Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 5,628
- 6,411
Ni wakati muhimu sana kutazama aina ya maarifa ya kileo tikihusisha maarifa ya asili kama mpinzani halisi katika vita ya kileo ya maarifa. Maarifa katika zama za hizi yamepokwa na kubebeshwa maslahi ya watu wachache chini ya mwamvuli wa Akili mnemba.
Ladha ya upekee ya ulimwengu, ladha ya kumiliki usio na mipaka imehodhiwa na watu wachache sana waliojipa nafasi ambayo kwa hakika hawana. Uvivu wetu wa kujiangalia ndani " inner engineering" ni janga kubwa la kibinadamu katika zama zetu.
Tuna hazina isiyokoma ya maarifa katika maarifa ya asili na siyo akili mnemba. Sipingani na ukweli kuwa akili mnemba inarahisisha sana utendaji wa kila siku katika zama hizi ila ninapinga milele kuwa nafasi ya utu na kumiliki asilia wa maarifa kupokwa na mifumo hii ambayo kwa hakika imebeba maslahi ya wachache.
Dunia leo inatawaliwa na hofu "negative energy" kutokana na mashaka yanayopaliliwa na wachache kujimilikisha kazi ya utu kupitia utendaji wa Akili mnemba ambao unatazamiwa kupoka shughuli nyingi zinazofanywa na binadamu leo.
Wamesikika wanufaika wa mifumo hii wakisema wazuwazi kuwa miaka mitano ijayo kutakuwa na uwezekano wa shughuli nyingi zinazofanywa na wanadamu kupokwa na mifumo ya akili mnemba, wengine wanatishia kabisa kuachana na kazi katika kuunda mifumo hiyo kwa sababu ya uchangamani wake na uwezo wa kuangamiza watu ndani ya miaka ijayo.
Ni kama tumemuumba mungu wetu na sasa anatutaka tuwe sadaka za kuteketezwa mbele yake. Swali la kujiuliza ni kwa maslahi ya nani?..Nyuma ya Akili unde Kuna maslahi mapana na fiche ya kuutweza utu wa wengi na kuinua utukufu wa watu wachache waliojipa nafasi ya kutawala wengine.
Silaha pekee iliyobaki ni kurudi kwenye misingi yetu ya asili ya maarifa "indigineous knowledge".