Maandamano ya Watanzania nchini Marekani wakati wa ziara ya Rais Samia; Je, suala la Katiba Mpya ni muhimu kwa Taifa letu la Tanzania!?

Nilijua utasahau kuweka namba ya simu usubiri teuzi sasa
 
Halikwepeki, watu wanataka serikali inayowajibika wa wananchi, bora enzi za mwendazake vitu vilikuwa havipandi bei ovyo.
Samia na ENABLERS wake lazima mjue kuwa hayo matembezi yenu huko nje mkitafuta mtaji wa kuifungua nchi hautafakiwa bila ridhaa ya wananchi ambao hivi sasa wanaamini kuwa bila katiba waitakayo wao hawawezi kupata maendeleo!!
Kuichelewesha katiba ni kulea ufisadi! Na ufisadi hauleti maendeleo kwa wananchi.
 
Mbona unaturudisha nyuma? Unajua rejea za Tume ya Jaji Warioba? Unauliza maswali bayo majibu yake yalikwishapatikana miaka mingi.
 
Nyumba za maboksi zikoje?

Amandla...
Kama watanzania katiba ni muhimu sana maana ndo njia pekee ya kuilinda nchi yetu bila kutumia mizinga tusiwaamini sana wanasiasa tuiamini mifumo iliyowekwa katika katiba sio kwa katiba tulionayo sasa
 
Tatizo la watanzania kwa sasa sio katiba walioratibu hili zoezi wamekosea sana yaani mtu yupo Marekani eti katiba yetu ndio tatizo lake kuu, hapa ndio naamini mpinzani wa mwenye kujenga hoja kulinga na wakati alikuwa Dr Slaa pekee. Hivi kweli wapinzani wanaamini kwamba kwa sasa wakidai katiba ndio watapata uungwaji mkono na wananchi waliobize na kutafuta mlo wa kila siku na kupambana na gharama za maisha?
 

Dawa ya kupambana na ugumu wa maisha ni kuondoa ufisadi uliokithiri nchini na hilo haliwezekani bila kuwa na mifumo mipya itakayoainishwa na Katiba Mpya!!
 
nina amini kuwa hatutakiwi kuwa na katiba, na kama tuna takiwa kufanya hivyo basi wananchi ndio waamue... wapo wasio taka katiba na wapo wanao taka katiba. isiwe tuna amuliwa na kupewa ambacho si hitaji la wananchi

wananchi wahusishwe wapige kura na kura nyingi zitoe maamuzi tuyafate... na sio kelele za wanasiasa, bali wanasiasa wana takiwa kutusikiliza sisi tunacho hitaji

na kwa kuwa tuna toka ktk mitazamo tofauti ndio maana nashauri kuwe na kura ya maoni (maamuzi) yenye kuwa njia kuelekea swala husika

na sio vikundi vya watu wachache wahamue maswala ya watu wengi... kanuni inasema wengi wape na wachache wasikilizwe...
 
Ni Nani wa kuwasemea hao wananchi kama sio hao hao unaowaita wanasiasa?? Na hata wapingaji wakubwa wa Katiba Mpya ni hao hao unaowaita wanasiasa.
 
Katiba mpya ni muhimu kabisa. Actually niseme mfumo mpya wa utawala kwani huu uliopo umeshindwa kabisa. Ona karne ya sasa tunakuwa na rais anayeamini maendeleo ya nchi yetu yataletwa na watu wa mataifaifa mengine ambao anawaita wawekezaji. Mama ameshajikatia tamaa kabisa anabaki kuzurura bila mpango huku na huko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…