Maandamano ya CHADEMA Mbeya: Lissu asema hatujamkimbia Makonda kwenye Mdahalo, ni jambazi anatakiwa kuwa gerezani

Maandamano ya CHADEMA Mbeya: Lissu asema hatujamkimbia Makonda kwenye Mdahalo, ni jambazi anatakiwa kuwa gerezani

Mwashamba yupo kwenye kilio kafatwa na watoto wa mjini wakamwambia kuwa Kuna teuzi inakuja ila atoe kiasi flani jamaa kajiloki kaachwa solemba hana hamu
Kwa kilichotokea jana Mbeya ninauhakika gagula wa Mbeya atamtema, atagundua anamdanganya la sivyo kwanini akimbilie milimani Kawetere!
 
Maandamano ya CHADEMA yanaendelea Mbeya sasa hivi


Tundu Lissu:

- Tutaandamana mpaka tutakapopata Katiba mpya, mfumo mpya wa uchaguzi, mpaka tutakapowaondoa madarakani hawa wanaotunyonya.

- Hatuandamani kwa sababu tunataka kujifurahisha, au kufanya mazoezi, tunaandamana sababu tuna hasira na hiyo hasira ndiyo itakayoleta mabadiliko. Tunaandamana kwasababu njia za mazungumzo zimekataliwa, mlango mmoja ukifungwa mingine lazima ifunguliwe kwahiyo njia ya maandamano ni njia ya shinikizo kwa wale waliokataa meza ya mazungumzo.

Akijibu kuhusu madai ya Makonda kuwa CHADEMA ndio waliokataa maridhiano Lissu amesema, Mimi kwenye maridhiano sijauona Makonda nimemuona kinana, Mzanzibari Spika na wengine kwenye maradhiano. Hawa ndio wanaweza kuzungumza kimejadiliwa kitu gani na tumeshindwana kwenye kitu gani, sio Paul Makonda.

Akijibu kuhusu Makonda kusema amewakimbia kwenye Mdahalo Lissu amesema, "Sisi tutakaaje na mhalifu yule, sisi tutakaaje na muuaji yule, kuteka watu nyara, kuvamia vituo vya televisheni kama clouds tutakaaje na mtu anayepaswa kuwekwa gerezani? Na haya ni kwa uthibitisho wa mambo aliyofanya na anayotuhumiwa kuyafanya, ndio maana Wamarekani wamempiga marufuku kwenda Marekani, ni mhalifu, hatuwezi kukaa na jambazi. Watanzania wajue kwamba hatuwezi kukaa na jambazi.

Mwabukusi

Wanatuambia wamebinafsisha bandari lakini ukweli ni kwamba wameziuza. Tutaendelea kupiga kelele na kukataa mikataba hii sababu mikata hii taitendei haki kama Watanganyika.

Swala la bandari halijaisha mahakamani, mahakama ilisema imefungwa mikono, mahakama ilisema sheria imekiukwa, sisi tunataka mikono ifunguliwe na bandari isrudishwe kwa watanganyika. Suala hili halijatulia bado bado kwani tumekata rufaa, hata wao hawajatulia ndio maana wamewadanganya watanzania kuwa wamefanya maerekbisho. Mimi nawauliza kama wamefanya marekebisho watuambie lini IGA ilienda bungeni ambao bunge, ikatambua unquestionable terms zote katika wizara husika, lini zilifika mbele ya baraza la mawaziri na kufanyiwa kazi, lini zilikwenda bungeni na kufanyiwa kazi, na lini zilikwenda Dubai kujadiliwa na kusaniwa? Hawasemi ukweli, jambo la bandari bado sana kuisha.

Hao ni wavuta bangi hamna akili hapo. Mara mzanzibari, hana adabu huyo mbwa. Mara watanganyika nchi ambayo haipo kwenye ramani ya dunia. Ni zuzu tu ndio atawasikiliza.
 
Hao ni wavuta bangi hamna akili hapo. Mara mzanzibari, hana adabu huyo mbwa. Mara watanganyika nchi ambayo haipo kwenye ramani ya dunia. Ni zuzu tu ndio atawasikiliza.
Tanganyika haipo kwenye ramani ya dunia? Mbona wilaya ya Tanganyika ipo, uliwezaje kujiunga na Jamii Forum wakati elimu yako ni ya madrasa!
 
Lisu ni tofauti sana na Mbowe,
mara nyingi Mbowe anaongea point kwenye mambo husika ya kitaifa kwa ufafanuzi mpaka watawala wanahisi lipo tatizo mahalla.

balaa sasa ni Lisu litakalo kuja mdomoni ndio hilohilo,akisikia maumivu ya mguu juu ya jukwaa anaruka na Magufuli.
 
Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Mbowe amewashukuru Waandamanaji wa Mbeya kwa kusema "Mungu wa Mbinguni awabariki sana watu wa Mbeya"

Nami Johnthebaptist na ndugu yangu mzee Mgaya kwa niaba ya Kanda ya Nyasa tunasema "Amina"

Yesu Kristo alisema Wabarikini watu muingiapo na mtokapo. Ahsante sana Mh. Mbowe 😀
 
Mwenyekiti wa Chadema mh Mbowe amewashukuru Waandamanaji wa Mbeya kwa kusema " Mungu wa Mbinguni awabariki Sana Watu wa Mbeya"

Nami Johnthebaptist na ndugu yangu mzee Mgaya kwa niaba ya Kanda ya Nyasa tunasema " Amina"

Yesu Kristo alisema Wabarikini Watu muingiapo na mtokapo. Ahsante Sana mh Mbowe 😀
Chairman alimfurahisha sana Dr.W.P.Slaa sikuile kwa kumpatia chance ya kuzungumza na wana mbeya wachache walioshiriki maandamano mdororo, Lakin pia alimdisapoint sana puppet baada ya kumbania kuzungumza akati alikua amejiandaa vizuri kichizi kubwabwaja...

Chairma anatumia mbinu za kisayansi sana kumkwepa kibaraka
 
Mwenyekiti wa Chadema mh Mbowe amewashukuru Waandamanaji wa Mbeya kwa kusema " Mungu wa Mbinguni awabariki Sana Watu wa Mbeya"

Nami Johnthebaptist na ndugu yangu mzee Mgaya kwa niaba ya Kanda ya Nyasa tunasema " Amina"

Yesu Kristo alisema Wabarikini Watu muingiapo na mtokapo. Ahsante Sana mh Mbowe 😀
Sasa na ccm watasemeje hapo
 
CHADEMA nao wameiga matarumbeta ya CCM
Jana RC wa mbeya Juma Omera ameyaita maandamano ya CDM kuwa ni ya kutafutia Kiki.

Akashauri kuwa wananchi mkoani humo kujifanyia shughuli zao badala ya kwenda kwenye maandamano hayo.

Nafikiri alikuwa anajidanganya sana maana yeye pia ni binadamu kama wengine tu.

Tupo hapa Mbalizi tunamsubiria mwenyekiti wetu taifa ili tuanze kupandiaha kilima na kuingia jijini.View attachment 2909824
 
Back
Top Bottom