Page 94
JF-Expert Member
- Oct 22, 2015
- 5,204
- 15,207
Heshima kwenu Wakuu.
Ikiwa Leo ni siku ya pili ya mwezi wa saba, siyo vibaya tukafanya analysis ya watu walioshika vichwa vingi vya habari humu JF kwa kuzungumziwa sana.
Watu hawa wanaweza wakawa wamezungumziwa kwa mazuri ama mabaya. Wafuatao ni wanaJamii watano waliotikisa sana humu Jukwaani kwa Mwezi June;
1. Joseverest
Huyu ni verified user wa JF. Amekuwa maarufu sana mwezi uliopita. Kilichozidisha umaarufu wake ni kuwa wa kwanza kucomment kwenye nyuzi nyingi, pengine kuzidi MTU yeyote. Hii iliwalazimu baadhi ya members humu kuanzisha nyuzi zaidi ya 6 kuhusu huyu kiungo mchezeshaji wa JF. Kuna wengine walizidisha minong'ono kwa kusema, ni Moderator wa JF katika kitengo cha Content controlling, hivyo hudaka Uzi ukiwa hewani.
Usishangae hata ukakuta yeye ndiye wa kwanza ku-comment katika Uzi huu.
2. Raimundo
Huyo member amekuwa maarufu sana tarehe za mwishoni za mwezi June. Tuhuma zake za kuhusika na utapeli, zimemfanya azungumziwe Sana humu JF. Harakati zake hizi zimesababisha kuzuka kwa neno jipya 'assist'
3. mtu mzito
Kama ambavyo imekua kwa member namba mbili, ndiyo ilivyo kwa huyu. Member huyu anasadikika kufanya utapeli kwa kutoa huruma feki ya Uganga na usafishaji nyota. Hii imekua zaidi baada ya mwanaJamii mmoja kuleta Uzi akiwaasa watu kuwa makini na huduma zake za Uongo.
4. barafu
Huyu ni member mwenye heshima nyingi sana JF. Mada zake zilizoandaliwa kwa umakini, zilizojaza maelezo ya kutosha pamoja na kujua vitu Vingi sana, vimemfanya awe maarufu sana mwezi June. Kutokana na kutawaliwa na mada za maboso/makinikia, mwanaJamii huyu alitisha zaidi alipoleta Uzi akisisitiza mshikamano katika swala la madini, kwani iliwashinda manguli wakubwa akiwepo MJKN.
Watu walienda mbali zaidi na kudai kuwa, huenda barafu asiwe Mtu mmoja bali taasisi kubwa.
5. ONTARIO
Kijana huyu, alianzisha Uzi kuhusu Forex trading. Uzi huo uliamsha ari na matumaini ya wanaJamii katika kuingia katika soko la dunia la ubadilishwaji wa fedha za kigeni. Uzi wake huo ulipata mapokeo makubwa sana na uliwatia watu ari ya kuijua zaidi kwa undani. Project yake pia ya kuanzisha mafunzo kuhusu biashara husika, imemfanya watu wasimsahau katika maandiko humu jukwaani.
Naam,hao ndiyo watu watano waliotisha sana humu Jukwaani. Na wengine, Sana nafasi nzuri ya kuendelea ku-trend kwa mwezi huu.