Maandamano ya kupinga ujenzi wa bomba la mafuta(EACOP) Kati ya Tanzania na Uganda nchini Ufaransa ni "Economic Espionage"

Maandamano ya kupinga ujenzi wa bomba la mafuta(EACOP) Kati ya Tanzania na Uganda nchini Ufaransa ni "Economic Espionage"

Artificial intelligence

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2021
Posts
1,265
Reaction score
2,252
Maandamano yaliyofanyika nchini Ufaransa leo tena yakiongozwa na Mkenya ni kiashiria cha ujasusi wa kiuchumi kuhusu Tanzania&Uganda juu ya ujengaji wa bomba hilo.

Kenya katika ukanda huu wa maziwa makuu imekuwa ikitumiwa sana na washirika wa magharibi na kampuni nyingi binafsi katika kufanikisha operations mbali mbali za kijasusi.

Ni wazi kwamba baadhi ya nchi na kampuni kadhaa hazitafurahishwa na ujenzi wa bomba hilo kutokana na sababu za kiuchumi. Kwahiyo watajaribu kukwamisha mradi huu kwa namna yeyote ile na leo tumeanza kuona ishara hizo.

Serikali zote mbili Tanzania na Uganda kwa kutumia vyombo vya ulinzi na usalama ni lazima washirikiane na kujipanga kikamilifu na kuhakikisha zinakuwa na counterintelligence strategies madhubuti ili kukamilisha ujenzi huu.

Mwigulu Nchemba

Screenshot_20220327-211658_1.jpg

Screenshot_20220327-203358_1.jpg
 
Kwenye ligi kama hizi, nilikuwa namwelewa sana shujaa wa Afrika JPM. Angesikiliza upuuzi hata hili bwawa la nyerere tusingejenga.Mama hangaya, kaza buti.
Kwenye huu mradi kutakuwa na subotage ya hali ya juu, ni lazima Serikali zote za nchi mbili Tanzania &Uganda ambazo ndiyo washirika na wanufaika wakuu wajipange kikamilifu.
 
Kenyata sio mtu mzuri na bahati mbaya awamu hii wamejipeleka huko.

Endeleeni kumchekea tu.

Ameshatuchungulia na kutuona tumekua wepesi.

Tusilale tufanyeni retaliation na kumminya sehemu itayomuuma vizuri.
 
Duh... Hivi hapa Kuna Undugu Kweli..? Wakenya ni Wanafiki Wakubwa..!
Kama nimeelewa vizuri huyo kinara ni raia wa Kenya lakini taarifa haijasema Kenya ndio imemtuma kufanya hayo maandamano !!

Tuweke akiba ya maneno !!
 
Kenyata sio mtu mzuri na bahati mbaya awamu hii wamejipeleka huko.

Endeleeni kumchekea tu.

Ameshatuchungulia na kutuona tumekua wepesi.

Tusilale tufanyeni retaliation na kumminya sehemu itayomuuma vizuri.
Vyombo husika si vipo
Inabidi wapambane nao
Kwenye vita hivyo

Ova
 
Economic Espionage

Unawayawaya tu. Acha kutumia maneno usiyojua. Ukisema sabortage unakuwa sahihi kukiko espionage ambayo kwa kiswahili chepesi ni “ujasusi”!! Maandamo ambayo ni overt events haziwezi kuwa espionage ambayo msingi wake mkuu ni covert - ya kisiri au kichinichini!!
 
Kwanza ni perception yako. Pili kwenye ujasusi hatuna neno sabortage bali tunatumia "neno sabotage".Tatu Espionage & Sabotage katika intelejensia ni twins words, hayahachani, so Sabotage ipo ndani ya Espionage.

Mwisho mimi situmii google kufahamu maana ya neno, Mimi natumia vitabu vyenye maarifa na taarifa na references sahihi kuhusu Economic Espionage nzima, kwahiyo nilichokikusudia na kukimaanisha hapa nakielewa vizuri.
 
Kama nakumbuka vizuri hili bomba mara ya kwanza lilikuwa lijengwe kupitia Kenya mafuta yaende Mombasa. Ila ghafla Uganda ikabadilisha nadhani kwa kushauriwa na muwekezaji kuhusu gharama.

Jambo hilo halikuwafurahisha sana Kenya. Kwahiyo anayedhania yule Mkenya analifanya mwenyewe tuu atafakari zaidi. Na kama ni mwenyewe basi tuone serikali yao ikikemea waziwazi.
 
Wakenya wachache wakiandamana kupinga ujenzi wa Bomba la mafuta,lawama tueapelekee wakenya wote?
Hapo sasa shangaa na wewe !! Ni sawa na baadhi ya watu humu jf ukitoa comments zinazosifu government wanadhani wewe ni wa chama tawala na ukitoa comments za kuipinga wanadhani wewe ni mpinzani !!

Wanasahau kuwa watu wengine wapo neutral !! Hawapo huku wala kule hawasukumwi na mihemuko ya kivyamavyama !! Narudia tena wapo watu wanasimama katika ukweli tu !!

Hawapo huku wala kule ! Japo Hao neutral pia wanaweza kukosea lakini bado wanakuwa hawajasukumwa na mihemko ya vyama vya siasa, je wale waliotumwa na Mange kimambi kubeba mabango huko majuu kipindi kile walitumwa na Tanzania !!??
 
Maandamano yaliyofanyika nchini Ufaransa leo tena yakiongozwa na Mkenya ni kiashiria cha ujasusi wa kiuchumi kuhusu Tanzania&Uganda juu ya ujengaji wa bomba hilo.

Kenya katika ukanda huu wa maziwa makuu imekuwa ikitumiwa sana na washirika wa magharibi na kampuni nyingi binafsi katika kufanikisha operations mbali mbali za kijasusi.

Ni wazi kwamba baadhi ya nchi na kampuni kadhaa hazitafurahishwa na ujenzi wa bomba hilo kutokana na sababu za kiuchumi. Kwahiyo watajaribu kukwamisha mradi huu kwa namna yeyote ile na leo tumeanza kuona ishara hizo.

Serikali zote mbili Tanzania na Uganda kwa kutumia vyombo vya ulinzi na usalama ni lazima washirikiane na kujipanga kikamilifu na kuhakikisha zinakuwa na counterintelligence strategies madhubuti ili kukamilisha ujenzi huu.

Mwigulu Nchemba

View attachment 2166365

View attachment 2166366
Hiyo ndiyo inaitwa vita ya uchumi mkuu. Mbaya zaidi kiongozi wa maandano ni jilani yetu Mkenya. Kenya siyo jilani mwema mama awe makini nae.
 
Back
Top Bottom