SI KWELI PreGE2025 Maandamano Mtwara leo ya wanachama wa ACT wakimkataa Mpina

SI KWELI PreGE2025 Maandamano Mtwara leo ya wanachama wa ACT wakimkataa Mpina

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Kuna hii video inaonekana kama si halisi, naomba uhalisia wake.

Na je, ni kweli kulikuwa na maandamano huko Mtwara leo Agosti




1764661509532.png
 
Tunachokijua
Baada ya barua kusambaa Mtandaoni ikionesha Katibu wa Itikadi na Uenezi wa ACT Wazalendo Dar es Salaam, Monalisa Ndala akieleza kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa amesema uteuzi wa Luhaga Mpina kuwa Mgombea Urais kupitia Chama hicho ni batili Kisheria, Ofisi ya Msajili ilithibitisha kuwa taarifa hiyo ni ya kweli.

Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza alipoulizwa amesema “Ni kweli tumeandika barua kwenda ACT kuwajulisha suala hilo (Mpina kutokuwa na vigezo) na Monalisa amepewa nakala.”

Aidha ACT Wazalendo ilithibitisha kupokea taarifa ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuwa Luhaga Mpina hawezi kuwania Urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2025 kupitia chama hicho kwa maelezo kuwa ni batili Kisheria, hivyo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa ACT inapitia kabla ya kutoa uamuzi wakati huohuo, ACT ikisema haitafuata maelekezo ya Msajili.

Madai

Kumekuwepo na Video inayosambazwa mtandaoni ikiwaonesha watu waliovalia nguo za zambarau wakisikika wakisema 'Mpina Sio Chaguo letu' huku ikiambatanishwa na kichwa cha habari kinachodai kuwa ni Maandamano ya ACT Wazalendo mkoani Mtwara.

Je, ni upi uhalisia wa video hiyo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia nyenzo za kidigitali umebaini kuwa video hiyo imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Akili Unde

Aidha video hiyo imebainika kuwa na mapungufu kadhaa yanayodhihirisha kuwa imetengenezwa kwa Akili Unde, mathalani makosa ya kiuandishi katika moja ya mabango na fulana zilizovaliwa na watu, uwepo gari ambalo halina namba ya gari 'plate number' iliyosajiliwa Tanzania.

Aidha hakuna taarifa rasmi iliyoripotiwa juu ya uwepo wa maandamano ya wanachama wa ACT Wazalendo mkoani Mtwara kupinga Luhaga Mpina kugombea urais kupitia chama hicho.
1756296383112-png.3454955

Attachments

  • ACT27AUG2025.mp4
    4.2 MB
Back
Top Bottom