Maandamano ya mabucha ya Nguruwe 1993

Ahsante kwa kuniwekea kumbukumbu sawa kuhusu Sheikh Kassim na BALKUTA, na nilikuwa sifahamu chanzo cha Mwaipopo ambae enzi zile alikuwa maarufu kweli kweli! Tena wala sikufahamu kwamba kumbe alikuwa ni kijana mdogo tu!!

Hilo la mijadala ya Yesu ni Mungu/sio Mungu niligusia kwenye post yangu lakini nika-edit kwa hofu kwamba wengine wasije wakavuruga mjadala manake JF Members bhana, kwa mihemuko ndo wenyewe!!!
 
Hizi block za Internet/social media kutoka kwa JPM mimi huwa hazinisumbui lakini ukweli ni kwamba, mijadala ya aina hii huwa najaribu kuikwepa manake wengine hawakawi kuleta mihemuko ya kidini!!
 
Umeandika kwa ufupi kaka Mohamed.

Wito na hamasa ya kwenda "kuyafunga" mabucha ya nyama ya nguruwe Mbokomu pale Manzese yalitolewa na baadhi ya wahadhir baada ya mtoto wa kiislamu kutumwa nyama na mzazi wake na akajikuta anauziwa nyama ya nguruwe! Mzazi alipofatilia kutaka arudishiwe pesa akakataliwa na wauzaji na yeye akalipeleka public

Katika madai yao Waislamu walisema njia zote za kisheria walizotumia kuhakikisha kunakua na mipaka/kutengwa kati ya maduka ya kuuzia nyama za nguruwe na wanyama wengine kama ng'ombe na mbuzi, sio tu zilishindikana bali pia walikua wanaambulia kauli za kashfa na kebehi kutoka kwa watendaji wa Wilaya/Manispaa ya Kinondoni na Jiji la Dar. Walikua wanadai sheria za kuzuia mabucha ya nguruwe kwenye maeneo ya mchanganyiko zipo lakini kwa makusudi na kwa kuwadharau Waislamu zilikua hazifuatwi

Baada ya sakata lile la kuvamia mabucha ya Mbokomu Pork Centre pale Manzese ili kuondoa "munkari" kwa mkono basi ndipo crackdown ya Masheikh ikafuata. Walisombwa waliohusika na wasio husika. Kama alivyosema mletaa uzi, miongoni mwao alikua Sheikh Kassim Bin Jumaa Bin Khamis, Imamu wa Msikiti wa Mtoro aliyekua safarini Arusha!

Kabda ya hapo kulikua na fukuto la hali ya kutoridhika kwa Waislamu kutokana na kuhisi walikua wanatendewa na serikali kama raia wa daraja la pili. Kuna vijana wanaharakati wa dini ya Kiislamu miongoni mwao ni marehemu Mtengwa Buruhani, marehemu Mdidi Musa, Mjeja na wengineo walikua "wamewaamsha" sana Waislamu na lile kundi lao la WARSHA ya waandishi wa Kiislamu katikati ya miaka ya 1980s kuelekea miaka ya mwanzo ya 1990s

Hii ilichukuliwa kama ni uamsho (renaissance) ya harakati za Waislamu na ni kwenye kipindi hiki (1992) Waislamu walipoamua kuichukua BAKWATA iwe mikononi mwao kwa mapinduzi ili iwe kwa faida yao kabda ya move hiyo kuzuiwa na Rais Mwinyi na baadae Augustine Mrema kuja kuendesha harambee ya pesa kutoka kwa viongozi wa kikristo ili kuiwezesha BAKWATA ifanye mkutano wake mkuu ambao walishindwa kuuitisha kwa muda mrefu kutoka na ukata pamoja na kua na rasilimali lukuki hapa nchini

Kuna watu humu wameandika kuhusu BALUKTA kwamba ilikua inamilikiwa na Sheik Kasim Bin Jumaa. Ukweli ni kwamba BALUKTA (Baraza la Kuendeleza Usomaji Kur an Tanzania) ilikua ni taasisi iliyoasisiwa na kuendeshwa na marehemu Sheikh Yahya Hussein. Taasisi hii ni miongoni mwa taasisi zilizokuja kupigwa marufuku na serikali(nadhani ilifutiwa usajili) katika kile kinachodhaniwa ni kuendelea kuipa BAKWATA nguvu ya kupumua baada ya Waislamu kuipuuzilia mbali

Kaka yangu Mohamed Said sina hadhi wala uwezo wa japo kukusogelea kwa tafiti na uandishi wako ila nime tabaruku katika kile kidoogo sana nikijuacho kutokana na kadhia ile ya mabucha ya nguruwe ambayo yalipelekea kufungwa jela kina Habibu Mazinge na wenzake japo kulikua na very strong "alibi" kwamba baadhi yao hawakuwepo kabisaaa Manzese wakati watu "wakiondoa munkari" kwa mkono
 
Chige,
Kuna pp niliwasilisha kwenye mkutano Chuo Kikuu Cha Kenyatta Nairobi mwaka wa 2007 bahati mbaya sana ni ya Kiingereza ingia uisome:

 
Kuna mambo yanapotokea tunategemea viongozi wetu wayasolve bila kuwakwaza raia kwa kufuata misingi ya sheria.

Kwa mfano hapo ilikuwa very simple, huyo aliyewauzia familia nyama ya kitimoto na amejulishwa kuwa amekosea then lilikuwa swala la kumalizwa serikali ya mtaa kwa kusuluhisha na kufidia gharama na wazazi kuwa makini wanapowatuma watoto.

Lakini pia, ilikuwa ni swala la kuhoji kama hayo maduka yana exists mitaa hiyo it means biashara ipo. Haiyumkiniki mfanyabiashara afungue duka manzese halafu wateja watoke kigogo, big no, wateja wapo mitaa hiyo.

Kitendo cha hicho kikundi kuvamia maduka haya na kuamua kuyavunja ni uvunjaji wa sheria za nchi na ni ukorofi dhidi ya raia. Elimu ni muhimu sana kutolewa na kuelimisha raia kutambua mipaka na kujua tofauti ya imani, dini na sheria za nchi zinazolinda maisha yetu ya kila siku.

Tukiruhusu kila mtu afanye vile akili, matakwa yake anapenda au kufuata mlengo fulani na kulazimisha wengine wafuate kwasababu tu anahisi yeye ni sahihi then tunafanya kosa kubwa sana kuwaza hivyo.....

Hili ni taifa, linamiiko, sheria, kanuni na taratibu ambazo viongozi, raia, na makundi ya itikadi na milengo tofauti wanapaswa kufuata. Kama unaona hii inchi haielekei kule unataka then why uingie gharama ya kutaka kutumia nguvu kubadili watu wote wafananie na wewe, kwann usihamie pale panapofanania na mitazamo yako ambayo uaniona halali.

Kukosa hekima, busara na uelewa ni tatizo kubwa sana miongoni mwa raia.
 
Samcezer, nakubaliana nawe kwamba masuala mengine yanaweza kumalizwa bila ya kuleta vurugu wala bughudha kwa watu

Lakini kuna kiburi na dharau cha baadhi ya watendaji wa serikali. Hii husababisha migongano isiyo ya lazima kwa wananchi. Pamoja na kwamba mwenye bucha aliona pale ndio kwenye biashara lakini sheria ndogo(by laws) za Manispaa zinakataza hilo

Hii inanikumbusha kwa mfano wakati wa upangaji wa miji ya Kibada, Kisota(Kigamboni) na Mbweni ambapo palipimwa viwanja 20,000 vya makazi na shughuli mbali mbali kulikua na maeneo yaliyopangwa kama sehemu za ibada bila ku specify eneo lipi ni kwa ajili ya ibada ya watu wa imani ipi.

Matokeo yake maeneo karibia yote yanayoitwa ya ibada yalichukuliwa na watu wenye imani moja maana inasemekana wao ndio walianza kupata taarifa ya kugaiwa viwanja kwa bei ndogo ya Serikali kabda ya taarifa rasmi kutolewa kwa umma! Katika hali ya kawaida watendaji wa mradi walitakiwa waainishe kwamba eneo fulani ni kwa ajili ya nyumba za ibada za imani fulani kama wanavyofanya kwenye upangaji wa makaburi ili kuweka uwiano mzuri na wa haki kwa jamii.

Sura iliyopo sasa ni kwamba katika maeneo hayo yaliyopimwa baada ya wakazi wake kunyang'anywa ardhi zao kwa fidia ndogo sana(yalichukuliwa kabda ya sheria mpya ya ardhi) kume tamalaki nyumba za ibada za imani moja tu na ukiona kuna nyumba ya ibada ya imani tofauti basi ujue ni mtu kaamua kujitolea kiwanja/viwanja vyake kwa ajili hiyo!

Ni vyema watendaji wa serikali katika ngazi zote wafanye kazi kwa uadilifu na kutenda haki kwa watu wote ili kuendeleza utangamano wa kitaifa
 
Ndahani,
Umezungumzia mgawanyiko ndiyo nasema ume- "assume."

Fanya utafiti ili ujue ukweli.

Mzee unalazimisha sana Baadhi ya mambo yawe kama unavyotaka wewe. Ukiongea na wapambe wako kadhaa, Haina maana tafiti wako una mashiko. Siku zote unasukumwa na agenda sadikika.

Dini hizi zinatupa changamoto sana, ila kama mimi na wewe tulivyokuja na tutakwenda, zenyewe zitaendelea kubaki kama zilivyo. Hakuna atakayezifuta.

Ukiwa unaongelea Tanzania, hebu acha dhana kwamba dini yako tu ndio inayoonewa. Nani ameionea? Eti Nyerere! Unajua Nyerere aliondoka madarakani lini.

Aliyemfuata ikawaje? Yeye hakufanya dhuluma za kidini?
Tanzania ni zaidi ya Imani ya dini moja. Nina hakika ipo siku utagundua unayofanya hayatakaa kutokea
 
Sesten,
Hiyo hapo chini ni pp nilitoa Kenyatta University kuhusu Sheikh Kassim Juma na Mabucha ya Nguruwe:

http://mohamedsaidsalum.blogsp...h?q=sheikh+kassim+juma&m=1
 
Shukran ila naomba uitume tena link Sheikh
Sesten,
Hiyo hapo chini ni pp nilitoa Kenyatta University kuhusu Sheikh Kassim Juma na Mabucha ya Nguruwe:

http://mohamedsaidsalum.blogsp...h?q=sheikh+kassim+juma&m=1
 
Mimi utaniita wapi[emoji16][emoji16]joking
 
Sijaokota chochote hapa zaidi ya udini na uharo.
 
Suala la kuchanganya nyama kwa mteja leo ndio nalisoma humu baada ya mdau mmoja ku share nasi; napata shida sana kukubaliana nae au kumkatalia cause wakati ile issue inatokea, hili halikua moja ya malalamiko yaliokwepo. Shida moja ya Historia you can cook the way you like. Baadhi ya hao vijana aliowataja ambao walishiriki uvunjaji wa hayo mabucha walikua wanaishi TEMEKE huko, sasa issue imetokea Manzese, huyu wa Temeke inamuhusu nini? Ambacho nakubaliana na huyu jamaa aliyezungumza kuhusu "mchanganyiko wa hiyo nyama" na hiki; je was it busara kua na maduka ya nyama ya kiti moto pamoja na nyama za wanyama wengine sehemu moja? Hili jambo ni uzembe kabisa wa serikali, uzembe kama uliosababisha kifo cha Akwirine kwa uchaguzi wa ubunge Kinondoni, the same. Sema tu serikali huwezi kuishtaki but mauaji mengine yanatengenezwa na serikali yenyewe.
 
... kati ya maamuzi muhimu ya kitaifa yaliyowahi kuamuliwa kwa hekima ya hali ya juu ni hili la Rais Mwinyi kuamua suala la uvunjaji wa bucha za nguruwe Dar-es-Salaam; ulikuwa uamuzi wa level ya "Hekima ya Sulemani"! Kwamba "anayetaka kula (chochote) ruksa, na asiyetaka ruksa"; haya yalikuwa maamuzi neutral sana na ya hekima yasiyoegemea upande wowote labda kwa wale ambao always walijiona kuonewa pengine wangependa kuona kauli ya Rais ikiwa-support directly lakini ilikuwa kinyume na matarajio yao!

Pili, majaabu yaliyotokana na uhuni ule ni kwamba kwa tukio lile nguruwe alipata daraja ya juu sana sio tu Dar bali nchini kote; ndio ikawa mwanzo wa hafla za "kiti moto" mtaa kwa mtaa nchini kote na hata maelfu kwa maelfu ya wale wengine wanashiriki hafla hizo nchini kote! Vijana wengi wakajiajiri, wakulima wakapata kipato, na watanzania kwa ujumla wakapata lishe.

Sina hakika kama wale jamaa walifanya tathmini kuona kama uamuzi wao ule ulikuwa na +ve au -ev effects! Labda Mzee Mohamed Said atakuwa na matokeo ya utafiti atujuze.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…