Maandishi ukutani

Maandishi ukutani

Kwa wasioelewa kunena Kwa lugha za Mbinguni wanenazo walokole,

Wajue kuwa mene mene tekel na peresi ni kuandika Kwa lugha ya Mbinguni.

Utasikia mlokole anarudia riririririririri, Unadhani anasema neno Hilo Hilo, kumbe anatamka vitu tofauti vingi na sentesi kamili Kwa codes Ili masikio msielewe Siri za Mbinguni.

Mene Mene- Tafsiri yake ni kuwa Ufalme wako umepimwa na umepunguka.

Lakini asomaye ukutani aliona maneno mawili tu mene mene na asielewe Kisha akatafuta mfasiri.

Ushauri: Ni muda muafaka, Wafalme wa Dunia kuwa na Manabii waliookoka Ikulu Ili kuwafungulia codes Wafalme ndoto waotazo, au waonapo maono Ili kuongoza Nchi Kwa ufasaha.

NB a uzuri ni kuwa, Danieli tayari yumo ndani ya palace.

Anyway,

HATOGOMBEA!!
 
Nawajibika na andiko langu siwajibiki na tafsiri yako

Mwenye hatia hukimbia hata asipokimbizwa

Nimenukuu kama ilivyoandikwa..

Neno mene mene tekel upharsin linaonekana katika Danieli 5, pamoja na tafsiri yake. Baadhi ya tafsiri hutamka upharsin kama parsin. Maneno hayo yalionekana ukutani katika jumba la mfalme Belshaza, kaimu mfalme wa Babeli. Anarejelewa kuwa “mwana wa Nebukadreza (Danieli 5:18, 22), ingawa hakuwa mrithi wa karibu wa Nebukadneza (Yeremia 52:31). Simulizi la Biblia la mwonekano wa kustaajabisha na wenye kuogopesha wa usemi mene mene tekel upharsin umetokeza usemi wa kisasa “mwandiko ukutani,” unaomaanisha “ishara au onyo la msiba usioepukika.”

🙏🏿🙏🏿🙏🏿😀 nikikumbuka hii mada yako huwa nacheka sana.. Anyway nimeokoka sasa sifanyi ulozi tena

Thread 'Mshana Jr, agent wa Shetani JF?' Mshana Jr, agent wa Shetani JF?
Baada ya maneno Yale na tafsiri kutolewa,

Unabii Ule ulitimia usiku Ule Ule na Belshazzar yalimkuta ya kumkuta na shamba likaenda Kwa Jirani.

Sasa ni muhimu kuyaangalia haya mapema ,maana tathmini ya mgombea sahihi wa chama kile hufanyika mwishoni my wa mwaka huu.
 
Maandishi Ukutani
1 Mfalme Belshaza alifanya karamu kubwa kwa ajili ya maelfu ya wakuu wake na akanywa mvinyo pamoja nao. 2 Wakati Belshaza alipokuwa akinywa mvinyo wake, aliamuru viletwe vile vikombe vya dhahabu na fedha ambavyo Nebukadneza baba yake alikuwa amevichukua kutoka hekaluni huko Yerusalemu, ili mfalme na wakuu wake, wake zake na masuria wake waweze kuvinywea. 3Kwa hiyo wakavileta vile vikombe vya dhahabu ambavyo vilikuwa vimechukuliwa kutoka Hekalu la Mungu huko Yerusalemu, naye mfalme na wakuu wake, wake zake na masuria wake wakavinywea. 4 Walipokuwa wakinywa mvinyo, wakaisifu miungu ya dhahabu na fedha, ya shaba, chuma, miti na mawe.
5Ghafula vidole vya mkono wa mwanadamu vilitokea na kuandika juu ya ukuta, karibu na kinara cha taa ndani ya jumba la mfalme. Mfalme akatazama kitanga kilivyokuwa kikiandika. 6 Uso wa mfalme ukageuka rangi, naye akaogopa sana, kiasi kwamba magoti yake yaligongana na miguu yake ikalegea.
7 Mfalme akawaita wasihiri, wanajimu na waganga waletwe, naye akawaambia hawa wenye hekima wa Babeli, “Yeyote asomaye maandishi haya na kuniambia maana yake atavikwa nguo za zambarau, na kuvikwa mkufu wa dhahabu shingoni mwake, naye atafanywa mtawala wa cheo cha tatu katika ufalme.”
8 Ndipo watu wote wa mfalme wenye hekima wakaingia, lakini hawakuweza kusoma yale maandishi wala kumwambia mfalme maana yake. 9 Basi Mfalme Belshaza akazidi kujawa na hofu, na uso wake ukageuka rangi zaidi. Wakuu wake wakapigwa na bumbuazi.
10 Malkia aliposikia sauti za mfalme na wakuu wake, alikuja katika ukumbi wa karamu. Akasema, “Ee mfalme, uishi milele! Usishtuke! Usibadilike rangi kiasi hicho! 11 Yuko mtu katika ufalme wako ambaye ana roho ya miungu mitakatifu ndani yake. Wakati wa baba yako, mtu huyo alionekana kuwa na ufahamu, akili na hekima kama ile ya miungu. Mfalme Nebukadneza baba yako, yaani nasema mfalme baba yako, alimweka kuwa mkuu wa waganga, wasihiri, wanajimu na waaguzi. 12 Mtu huyu Danieli, ambaye mfalme alimwita Belteshaza, alionekana kuwa na akili nyepesi, maarifa na ufahamu, pia uwezo wa kufasiri ndoto, kueleza mafumbo na kutatua matatizo magumu. Mwite Danieli, naye atakuambia maana ya haya maandishi.”
13 Hivyo Danieli akaletwa mbele ya mfalme, naye mfalme akamuuliza, “Je, wewe ndiwe Danieli, mmoja wa watu wa uhamisho walioletwa na mfalme baba yangu kutoka Yuda? 14Nimesikia kwamba roho ya miungu iko ndani yako, na kwamba una ufahamu, akili na hekima ya pekee. 15 Watu wenye hekima na wasihiri waliletwa mbele yangu ili kusoma maandishi haya na kuniambia maana yake, lakini hawakuweza kunifafanulia. 16 Basi nimesikia kwamba unaweza kutoa tafsiri na kutatua matatizo magumu. Ikiwa unaweza kusoma maandishi haya na kuniambia maana yake, utavikwa nguo za zambarau na mkufu wa dhahabu shingoni mwako, nawe utafanywa mtawala wa tatu katika ufalme.”
17 Ndipo Danieli akamjibu mfalme, “Waweza kubaki na zawadi zako mwenyewe na kumpa mtu mwingine zawadi zako. Hata hivyo, nitasoma maandishi kwa mfalme na kumwambia maana yake.
18 “Ee mfalme, Mungu Aliye Juu Sana alimpa baba yako Nebukadneza utawala, ukuu, utukufu na fahari. 19 Kwa sababu ya nafasi ya juu aliyompa baba yako, kabila zote za watu, mataifa na watu wa kila lugha walimhofu na kumwogopa. Wale ambao mfalme alitaka kuwaua, aliwaua; wale aliotaka kuwaacha hai, aliwaacha hai; wale aliotaka kuwapandisha cheo, aliwapandisha; aliotaka kuwashusha, aliwashusha. 20 Lakini moyo wake ulipokuwa na majivuno na kuwa mgumu kwa kiburi, aliondolewa kutoka kwa kiti chake cha ufalme na kuvuliwa utukufu wake. 21 Akafukuzwa mbali na wanadamu na kupewa akili ya mnyama, akaishi pamoja na punda-mwitu, akala majani kama ngʼombe, nao mwili wake ukaloweshwa kwa umande wa mbingu, mpaka alipotambua kwamba Mungu Aliye Juu Sana ndiye mtawala juu ya falme za wanadamu na kwamba humtawaza juu yao yeyote amtakaye.
22 “Lakini wewe mwanawe, ee Belshaza, hukujinyenyekeza, ingawa ulifahamu haya yote. 23 Badala yake, umejiinua dhidi ya Bwana wa mbingu. Uliletewa vikombe vya Hekalu lake, nawe na wakuu wako, wake zako na masuria wako mlivitumia kwa kunywea mvinyo. Ukaisifu miungu ya fedha na dhahabu, ya shaba, chuma, miti na mawe, miungu ambayo haiwezi kuona, au kusikia wala kufahamu. Lakini hukumheshimu Mungu ambaye anaushikilia uhai wako na njia zako zote mkononi mwake. 24Kwa hiyo ameutuma mkono ule ulioandika maneno.
25“Haya ndiyo maneno yaliyoandikwa:
mene, mene, tekeli na peresi
26 “Hii ndiyo maana ya maneno haya:

“Mene: Mungu amezihesabu siku za utawala wako na kuukomesha.
27 Tekeli: Wewe umepimwa katika mizani na umeonekana umepungua.
28 Peresi: Ufalme wako umegawanywa na kupewa Wamedi na Waajemi.”

29 Ndipo kwa amri ya Belshaza, Danieli akavikwa nguo za zambarau na mkufu wa dhahabu shingoni, tena akatangazwa kuwa mtawala wa tatu katika ufalme.
30 Usiku ule ule, Belshaza mfalme wa Wakaldayo akauawa, 31 naye Dario Mmedi akashika ufalme akiwa na miaka sitini na miwili.
Iliyochaguliwa sasa
Danieli 5:
Danieli 4 | Biblia NEN | YouVersion
Danieli 6 | Biblia NEN | YouVersion

Umesomeka mtumishi
NAMI nilifimuliwa na Nimeamdika humu, ya kuwa Kuna lidudu tangu 1961 baada uhuru na baada ya tambiko hili dude limekuwa likubwa mno limeshoba damu za watu Toka enzi, katika ulimwrngu huu wa mwili na nyama ni ngu kuliondoa au kuliua

Nimefunuliwa kuwa njia ya kuliondoa ni kuanza kiroho kwa watumishi wakiungana nchi nzima kufunga siku 40; huku wakiomba ndo njia ya kuliondosha


Ili matokea yaonekane kwenye ulimwrngu wa macho ya mwilini kwa kutishia kuandika katiba mpya then kuanguka kwenye uchaguzi huru

Nawasilisha
 
Hakuna linaloshindikana kwenye kijiji chenye Wazee na Taifa bora lenye msingi wa kikatiba na utawala wa sheria huthamini Utawala Bora na usalama wa Raia....Tuzungumze pamoja na kutafuta suluhisho endelevu la pamoja. Ni tarehe 5 Oktoba pale Ubungo plaza....Tusipozungumza kama wenye hekima tutaangamia kama wapumbavu
20241002_091214.jpg
 
Hakuna linaloshindikana kwenye kijiji chenye Wazee na Taifa bora lenye msingi wa kikatiba na utawala wa sheria huthamini Utawala Bora na usalama wa Raia....Tuzungumze pamoja na kutafuta suluhisho endelevu la pamoja. Ni tarehe 5 Oktoba pale Ubungo plaza....Tusipozungumza kama wenye hekima tutaangamia kama wapumbavuView attachment 3112828
 
1.Unamteka mtoto wa kike kwa mtutu wa bunduki

2.Kundi la wanaume saba wakatili mnakubali kwenda kumteka, kumdalilisha, kumnyanyasa na kutweza utu wa mwanamke kwa ujira wa fedha?

3.Mnafunga kitambaa usoni mwanamke kisha mnamtoa nyumbani kwake Kibiti mnamsafirisha hadi mapori ya Kisarawe kwenda kumnyanyasa na kumfanyia ukatili

4.Mnajitambulisha kuwa ni maafisa wa chombo cha dola kisha mnatumia gari la kodi za wananchi, pingu na bunduki zilizonunuliwa kwa kodi zetu.

5.Mnachana nguo za mwanamke aliyefunzwa kujistiri kwa dini yake safi ya kiislamu tangu utotoni na kumuacha utupu.

6.Mwanamke mmoja anashirikiana na wanaume saba kumshambulia na kumdhalilisha mwanamke mwenzake kwa ujira wa pesa tu

7.Mmemaliza kumfanyia ukatili Mwanamke mnamtekeleza maporini mnaondoka na kujiona wajanja... mnajiona mmeyapatia maisha kweli.

8.Nawakumbusha yupo Mungu juu anayeona kila kitu muda wote na sehemu zote. Ipo siku kabla hamjazikwa na kufukiwa na udongo huu mnaotumia kumwaga damu, mtakumbushwa kila tukio moja mlilotenda.

9.Nawaonea huruma ninyi watekaji na wauaji, kwa kuwa najua hamjui watu makatili kama ninyi mwisho wenu unakuwaga vipi.

10.Lakini niwahakikishie akili za upinzani na harakati hazizimwi kwa mtutu wa bunduki na kufuli la Jela tulifikiri mmejifunza kwa Hayati Magufuli

Hamtoweza kuua watu wote,wapo watakaobaki nyuma yetu,wao watatulipia visasi vyetu.hilo mnatakiwa kulielewa siku zote.

Hakunaga Jambo linafanywa na watu zaidi ya wawili likabakia kuwa siri.
credit: Boni yai Twitter
20241023_051623.jpg
 
Back
Top Bottom