Maandamano ya Gen-Z: Ukimya unaonekana kama ushindi kwa watawala, lakini ukweli ni mwingine

Maandamano ya Gen-Z: Ukimya unaonekana kama ushindi kwa watawala, lakini ukweli ni mwingine

Kama ilivyotangazwa mapema, kundi la vijana maarufu kama Gen-Z lilipanga kufanya maandamano tarehe 9 Desemba kupaza sauti juu ya masuala ya kijamii, kiuchumi na kisiasa yanayoikabili Tanzania. Hata hivyo, mpaka sasa maandamano hayo hayajatajwa wala kuonekana popote nchini. Kwa macho ya juu juu, hali hii inaweza kutafsiriwa kama ushindi kwa walioko madarakani, hususan kutokana na kujengwa kwa taswira kwamba vijana wameogopa au kuyumba kwenye msimamo wao.

Lakini kufikiri hivyo ni kupuuza uhalisia wa kile kinachoendelea Tanzania tangu uchaguzi wa Oktoba 29. Tangu siku hiyo, taifa limeingia kwenye hali ya sintofahamu na mkanganyiko ulioleta athari za kweli kwenye uchumi, diplomasia, na mwenendo wa kijamii.
​
TENSION YA KISIASA NA ATHARI ZAKE ZA KIUCHUMI
Tangu matokeo ya uchaguzi kutangazwa, nchi imekumbwa na tension kubwa. Wawekezaji, ambao kwa kawaida hutegemea utulivu wa kisiasa kabla ya kuweka fedha zao, wameamua kugoma kuwekeza mitaji mipya. Kutokuwa na uhakika juu ya mwelekeo wa kisiasa na uwezekano wa machafuko kumewafanya wengi kupunguza kasi au kusitisha mipango yao ya uwekezaji.

Athari ya moja kwa moja ya hili ni kudorora kwa uchumi, kuchelewesha miradi, kupungua kwa ajira mpya, kushuka kwa thamani ya fedha, na kupungua kwa mzunguko wa pesa kwenye biashara za kawaida. Wakati serikali ikionekana shwari juu ya kutofanyika kwa maandamano, hali halisi ya kiuchumi inaendelea kuwa ngumu kwa wananchi wa kawaida.
​
MISIMAMO YA JUMUIYA YA KIMATAIFA: ISHARA YA MAMBO SI SHWARI
Katika majuma machache yaliyopita, jumuia za kimataifa zimekuwa zikituma ujumbe mzito juu ya hali ya kisiasa Tanzania. Mashirika ya haki za binadamu, balozi mbalimbali, na taasisi za kimkakati zimeeleza wazi wasiwasi wao kuhusu mwenendo wa kisiasa, haki za raia, na usalama wa wananchi.

Kauli hizi si tu kwamba zinaathiri taswira ya nchi kimataifa, bali pia zinaongeza shinikizo kwa serikali kuhakikisha kunakuwa na mazungumzo, upatanisho, uwazi na kuheshimu misingi ya demokrasia. Nchi inapopoteza imani kwa mataifa washirika, matokeo yake huturudiia kwa njia ya kupungua misaada, ongezeko la masharti ya mikopo, na hata kusuasua kwa ushirikiano wa kiuchumi.
​
KUDORORA KWA SHUGHULI ZA KIJAMII
Miongoni mwa athari zinazoonekana wazi ni kudorora kwa shughuli za kijamii. Wananchi wamekuwa na taharuki, wafanyabiashara wamepunguza safari na manunuzi, taasisi mbalimbali zinafanya kazi kwa tahadhari, na hata maisha ya kawaida ya miji mikubwa yanayumba. Watu wanaishi katika hali ya kutokuamini kinachoendelea, na hilo linaathiri hali ya utulivu wa kihisia na kiakili kwa jamii kwa ujumla.
​
UKIMYA WA GEN-Z SI UDHAIFU, NI DALILI YA MPASUKO MKUBWA
Kutotokea kwa maandamano hakumaanishi kwamba hoja za vijana au wananchi zimefutika. Badala yake, ukimya huu unaonesha mpasuko wa ndani ya jamii, mahali ambapo watu wanahisi kunakuwa na gharama kubwa za kupaza sauti zao. Hii ni ishara kwamba sauti zimebanwa, hofu imeongezeka, na demokrasia inahitaji nafasi zaidi ya kupumua.

Gen-Z wameonyesha mara kadhaa kwamba wakiamua kusimama, wanafanya hivyo kwa nguvu na ubunifu mkubwa. Ukimya wao wa sasa usitafsiriwe kuwa ni kukubali, bali ni ishara ya mazingira magumu ya kuonyesha msimamo wao hadharani.
​
HITIMISHO
Badala ya kushangilia kutofanyika kwa maandamano, ni muhimu viongozi kuona picha kubwa: Nchi ina msukosuko, uchumi unayumba, diplomasia inatikisika, na wananchi hawana imani. Ushindi wa kweli haupatikani kwa kupiga marufuku sauti bali kwa kurejesha imani ya wananchi, kujenga maridhiano, na kuimarisha misingi ya haki na demokrasia.

Tanzania ina uwezo mkubwa, lakini uwezo huo unahitaji utulivu wa kisiasa, ushirikishwaji, uwazi na demokrasia yenye nguvu.

​
Wewe BWEGE badala utoke ukaandamane, wewe uko humu kutunga nyuzi za kuhamasisha. Nyabaaaf
 
Bado siku ni ndefu hii
Sasa si uingie barabarani na wewe!! Mbona mnategemea wengine tu ndiyo waingie?? Duh Mshana Jr bana!! Akiandika utadhani ni mtu wa vitendo!! Kumbe ni key board warrior
 
Jeshi limepoteza heshima. Hamna jeshi Tanzania.

Niwasenge Tu. Walinzi wa CCM hao.
Mna hasira za kipumbavu nyie Nyumbu!!
Mlitaka kuifanya nchi kama matako yenu, sasa mmeshindwa mnaona hakuna jeshi. LOFA NA WAPUMBAVU.
 
Kwa akili ya samuya hawezi kung'amua hili, tusubiri propaganda kwamba wamefanikiwa kudhibiti mipaka hivyo waandamanaji kutoka nje hawakuingia nchini kuvuruga amani yetu!!

Chai nyingine watatuambia wamefanikiwa kudhibiti miamala ya NGO's kadhaa ambapo pesa zingetumika kulipa waandamanaji!

Yaani hii serikali ya mama inaishi kwa propaganda za kitoto kwelkwel!
Mie nadhani wamefeli watawala maana hauwezi kubeba siraha nzito nzito dhidi ya watu wasio hata na fimbo zaidi ya mabango yao. Hii ndo inaitwa kuua sisimizi kwa nyundo. Hapa tumefeli sote tu
 
Jeshi limepoteza heshima. Hamna jeshi Tanzania.

Niwasenge Tu. Walinzi wa CCM hao.
Polisi na wanajesh huwa wapo kulinda maslai ya watawala na kuwashughulikia watu wote watakaoonekana ni threat kwa watawala na maslai yao....PATHETIC..
 
Acheni kuchochea vijana wakapoteze uhai wao hali ya kuwa nyinyi mpo majumbani kwenu mnasubiri watu wafe ili mlipwe na wazungu.
Mambo huwa ni hivyo..

Ukombozi hupiganiwa na watu wachache sana. Soma na jifunze historia uelewe...

Gidioni kamanda wa jeshi la Israel aliongoza jeshi la watu 300 tu kupigana na jeshi kubwa la mamilioni ya Wamidiani. Hapo kabla alipoambiwa na Mungu jiandae ukawakomboe ndugu zako toka utumwa wa kuonewa na Wamidiani, alikusanya jeshi la watu 300,000. Mungu akamwambia hawa ni wengi mno. Akawapunguza hadi 30,000, akaambiwa hawa bado ni wengi mno. Akapunguza hadi watu 300 tu na ndio walioenda vitani na kulishinda jeshi kubwa la waovu la taifa la Midiani....

Kwa hiyo hiyo propaganda yenu ya mbona hamtoki na kuwaacha wachache - GenZ, ni ya kijinga toka kwa watu wasio na ufahamu pekee juu ya mikakati ya kivita. Lakini all in all ni kuwa, KAMA MUNGU WA MBINGUNI, MUNGU MKUU ASIPOKUWA PAMOJA NASI UPANDE WETU, basi kuipigana kwetu ni kazi bure..

Tuko Watanganyika karibu 70,000,000 sasa. Hawa hawawezi kutoka na kwenda vitani - barabarani wote. Ni watu wachache tu wanaweza kupigana na kuushinda uovu...

Sisi wengine si kwamba hatushiriki mapambano haya. Tunashiriki kwa njia zingine...
👉🏻👉🏻Wako walio field (infantry soldiers - GenZ)
👉🏻👉🏻Wako wana mikakati (strategists) - ukipenda tuite jina lolote lile kama vile "Computer Keyboard Fighters" na;
👉🏻👉🏻Wako wanajeshi wa kupigana vita visivyoonekana kwa macho ya nyama na mwili huu - vita vya kiroho (maombi ya kanisa) tukiongozwa na watu kama Mch. Josephat Gwajima, TEC - Catholic Church na wengine usiowajua .

Maombi (vita ya kiroho)ndio silaha hatari zaidi na mnayopaswa kuiogopa zaidi kuliko hata walio field yaani GenZ...

Hebu vuta fikira kidogo kurudi nyuma. Kulitokea nini pale Askofu Josephat Gwajima alipotangaza siku 14 za maombi ya kuomba utekaji na watekaji kwisha Tanganyika?

Kama umesahau ni kuwa, watekaji waliona tunaenda kupigwa na kupotezwa. Cha kufanya kilichokuwa ndani ya uwezo wao ni haraka haraka kinyume cha sheria kukimbilia kufunga majengo ya kanisa la GCTC - Ufufuo na Uzima linaloongozwa naye..!!

Ni wajinga hao. Kwa sababu wanafikiri Mungu anakaa ndani ya majengo au usajili wa jina la dhehebu la kanisa. Hawakujua kuwa Mungu anaishi ndani ya watu waliomkubali na kumpokea..

Maombi yaliendelea. Na matokeo yake the whole CCM government and Samia are both falling down to their graves....!!
 
Watawala wameficha kichwa chini kama mbuni. wanafikiri tatizo limeondoka kwa kuua vijana! Damu itanena tu
 
Back
Top Bottom