Maandamano ya amani kwa waliokosa mkopo HESLB tarehe 15 October

hahahahaaa kweli ripoti iliyotoka juzi kuhusu ugonjwa wa akili we umo aisee!!!utasomaje chuo kama huna mkopo mtoto wa familia maskini

Mimi na wewe nani mwenye akili? Maana nimeuliza swali hujajibu swali langu.
 
Maandamano ni haki ya mtu huombi kibali bali unatoa taarifa kuomba ulinzi!!!tatizo watanzania ni mambumbumbu mpaka basi hayajui haki zao



wewe umetoa taarifa na je hiyo taarifa imekubaliwa? Makee mkuu wa police wa eneo husika anauwezo wa kukataa kama anamashaka na hayo maandamano juu ya usalama wa raia, sasa sijui kama taarifa yako ishakubaliwa. Hamna haki isiyokuwa na mipaka
 
Acheni uoga nyie watoto wa mama ntilie! NINYI MNAONA SAWA TU HAWA VIONGOZI WA NCHI HII WANAVYOJIGAIA PESA, KAMA KWENYE BUNGE LA BUDGET LILILOPITA UMEONA NI JINSI GANI WANAVYOJIGAIA 300000 NA KUPITISHA KATIBA YENYE GANDA JIPYA LAKINI NI YENYE MAUDHUI YA ZAMANI YENYE KUSHIBISHA MATUMBO YAO, MWANAFUNZI ANAKOSA DAWATI LA KUKALIA NA WAKATI MITI IMEJAA LUKUKI, CHA KUSHANGAZA ZAIDI NI MWANAFUNZI ALIYEPAMBANIA ELIMU NA KUFIKA ELIMU YA JUU ANAKOSA KUSOMESHWA NA SERIKALI WAKATI WABUNGE WANAGAWANA POSHO YA LAKI 3 NA KUCHEZA KITORONTO KWA KUPITISHA KATIBA MBOVU NA ILIYOOZA. Jitambue, MABADILIKO NI MIMI NA WEWE, SOLIDARTY FOREVER
 
Nani Muoga???Toa Sehemu Ya Sentensi Niliyoonesha Uoga wangu.

Unakera hadi natamani kukutukana mods wanifungie,kwa kushindwa kusimamia khaki yako na ya wengine nina mashaka na stability ya maisha yako
 
Nadhani haya ndiyo maandamano ya muhimu sana.
UKAWA wanasemaje kuhusu haya maandamano.

Mngefanya kwanza mkutano mkubwa Jangwani ili wananchi nao wajue huo ubaguzi wa wengine kupata na wengine kukosa.
Ule ni mkopo kwa nini usitolewe kwa kila mwanafunzi aliyeomba?
 
Ninacho kiamini sio kwamba serikali ina pesa ila haitaki kutupa,ila yote washapewa wenye nchi wakati wanachakachua maoni ya wananchi dodoma so kuandamana tena bila kibali inaweza sababisha vipigo tu kama wengine wanavyo pigwa bila hatia
 
Nakumbuka kipindi nipo chuo niliteseka sana na hii kitu.mwaka wa kwanza nimpeta bila ya shida inakuja mwaka wa pili naambiwa huwezi kupata mkopo kisa eti nalipiwa na wizara ya fedha...imeniuma hadi leo siwezi sahau kwasababu nilienda kwny ofisi zao (heslb) kwa zaidi ya mara 15 bila ya msaada.

Acha tu..na mie sirudishi mkopo wao mpaka watakaponibaini nilipo shenzi hawa wanatusumbua na hela zetu.
 


Kamati ya kukusanya maoni ya rasimu ya katiba mpya unasema siyo matuzi rasmi ya fedha ambazo zinatokana na kodi za watanzania, hivi wewe ni mzima kweli wewe? Hapana shaka kila Mtanzania anashauku ya kupata katiba mpya yenye kujitoshereza afu Leo hii unakurupuka tu etu tuandamane kudai hela za mikopo. Fyuu kabisa yan hapo utaandamana mwenyewe.
Polee
 
siwezi kuwasapoti kuandamana kwa kuwa hamna mkataba kuwa lazima aliyeomba atapata, ila kiukweli na kwa masikitiko makubwa nimesononeka kuona watoto wa maskini ndio wamekosa mikopo na matajiri ndio wamepata, wengi waliosoma diploma wamenyimwa mikopo. Nasikitika kuna watoto wa majirani zetu kama watatu familia tofauti tofauti licha ya kuhangaika kusoma leo hii woote wamekosa mikopo alaf zaidi ni watoto wa kike... naiomba bodi ifikirie mara ya pili awa watoto pamoja na wengine wanaostahili waweze kutimiza ndoto zao. Poleni sana ¬¬
 
ningekuwa dar ningeandamana koz nimekosa mkopo ila kesho nitaenda shamba kulima nikajiandae mwaka kesho
 

Ngoja tuone kama waziri kivuli wa UKAWA kama atakuwa kwenye haya maandamano haya ndio maandamano yenye tija na hapa ndipo pa kupima unafiki wa vijana mambo yao msingi wanajitenga yakija maandamano yasio na kichwa wala miguu ndo wa kwanza kuandamana
 
Ngoja tuone kama waziri kivuli wa UKAWA kama atakuwa kwenye haya maandamano haya ndio maandamano yenye tija na hapa ndipo pa kupima unafiki wa vijana mambo yao msingi wanajitenga yakija maandamano yasio na kichwa wala miguu ndo wa kwanza kuandamana

Kweli kabsa Mtamile, haya ni maandamano ya amani, syo vurugu! Mi nataka watuambie kwanini mtoto wa maskini anakosa mkopo ilihali wanavigezo halali ya kupata! Wanasiasa wanashindwa kukosa uzalendo na kufanya madudu bungeni, wakidhani wanachi hawashudii kitoronto wanachocheza baada ya kuweka kibindoni kila siku tsh 300000 km Posho ya siku! Hakuna kuogopa, dai haki yako! Solidarty forever!
 

Kesho tunakinukisha vibaya sana.
 
Solidarty forever, hii nchi si maskini! Watanzania ndyo tu maskini! Hakuna ki2 watatueleza board ya mkopo kwani wao wanakula mishahara minono na kukaa kwenye kiyoyozi nakutembelea magari ya mamilioni huku wakishindwa kumgaia mtoto wa mkulima tena maskini kama nini mkopo wa kusomea! Hakuna ki2 wanafanya hawa wa2mishi wa serikali, haya ndyo maisha bora kwa kila mtanzania waliyokuwa wana-ahidi! Tanzania inanuka rushwa, Ufisadi na ubadhirifu wa pesa huku ikisifika kwa amani! Hakuna ki2 wanafanya hawa wa2mishi wa Umma! Jana tarehe 13/10/2014 mnamo saa 7 mchana wakati mtoto wa maskini nmekaa na kuhoji hao watendaji wa board, watendaji wakuu wakapanda ma-VX Yao na kutokomea kusiko julikana! Mnacheka na nani, THIS TYME HATUCHEKI NA MTU.
 
Labda waje jw lakini wakija wale wa CCP tutaenda nao sambamba mbona
 
Mabadiliko ni mimi na wewe, serikali hii ina budget ya majanga! Hii idadi ya wanafunzi kukosa mkopo ni janga la taifa! Mabadiliko ni mimi na wewe!
 
Najua wapo wanao jidanganya kuwa kwa vile wamepitia jeshi hata wakiandamana hawata fanywa kitu lakin tambuenii hii nchi wapo wakubwa walio organize maandamano lakini siku ya maandamano walikuwa south africa....walijua nn kingewakuta cku ya maandamano na kuwaacha wale wasio jielewa kuundamanaa

Mnaweza mkaandamana watu 200 na mabadiriko yakafanyika kwa watu wa 5 ambao hata kwenye maandamano hawakuwepo coz mm namini hakutakuwa na kuandika majina kwa walio hudhuria maandamano.......na mkumbuke wakirejea kwenye maandishi nyinyi mtakuwa na makosa coz hakuna MKATABA KATI YA MUOMBAJI NA MTOAJI KUWA ukiomba mkopo ni lazima upateee.....mda mnao poteza na hela za daladala mnazo poteza na hela za maji mnazopoteza ni heli ungekaa nyumbani na familia ako mkajadili nn kifanyike kupata pesa mtu kwenda chuo...... lakin co huo upuuzi wa kuandamana while hakuna cha kubadirika.....yalishindwa maanda mano makubwa ya kupinga katiba kitu muhimu nchin sembuse mkopo....guyz akili za mwenzio changanya na zako walikosa watu kipnd cha nyuma mkopo lakin wapo kimya leo hii muwe nyinyi

Pengine huyu ambaye leo ana organize mkopo pengine hata hakuomba mkopo au kapewa kabisa na pengine asiwepo kwenye maandamano.....lakini wengne walivyotoa majina ya walio kosea kujaza form hamkutaka kwenda kubadirishaaaaaa.....wengine hata application hamkufanya leo hii unataka kuandamana.....am sure 100% maamuzi ya nchi hii huwa hayarudi nyuma kamweeeeeeee......waliandamana kupinga mauaji ya wandishi wa habari lakin nthng has bn done......nyieeeeee

Nendeni wapewe wasio hudhuria maandamano na ww kapoteze mda wako akili ya mwenzio changanya na yako

Ol da best
 

Hakuna kitu unaelewesha hapa wewe Danya, mimi nafikiri wewe una zile akili za kunguni yenye dhambi ya uoga, cdhani kama unawaza vizuri na halmashauri yako yankichwa inakushauri vizuri, sikulaumu maana pengne nawe ni mmoja wa wanaokula kodi ya wananchi maskini kwa kugawana posho huku Mwanafunzi wa shule ya msingi akikaa chini sakafuni sababu eti madawati hakuna na wakati nchi imejaa misitu! Hakuna kitu unaweza kunieleza wewe maana ni dhahiri unatumika pasipo kujielewa! Wewe uliona wapi nchi ikaendelea pasipo kuwekeza katika sector ya elimu! Hii SIRIKALI (serikali) inatuzuga hapa kwa kujifanya inawapa walimu kipaumbele wakati mazingira ya Mwalimu husika ya kufanyia kazi ni mabovu, juzi wanakuja na formula ya kuwakata elfu 10 walimu ili wajenge maabara, kwanini wasianze kujikata wao katika posho zao za laki 300000 wanazogawana kwa siku! Hamna kitu unaongea wewe Danya! Waliokutuma waambie kwamba wamekuagiza utumbo! Unatoa quote za uwoga, eti akili za kuambiwa changanya na zako! Nyamaza kama huna hoja za msingi, si unawakilisha utumbo!
 

Mkuu hebu soma kwanza Thread nzima harafu ndo urudi
 
nawatakia maandamano mema MUNGU awaongoze kisha awapunguzie laana viongozi wabadhilifu wa mali za umma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…