Kesho siku ya jumatatu tar. 23.09.2024 yanatarajiwa kufanyika maandamano ya wananchi wakipinga serikali kutochukua hatua stahiki dhidi ya Utekaji, utesaji na mauaji ya watu ambayo yamekuwa yakifanyika hivi karibuni hapa Nchini. Maandamano hayo yanakwenda ama kuwamaliza kabisa kisiasa na kimahusiano viongozi waliopo madarakani au kuwajenga.
Ikiwa viongozi wetu waliopo madarakani watatumia nguvu kubwa zaidi kuzima maandamano hayo mpaka kupelekea majeruhi au vifo, kwa hakika hilo litakuwa ndo kaburi lao kisiasa na kimahusiano.
Ikumbukwe kuwa, mambo yanayosababisha maandamano kufanyika tayari yameshapigiwa kelele sana na:-
*Watanzania mbalimbali.
*Viongozi mbalimbali wa kisiasa.
*Taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa.
*Viongozi mbalimbali wa Dini hususani Roman Catholic yaani TEC na Masheikh.
*Mabalozi mbalimbali hususani wa Marekani.
Kwa maana hiyo, maandamano hayo yatafuatiliwa kwa karibu sana na Dunia nzima.
Maoni yangu ni kwamba, Mama asikubali kuchafuliwa kizembe namna hiyo, hivyo:-
*Afute kauli yake ya juzi dhidi ya Mabalozi nk.
*Leo hii kabla ya maandamano, afanye mazungumzo na viongozi wa CHADEMA ili kutafuta suluhu.
*Kama hataki mazungumzo, basi azuie maaskari kutumia nguvu kubwa, yaani maaskari wasimpige mwandamanaji hata mmoja. Hiyo itakuwa ndo salama ya Mama.
Nawasilisha.