Ahsante kwa kunikaribisha kwenye mjadala ingawaje sina mengi sana ya kuchangia kwa sababu wakati ule bado nilikuwa kijana mdogo tu... ndo kwanza nilikuwa nimeanza Form I.
Hata hivyo, si kwamba nilikuwa kijana mdogo kama walivyo vijana wadogo wengi wasiopenda kufuatilia kinachoendelea nchini na duniani kwa ujumla, manake, moja ya mambo ambayo nilikuwa nawashangaza sana watu pale nyumbani na mtaani ilikuwa ni tabia yangu ya kupenda kusikiliza BBC, station ambayo ilionekana kama ni ya watu wazima na sio watu wa rika langu!
Lakini kwa upande mwingine, nimekulia kwenye kota za polisi... kwa maana nyingine, ingawaje sikuwa mkubwa sana lakini sikutoka kapa moja kwa moja kuhusu kilichokuwa kinaendelea kwa sababu kwa upande mmoja nilikuwa mtoto wa BBC, na kwa upande mwingine, nilikuwa nashuhudia kwa macho yangu harakati za polisi baada ya lile tukio!!!
It's a mess!!!
Sifahamu ni nini hasa kiliwapelekea baadhi ya Waislamu kuvamia mabucha ya nguruwe ingawaje utetezi ulikuwa kwamba, wao kama wao hawakuwa wakipinga uwepo wa hizo bucha bali walikuwa wakipinga uwepo wa bucha hizo kwenye maeneo yenye mchanganyiko wa watu, huku mengi yake yakiwa kwenye maeneo yanayokaliwa na Waislamu wengi hapo Magomeni na Manzese, huku wakidai hiyo ilikuwa ni kinyume hata na sheria zenyewe (bila shaka za mipango mji), na wakazi wa huko walipojaribu kulalamika, serikali iliwapuuza na ndipo watu wakachukua sheria mkononi!
Nakumbuka siku anayoisema Mohammed Said hapo juu, nilikuwa naenda pale Central alipokuwa Bi Mkubwa hata hivyo kufika Posta ya Zamani nililazimika kugeuza manake Posta yote ilikuwa imetanda magari ya polisi waliobeba silaha za kivita!
Uzoefu wangu wa kuishi Kota za Polisi haukusaidia kunipa ujasiri wa kutowaogopa polisi wale manake ilikuwa ni kama Uwanja wa Vita!!
Huyo Sheikh Kassim Bin Juma sie wengine ndo tulianza kumfahamu kupitia tukio hili! Na kama kumbukumbu zangu zipo sawa, movement mzima ilikuwa inaendeshwa na BALKUTA iliyokuwa chini ya Sheikh Yahya Hussein.
Sina uhakika wa uhusiano wa Sheikh Kassim na BALKUTA lakini nisicho na shaka nacho ni ushawishi wake mkubwa aliokuwa nao pale Msikitini kwa Mtoro!
Hii BALKUTA ilikuwa mwiba mkali kwa serikali... cjui ilifia wapi lakini nadhani ilipigwa ban na serikali, manake kwa jinsi ambavyo ilikuwa na ufuasi mkubwa hususani wa vijana, I doubt kama ingeweza kufa yenyewe!
Bila shaka
Mohamed Said atakuwa analifahamu vizuri hili suala na kuweka kumbukumbu isiyo shaka sawa! Na kama kweli ilifutwa na serikali basi sina shaka moja ya taasisi ambazo zilifanya sherehe kutokana na kufutwa huko basi ni BAKWATA ambayo wakati ule ilikuwa chini ya Sheikh Hemed bin Juma bin Hemed!!
BAKWATA ilikuwa inanyimwa sana usingizi na BALKUTA!!
Hizi movements za Sheikh Ponda si lolote si chochote mbele ya BALKUTA manake hata mapinduzi kwenye misikiti ili kuondoa ma-Imam wa BAKWATA, kama sikosei movement za aina hiyo ziliasisiwa na BALKUTA, na kufutwa kwa BALKUTA ndiko kukaja kuibua akina Sheikh Ponda!!
Anyway, kilikuwa ni kipindi kigumu sana kwa Tanzania, hususani Dar es salaam!!!