Mimi nakataa Kikwete siyo chaguo la Watanzania
1. Sikumpigia kura yangu. Ndugu zangu wa karibu na marafiki zangu wengi hawakuwa wakimtaka na walikiri kutompigia kura
2. Kachaguliwa na Watanzania 5,276,827 (Zikiwepo na kura za maluani - uchakachuaji) kati ya Watanzania zaidi ya Milioni 40
3 Wananchi waliojiandikisha zaidi ya 11,511,020 ambao ni asilimia 57.16% hawakupiga kupiga kura kutokana na either kuhofia kura zao kuchakachuliwa au mfumo mbovu uliowekwa ili kupunguza kura za wapinzani mfano, kuzuia raia kupiga kura ya raisi sehemu yoyote ya nchi wakati anachaguliwa raisi wa nchi nzima au kufunga vyuo vya elimu ya juu na mashule.
4. Kachaguliwa na wananchi wengi walio vijijini kutokana na uelewa mdogo.
5. Amesaidiwa sana na vyombo vya ulinzi na usalama na taasisi za serikali vikiwemo vyombo vya habari vya serikali kufanikisha matakwa yake na familia yake
6. Katumia gharama kubwa sana katika kampeni (Mabango kutoka Canada, magari ya kifahari nk. wakati Watanzania wanaishi maisha ya dhiki kubwa
7. Ahadi zake ni nyingi na amezitoa nje ya Ilani kama alivyothibitisha meneja wa kampeni zake na yeye mwenyewe alisema nyingine zilikuwa za papo hapo.
8. Miaka mingine mitano ya Wadanganyika kudharaulika na kunyanyaswa na mafisadi wakati president akijikomba kwa wale Nyerere aliosema - nanukuu "Mijitu hii lengo wao ni kututawala, kwa nini tunawaongezea uwezo wa kututawala?'' mwisho wa kunukuu
Waliopiga kura 8,626,283 = 42.84%
Kura zilizoharibika = 2.64%
Mgawanyo wa kura ni hivi:
APPT: 96,933 = 1.12%
CCM: 5,276,827 = 61.17%
CHADEMA: 2,271,941 = 26.34%
CUF: 695,667 = 8.06%
NCCR: 26,388 = 0.31%
TLP: 17,482 = 0.20%
UPDP: 13,176 = 0.15%