Maandamano ya vijana Kenya yamepoteza uelekeo na hayana maana tena

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Vurugu, uharibifu na uporaji wa maduka na mali mbalimbali binafsi na za umma vimewafanya kuonekana na kuwabainisha rasmi mchana kweupe, kumbe ni majambazi, magaidi na wezi tu, waliyo jificha kwenye kudai eti miswada wa fedha wa Serikali ya Kenya kwa mwaka 2024/2025 ni mbaya na haufai. kumbe wao ndio wabaya, waharibifu na hawafai na wamethibitisha walivyo kwa vitendo kabisa leo hii.

Bila shaka, hasara ya miundombinu na yakiuchumi waliyo isababisha vijana waandamanaji,
ni dhahiri itachochea ulinzi na usalama kuimarishwa pande zote Kenya, wafanyabishara na serikali wataungana, kukabiliana vilivyo na kwa nguvu zote na mabandits hawa ili wasije kusababisha uharibifu zaidi.

Naamini serikali madhubuti sana ya Dr. William Samoe Arap Kipchirchiri Ruto haitaruhusu wala kuvumilia tena uharibifu zaidi ya uliotokea leo. na muandamanaji atakae jitokeza kuandamana tena atadhibitiwa na kuwajibishwa vilivyo kwa mujibu wa sheria za Jamuhuri ya Kenya.

Heko na kongole nyingi sana kwa maafisa usalama wa kenya kwa weledi wao na umakini mkubwa katika kusimamia usalama wa waandamanaji vijana.

Waandamanaji wachache waliopata majeraha mabaya, ni katika purukushani na harakati za wao kwa wao kupora, kuiba bidhaa na mali mbalimbali kwenye ma supermarkets waliyoyavunja na kukimbia kiholela. na wale wachache waliogongana bahati mbaya katika uporaji huo ndio hao wamejeruhika.

Nawapa pole sana wote, lakini mmekosea sana vijana, na mmepoteza lengo.

Mungu Ibariki Jamuhuri Ya Kenya na Amani :pulpTRAVOLTA:
 
Bidhaa zote zinazotoka kenya zilipanda kwa asilimia kubwa tangu mwezi wa tatu
Je sasa itakuaje??? Baada ya kupitishwa mswaada mpya?
Tuna import mpaka vifungashio vya ubuyu kenya
Unalijua hilo wewe chawa
Unajua tanzania hakuna kitu kinaitwa icing sugar yote yatokea kenya
……
Punguza uchawa #kenya hauhitajiki
 
Vurugu, uharibifu na uporaji wa maduka na mali mbalimbali binafsi na za umma vimewafanya kuonekana na kuwabainisha rasmi mchana kweupe, kumbe ni majambazi, magaidi na wezi tu, waliyo jificha kwenye kudai eti miswada wa fedha wa Serikali ya Kenya kwa mwaka 2024/2025 ni mbaya na haufai. kumbe wao ndio wabaya, waharibifu na hawafai na wamethibitisha walivyo kwa vitendo kabisa leo hii.

Bila shaka, hasara ya miundombinu na yakiuchumi waliyo isababisha vijana waandamanaji,
ni dhahiri itachochea ulinzi na usalama kuimarishwa pande zote Kenya, wafanyabishara na serikali wataungana, kukabiliana vilivyo na kwa nguvu zote na mabandits hawa ili wasije kusababisha uharibifu zaidi.

Naamini serikali madhubuti sana ya Dr. William Samoe Arap Kipchirchiri Ruto haitaruhusu wala kuvumilia tena uharibifu zaidi ya uliotokea leo. na muandamanaji atakae jitokeza kuandamana tena atadhibitiwa na kuwajibishwa vilivyo kwa mujibu wa sheria za Jamuhuri ya Kenya.

Heko na kongole nyingi sana kwa maafisa usalama wa kenya kwa weledi wao na umakini mkubwa katika kusimamia usalama wa waandamanaji vijana.

Waandamanaji wachache waliopata majeraha mabaya, ni katika purukushani na harakati za wao kwa wao kupora, kuiba bidhaa na mali mbalimbali kwenye ma supermarkets waliyoyavunja na kukimbia kiholela. na wale wachache waliogongana bahati mbaya katika uporaji huo ndio hao wamejeruhika.

Nawapa pole sana wote, lakini mmekosea sana vijana, na mmepoteza lengo.

Mungu Ibariki Jamuhuri Ya Kenya na Amani :pulpTRAVOLTA:
Umetumwa na ubalozi wa Kenya.
Hata hivyo umefikisha ujumbe vyema
 
Back
Top Bottom