchoma magari yao, kuwafukuza ndani ya nyumba, kuchoma moto vitu vyao na wakimuona immigrant yoyote especially mweusi walikuwa wanamkamata na kumpiga vibaya, all kwa sababu ya kosa la mtu mmoja.

Ikumbukwe watu wa Ulaya wengi wao walikuwa wanapondea Marekani kwenye maandamano ya Black Lives Matter kuwa walikuwa wanachoma vitu vya watu kwa kosa la mtu mmoja. Sasa leo hii na wao Belfast wakafanya the very same thing. Kosa la Msudani mmoja wakaenda kuvamia makazi ya innocent immigrants ambao wanajitafutia tu maisha kwenye nchi za Ulaya.

Baada ya maandamano hayo ya Belfast kutokea, yamezuka maandamano mapya ambayo ni makubwa zaidi yakipinga kilichofanywa na watu wa Belfast kwenda kuchoma nyumba za immigrants na kupiga watu weusi na wa brown.

Kwa mtazamo wangu, Ulaya haipaswi kuzuia immigrants kuingia kwenye nchi zao lakini wanapaswa kuwa very selective. Tatizo lao wao wanaingiza tu immigrants mamilioni ili kuwaokoa kutoka kwenye vita. Sheria zao za immigration zinapaswa kuwa sawa wahakikishe wanaingiza watu wengi ambao ni skilled, no criminal records, ni watu ambao wanaweza ku assimilate kwenye Western culture na sio kusomba tu mamilioni ya wakimbizi na kuwabwaga nchini kwako. La sivyo matatizo kama haya yatazidi kuwakumba.
Wakimbizi kutoka Somalia au Sudan sio lazima wapelekwe Ulaya. Wanaweza kupelekwa kwenye miji mikubwa kama Khartoum au Mogadishu nk ambako huwa hakuna vita. Sio nchi nzima huwa zina vita. Kuna maeneo salama nchini kwao ambako wanaweza kupelekwa
 
nini kilitokea mkuu mpaka mwafrika mwenzetu akamjeruhi mzungu?
 
Back
Top Bottom