Pre GE2025 Maandamano ya CHADEMA: Lissu kwenda kuripoti Ofisi ya RCO Kinondoni asubuhi hii

Pre GE2025 Maandamano ya CHADEMA: Lissu kwenda kuripoti Ofisi ya RCO Kinondoni asubuhi hii

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu amesema asubuhi hii (leo, Jumatatu Septemba 23, 2024) amefuatwa na maafisa wa Jeshi la Polisi nyumbani kwake, na kuelezwa kuwa anahitajika kuripoti kwa RCO wa mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Dar es Salaam, ambapo amesema yuko tayari kwenda kuitikia wito huo;

Pia soma: Freeman Mbowe: Tutaandamana kudai watu waliopotea

"Three Police vehicles full of officers in riot gear are outside my residence. They've informed me I'm directed to be taken to the Regional Crimes Officer Kinondoni. I'm getting ready to go"

Pia soma: Yanayojiri maandamano ya CHADEMA

1727068249690.png
 
Atii bila shuruti,huo ni utaratibu wa kawaida kabisa katika nchi...
 
Alijua fika atafatwa kwake kabla ya maandamano na akakaa kusubiri mpaka afatwe. Awa viongozi wa chadema wanacheza na akili za wafuasi wao mazuzu hakuna aliye seriously na kuandamana.

Bado mbowe kuja na excuse yake.
 
Bila shaka yule dreva wake wa kwenye lile tukio la kupigwa risasi kule Dodoma, amesharejeshwa nchini. Hivyo ile kesi yake iko mbioni kuanza kwani dreva huyo ndiye shahidi muhimu sana kwenye hiyo kesi na alikuwa anasubiriwa kwa hamu kujua mbichi na mbivu katika sakata hilo.
 
“Enyi mlioamini! Kuweni wasimamizi wa uadilifu, kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, mashahidi kwa uadilifu. Wala chuki ya watu isikufanyeni kutenda isivyo haki. Tendeni haki; hiyo ndiyo iliyo karibu zaidi na ucha Mungu. Na mcheni Mwenyezi Mungu; hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye khabari za yale myatendayo.

”Aya hizi zinafundisha kuwa haki lazima ipewe kipaumbele katika hukumu, na kuhukumu kwa usawa ni sehemu ya ucha Mungu.
Qur'an inaweka msingi thabiti wa maadili ya haki katika hukumu na inawataka Waislamu kuwa waaminifu na waadilifu katika kila jambo la hukumu na maamuzi.
 
Back
Top Bottom