FRANC THE GREAT
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 5,500
- 8,060
Mgomo wa kitaifa umeathiri shule na usafiri wa umma nchini Ufaransa
Shughuli za usafiri zimesitishwa, shule zimefungwa, na katika mnara wa Eifel, hakuna watu baada ya vyama vya wafanyakazi kuitisha migomo kupinga mipango ya serikali ya kuufanyia marekebisho mfumo wa pensheni.
Jiji la Paris limetuma askari polisi 6000 kwa kile kinachotajwa kuwa maandamano makubwa kabisa kuwahi kushuhudiwa katika mji mkuu huo wa Ufaransa, mikusanyiko ya watu waliomkasirikia rais Emmanuel Macron na mpango wake wa mageuzi ya mfumo wa pensheni wanayosema utahatarisha mtindo wao wa maisha walioupigania.
Mnara wa Eifel na makumbusho ya Louvre, wamewaonya watalii dhidi ya vurugu zitakazosababishwa na mgomo huo na hoteli za mjini Paris zinatapa tapa kupata wageni.
Wageni wengi ikiwa ni pamoja na waziri wa nishati wa Marekani, wamefutilia mbali mipango ya kuitembelea nchi hiyo ambayo ni mojawapo ya nchi zinazotembelewa na watu wengi zaidi ulimwenguni.
Vituo vya safari za reli ya chini kwa chini katika jiji la Paris, vimefungwa na kuzidisha vurugu katika shughuli za usafiri ambazo tokea hapo ni za vurugu.
Wafanyakazi wengi wa Paris na vitongoji vyake, wanafanyakazi majumbani wameamua kutokwenda kazini ili kusalia na watoto wao majumbani kwakuwa asilimia 78 ya waalimu wa jiji hilo wamejiunga na mgomo huo.
Vituo vya kihistoria vya treni vitupu na treni moja kati ya kumi za mwendo wa kasi ndio inayofanyakazi. Safari nyingi za ndege katika uwanja wa ndege wa Charles de Gaule zimefutwa kwakuwa shirika la ndege la Air France limefuta takribani asilimia 30 ya safari za ndani.
Wakijiandaa kukabiliana na uwezekano wa kutokea machafuko na uharibifu katika mitaa ya mji mkuu Paris, Polisi wamewatolea wito wafanyabiashara wafunge mikahawa na vituo vingine vya kibiashara.
Maafisa wa serikali wametangaza marufuku ya watu kuandamana katika mtaa mashuhuri wa Champs Elysée, karibu na kasri la rais, bunge na karibu na kanisa kuu la Notre Dame.
Wanaharakati wa vizibao vya manjano wamejiunga na vyama vya wafanyakazi kuandamana mjini Paris na katika miji mingine kote nchini humo wakipania kushinikiza madai yao kuhusu haki sawa za kiuchumi.
Sources: DW | BBC | The Guardian