Maandamano ya CHADEMA yamelipaka matope taifa

Tabutupu

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2010
Posts
13,206
Reaction score
18,549
Kitendo cha vyombo vya kimataifa kuripoti maandamano haya kwa sura kwamba raifa sasa limerudi nyuma kwenye kiasi cha kulinganishwa na nchi za kidikteta ni jambo ambalo kama watanzania limetupa hisia mbaya.

Maandamano ya chadema ambayo kwa nje yanao ekana kuto fanikiwa lakini impact yake imekuwa kubwa kupita maandamano yoyote ambayo yamewahi kufanyika na chama cha siasa.

Serikali inahitaji kuliangalia hili kwa jicho la kijasusi na kikachero, ili kunusuru taifa hili kuwekwa kwenye kundi moja la nchi za hovyo zisizo fuata demokrasia.
 
Samia analifungamanisha taifa letu na nchi za kiarabu amabazo hazifuati misingi ya kidemokrasia, ndiyo maana hajali kitu. Na maliasili zetu zote anawauzia waarabu.
 
Tunajitakia wenyewe. Zamani niliandika makala kuhusu siasa za Afrika. Nikasema viongozi wengi wa Afrika wanaahidi mengi na mara tu wakipata madaraka hubadilika. Huanza vizuri mwanzoni, lakini baadaye hubadilika. Kuna mifano mingi. Nakumbuka John Macelela akiwa Waziri Mkuu wakati wa Serikali ya Awamu ya Kwanza aliwahi kusema: "Waafrika hatuna utamaduni wa kuendeleza mazuri tuliyonayo au tunayoyakuta."
 
Wazungu wanataka rasilimali zetu, askari wanalinda mishahara yao, viongozi wanalinda tawala,(madaraka) yao,, matajiri wanalinda mali zao, sisi kapuku tunapigania uhai wetu. Ila mwenye nguvu siku zote ndiye mshindi.
 
Wazungu wanataka rasilimali zetu, askari wanalinda mishahara yao, viongozi wanalinda tawala,(madaraka) yao,, matajiri wanalinda mali zao, sisi kapuku tunapigania uhai wetu. Ila mwenye nguvu siku zote ndiye mshindi.
Wewe ni mjinga. Nani ana nguvu kati ya hao watumishi wa raia (rais, mbunge, polisi, jaji au waziri)?

Raia ndio wana nguvu na ndio waajiri wa wote hao. Hivyo raia wanapotaka kuandamana kudai haki zao na serikali kutumia nguvu kubwa kuwazuia ni sawa na kumfokea boss wako, anaweza kukuvumilia kwa muda ila kuna siku atakufukuza kazi
 

, sasa hizo nguvu zako zimekusaidia nini zaidi ya kulialia.
 

, sasa hizo nguvu zako zimekusaidia nini zaidi ya kulialia.
 
Maandamano yaliyofanywa na Polisi tarehe 23 September 2024 yamethibitisha madai ya Chadema kuwa CCM inalitumia jeshi hilo kukandamiza upinzani na hata kuiba kura nyakati za uchaguzi.
 
Unaosema hawana nguvu ,wako madarakani since 1961, unadai, wanaiba kura, wanapora ardhi, wanateka, wanauwa, wanabadili mikataba/sheria watakavyo, wanawekana ajira kiukoo, wanafanya kila kitu upo tu. Halafu unajiita una nguvu. Hicho ni kichekesho. Nguvu zako zimewazuia kuharibu nini kati ya hayo. Mwenye nguvu halisi halii lii, anapambana, anashinda anamiliki, anatawala. Tunisia, Libya, Egypt, na kwingineko wakisema wana nguvu ni sahihi. Lakini nguvu za ku type huku unazeeka kulilia kuonewa, huo ni ubwege. Mwenye nguvu au mpishe au pambana naye. Huna nguvu za ummma wala jijiko.
 
Jombaa ni just a matter of time. Kuna dynasty ziliwahi tawala for 1000 years ila in the end? Zote ziliangushwa sembuse kizimkazi dynasty
 
Lawama zote kwa Samia Suluhu Hassan.
 
Ni zaidi ya tope kaka, Taifa limepakwa mafuta limepakatwa na demokrasia wameibend over.
 

Attachments

  • 20240921_041858.jpg
    140.9 KB · Views: 3
Tunasubiri uchaguzi kuona Polisi kuwa wengi katika vituo vya kura kuliko raia wanaopaswa kupiga kura
Ndiyo imeanza hiyo!!
 
Matukio ya utekaji na mauaji kwa wakosoaji na wapinzani hasa Chadema yamezidi kiwango cha enzi za awamu ya tano hiki ni kiashiria kuwa hata uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu utavurugwa kwa kiwango kibaya zaidi kuliko ilivyokuwa enzi za awamu ya tano. Nchi inapelekwa kuzimu kabisa hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…