Uchaguzi 2020 Maandamano ya tarehe 2 Nov: Je, Ni Demokrasia au waliokosa wanapigania Maslahi Binafsi?

Uchaguzi 2020 Maandamano ya tarehe 2 Nov: Je, Ni Demokrasia au waliokosa wanapigania Maslahi Binafsi?

jijiletublog

Member
Joined
Jul 23, 2020
Posts
31
Reaction score
74
Tarehe 31 Oktoba tumeshuhudia kuitishwa kikao cha waliokosa nafasi mbalimbali za ubunge na urais ili kutangaza kufanya maandamano siku ya tarehe 2/11/2020. Tangu kuanzishwa kwa uchaguzi wa mfumo wa vyama vingi mwaka 1995, vyama vya upinzani havijawahi kukubaliana na matokeo katika kila sehemu walizoshindwa. Kwa miaka ya nyuma viongozi wa juu wa vyama vya CHADEMA, CUF na ACT-Wazalendo walizoea kushinda na kurudhika na matokeo huku wakisaini malipo ya mishahara na posho za ubunge kila mwezi bila kujali majimbo ambayo wengine walipoteza katika vyama vyao.

Sote tunafahamu kuanguka kwa wenyeviti wa vyama kama Zitto Kabwe na Freeman Mbowe kumekuwa na mshtuko kwa watanzania kutokana na umaarufu na umashuhuri walionao kwa taifa lakini sio suala linalowashangaza wapiga kura katika majimbo yao kutokana na hali ya ushawishi wao ilivyopungua huko majimboni.

Suala tunalotakiwa kujiuliza juu ya uamuzi wa kuandamana, Je! Tunaandamana kwa lengo la kutafuta demokrasia au tunatumia kivuli cha demokrasia kutetea maslahi binafsi ya viongozi wa vyama vilivyoanguka? Ni kwa nini picha za mauaji yaaliyotokea nchi nyingine zitumike kuidanganya umma wa watanzania na jumuia za kimataifa kuwa mauaji haya yanatokea Tanzania? Majibu ya maswali haya yanatupekea kuamini kuwa nia si demokrasia bali ni maslahi binafsi.

Tukumbashane tu nchi ya Marekani na Kenya ndizo zimekuwa vinara wa ufutiliaji na ukosoaji wa uchaguzi huu. Taasisi kama FICHUA TANZANIA na TANZANIA ELECTION WATCH zimeonyesha kuwa na usajili kutoka serikali ya Kenya na ndizo zimekuwa zikiongoza mashambulizi dhidi ya ushindi wa CCM.

Sababu kubwa ambayo watanzania wanatakiwa kuielewa ni maslahi binafsi ya nchi kama Kenya na USA. Itambulike kwamba kuna vita kubwa kiuchumi na watu hawa wanaopanga kuandamana wamekuwa wakitumika kwa muda mrefu ili kuuza nchi yetu kwa ajili ya uchu wa madaraka na maslahi binafsi kwani wamekuwa wakipokea fedha nyingi ili kufanikisha vurugu kupitia mitandao ya kijamii. Kwa muda wa miaka mitano, Tanzania chini ya uongozi wa Magufuli, imeshuhudia mtazamo wa nchi kujitegemea kiviwanda na mikakati ya ujenzi wa miundombinu wezeshi kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda imekuwa sumu kwa taifa la Kenya kwa sababu Tanzania imekuwa mnunuzi mkubwa wa bidhaa kutoka Kenya. Uwekezaji wa viwanda Tanzania ni mwiba kwa viwanda vya nchi hiyo.

Kwa upande wa Marekani (USA), sera ya demokrasia hutumika kama njia ya kuingilia kwenye nchi nyingi lakini kwa undani huwa ni maslahi ya kiuchumi na uwezo wa kutawala nchi za Africa. Suala kubwa ni kuvunjwa kwa mkataba mbovu wa SYMBION chini ya utawala wa Dr. John Magufuli. Hali hii imepelekea USA, kupiitia Balozi wake nchini Tanzania Dr. Donald J. Wright, kutumia mwamvuli wa demokrasia kuchafua serikali ya Tanzania baada ya kufuta mkataba huo. Katika mkataba huu tuliibiwa zaidi ya bilioni 6 kila mwezi na kuuziwa umeme kwa gharama kubwa sana. Watu kama MANGE KIMAMBI kupitia account za mitandao ya kijamii wa INSTAGRAM na GOODLUCK HAULE, KIGOGO2014, FATMA_KARUME, HILDERNEWTON21, JJMNYIKA kupitia account ya TWITTER ndio wamekuwa wakitumiwa sana kuhakikisha wanaharibu amani na kuchafua jina la Tanzania ndani na nje ya nchi.

Ikumbukwe kuwa vurugu za nchini Libya zilianza kwa maandamo ya kile kilichotajwa demokrasia lakini baadae mataifa makubwa yakiongozwa na marekani yalivamia kijeshi kupitia nafasi ya vurugu zilizoanzishwa na walibya wenyewe. Muda mfupi baadaye, uzalishaji wa mafuta ulishuka kwa kasi kutoka katika nchi iliyokuwa na hazina kubwa ya mafuta Africa na kuifanya nchi yenye uchumi unaosuasua ukiambatana na vita kabla ya Marekani kurudi na kukiri kufanya makosa katika uvamizi huku wakiiacha nchi wa Libya ikiendelea kuangamia kutokana na madhara ya vita hivyo.

Hali itakuwa hivyo Tanzania endapo tutawafuata wanaotaka kuandamana kwa maslahi binafsi.

Ukisikiliza kampeni zilivyokuwa zikiendeshwa kwa upande wa vyama vya upinzani, mtakubaliana na mimi kuwa mgombea wa CHADEMA alipanga kuandaa maandamano kwa kuwa alijua hawezi kushinda. Mara kadhaa amekuwa akihubiri kuwa iwe kwa amani au kwa vita anataka kushinda uchaguzi huu.

Hii iliashiria malengo ya kuharibu amani tangu siku ya kwanza. Ikumbukwe tu katika mpango huu, hata kama Jeshi halitaingilia kati, Vikundi maalumu vya CHADEMA na ACT-Wazalendo vimeandaliwa ili kuanzisha vurugu na kuwapiga waandamanaji wenzao ili kuonyesha jamii ya kimataifa kuwa Tanzania kuna vurugu. Tuepuke hili kwa nguvu zote ili kuondoa maslahi binafsi ya Freeman Mbowe, Maalim Seif, Tundu Lissu na Zitto kabwe.

Ifahamike tu kuwa Robert Amsterdam, mwanasheria na wakili wa Tundu Lissu, ambaye kwa sasa yupo Uturuki baada ya kuondoka aliwekwa kwa ajili ya kuhakikisha anafanikisha zoezi la kuleta vurugu na kuiacha Tanzania katika mazingira ya sintofahamu kabla ya mataifa makubwa kuingia na kuiba mali za nchi hii kupitia vita.

Niwapongeze watanzania kwa kutokubaliana na mkakati huu wa mataifa makubwa. Niwakumbushe tu huu ni wakati wa kuwaonyesha mabeberu namna watanzania tulivyo na umoja na tunavyoweza kuamua masuala yetu wenyewe bila kuwategemea wao ambao wanatuletea masharti ya ushoga na kutuibia malighafi kwa kigezo cha kupigania demokrasia.
 
Chadema ni wahuni na wapumbavu [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Ninyi jamaa "Mwalimu Nyerere alipata Sema "ukizoea kula nyama ya mtu hutaacha "mumekula uchaguzi wa serikali za MiTAA mkaona Tamu sasa mumenogewa mnakula uchaguzi Mkuu hatua ya tatu mtakula Nyama za watu ".

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Hiyo demokrasia imekosekana baada ya wabunge nguli wa upinzani kukosa nafasi ya uwakilishi bungeni? Kwanini wasingegoma kushiriki uchaguzi ambao unaonekana sio huru na haki?

Hapo wanateteta ugali,ni vyema waandamane wao na familia zao,kwenye posho ,mishahara na malupulupu wanakulaga na wananchi ?

Kuna vijana hawana ajira toka 2015 ,mbona hawakuitisha maandamano ili kufosi wapate ajira.
Zamu yao sasa na wao waangalie mambo mengine,waone utamu wa kijiweni.wajiajiri sasa.
 
Najiuliza tu hivi kwa jinsi Chadema ilivyo kama kweli wangemkamata mwana ccm akiwa na begi la kura feki wangemuacha salama kweli? Kama tu sasa hivi wanadiriki hata kutumia picha za mauaji ya nchi nyingine kutaka kuaminisha umma kuwa Tanzania kuna mauaji makubwa je wangeshindwa hata kumpiga picha mwanaccm au polisi au mtumishi wa tume ya uchaguzi aliyekutwa na kura feki?

Chadema wanaprint kura feki halafu wanajifanya wamezikamata, ili aliyekamatwa nazo hawamuoneshi na wala hawamchukulii hatua zozote. Wanaenda mbali na kukimbilia kuzichoma kura ikiwa ni kidhibiti cha ushahidi wao. Hawa jamaa wanatufanya watanzania watoto na mazoba wa kiwango cha juu.
 
Hapo ni maslahi binafsi. Mbona serikali za mitaa waliacha lipite? Halafu eti wanazuia wake wabunge wasiende kuapa. Mbowe acheni ubinafsi. Waacheni walioshinda waende. Nyie mliokatwa piganieni haki huku nje.
Kwenye serikali za mitaa mliwatoa wenzenu mhanga kwa sababu nyie mlikuwa hamgombei. Sasa yamewakuta mnalia lia.
 
Hiyo demokrasia imekosekana baada ya wabunge nguli wa upinzani kukosa nafasi ya uwakikishi bungeni? Kwanini wasingegoma kushiriki uchaguzi ambao unaonekana sio huru na haki?
Hapo wanateteta ugali,ni vyema waandamane wao na familia zao,kwenye posho ,mishahara na malupulupu wanakulaga na wananchi ?
Kuna vijana hawana ajira toka 2015 ,mbona hawakuitisha maandamano ili kufosi wapate ajira.
Zamu yao sasa na wao waangalie mambo mengine,waone utamu wa kijiweni.wajiajiri sasa.
 
Aagh!! Sawa waende haohao wenye shida ya ubunge. Wananchi wameshaamua fullstop na kesho kama wananchi hawataandama itakuwaje?
 
Bro me nakuaminia, inyeshe mvua liwake jua, kesho ni kesho,
Sema nini? siache kutupia picha za maandamano hiyo kesho.
Hatuandamani ili kupiga picha. Tunaandamana ili kupinga udhalimu. Vyovyote vile, ni lazima kama binadamu tuliopewa akili na Mungu tupinge udhalimu kwa namna zote.
 
Kama ni hivyo kesho maandamano yatatamalaki,mkiona kimya mjue ndio hivyoo hampendwi na wananchi.
 
Back
Top Bottom